MENGI NA IPP WanaHUJUMIWA?

MENGI NA IPP WanaHUJUMIWA?

TBC inapomfuata mfanyakazi mmoja na kumshawishi ajiunge nayo, maana yake hawatamfanyia interview. Je, kumuajiri mtu bila usaili sio ukiukwaji wa taratibu za kuajiri watumishi serikalini? Naombeni ufafanuzi.

Hiyo inaitwa "head hunt" na inaruhusiwa kutegemeana na kanuni za kazi za taasisi au shirika husika.
On the other hand wafanyakazi wanaondoka sehemu kama maslahi hayaeleweki na muda mrefu wafanyakazi wa IPP wamekua wakilalamika kuhusu maslahi bila mafanikio. kumbuka kuna mdada fulani alifariki akiwa amefanya kazi ITV/Radio1 kwa muda mrefu lakini hakupata mafao yake!

so its just normal labour turnover phenomena. hakuna hujuma wala nini.
 
Me i concur with the first presenter, i suspect tibisi wanahujumu aitivii ! Ni kweli kuwa bwana mengi amekuwa akipambana na mafisadi na tumeshuhudia...! Kama mnakumbuka kuna hoja ilitaka kupelekwa bungeni katikati ya mwaka huu...ikiwana lengo la kuzuia watu binafsi au mashirika binafsi kuwa na chombo cha habari zaidi ya kimoja...!!! Nazani wadau mnakumbuka...hoja hii ilikuja wakati hoja za mafisadi papa na nyangumi zikiwa motomoto!!! Hapo mnaweza kuona mahusiano yaliyopo! Hvi huyu ra kiburi anatoa wapi?
 
IPP Media kuna ubaguzi. Na hili ndio tatizo lao kubwa. Wacha vijana wakafanye kazi serikalini kwani hiyo ndiyo iliyowasomesha kwa kodi za wananchi na hawakusomeshwa na mengi mpenda sifa.
Pia mjue kuwa ITV inamuonyesha zaidi mengi kuliko hata RAIS wa nchi.
 
Laana za mkewe aliyemtelekeza!mengi hodari wa kuanzisha biashara kisha anachukua mkopo bank kisha anaingia mitini halipi!
 
Mengi amefanya mengi sana kwa taarifa yako wewe bongo lalaa! Umelala kweli...nakumbuka wakati mmoja mengi alikuja kwetu kule kahama shinyanga kuchangia ''' vicoba '' wanawake walifurahi sana wakasifia wakasema serikali imeshindwa kufanya hayo lakini mengi wanampongeza....mengi si sawa na hao mafisadi wenu!!!!!!!!!!!
 
Bravo Mr. Reginald Mengi!!! Tungekuwa na kina Mengi watano wazalendo kama wewe basi nchi hii ingekuwa imesaidia sana wengi. Pamoja na mapungufu yako ya kibinadamau kama ilivyo binadamu wengine but hakuna awezaye kunitenganisha na mzee Mengi. Mzee Mengi amefanya mengi kusaidia wazalendo, ameniwakilisha mimi ambaye pengine ningetaka kusaidia ila mafisadi walishanipunguzia share yangu hivyo siwezi fikisha mkono wangu wa msaada mbali zaidi ya ndugu zangu tegememezi na wale wahitaji wa karibu of my reach. Again Bravo Mzee Mengi, you will be remembered by many, your legacy will live forever, no doubt!!
 
Kila kitu kina pande mbili. Mkikaa hapa kuongelea upande mmoja, kamwe hamtafikia conclusion ya maana.

Yako mengi tu ambayo bwana Mengi ameyafanya, haihitaji kuorodhesha hapa. Lakini pia, yapo mapungufu ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuboresha sura ya mjasiria mali huyu mbele ya jamii:-
  1. Ajira kwa baadhi ya wafanyakazi wake wa vyombo vya habari zina utata. Tukumbuke yule marehemu Rehema aliyefanya kazi kama kibarua kwa miaka mitano.
  2. ITV & Radio One ZIMEDUMAA. Ukiacha Watanzania wachache wanaoangalia na kusikiliza matangazo kwa kutumia satellite dishes, matangazo yake yanapatikana DSM, Arusha mjini, Moshi, Mwanza mjini na Dodoma mjini pekee. Radio Free Africa na Star TV wapo nchi nzima. Anazidiwa kwa sasa na hata Clouds FM, Radio 5, Radio Maria...... Angalau tangu mwaka 1994 tungeona expansion kwenda pembe zote za nchi.
  3. Vyombo vyake vya habari havina uwakilishi nchi nzima. Matokeo yake, habari nyingi za nchini ni kutoka hayo maeneo machache.
 
Back
Top Bottom