Ushauri nasaha kwa Mzee Mengi Watanzania hatuna haja ya kutaka kujuwa Urafiki wake wa karibu na watokea zamani kwa Rais Kikwete sisi hautusaidiii ni yurafiki wenu na mnajuwana wenyewe au mtajuwana wenyewe kwani Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba wahenga walinena. Towa ushahidi Mahakamani wa Mafisadi PAPA nasi tuko Nyuma yako, lakini ikiwa sio kweli umesimama kwa ajili ya Kukashifu wenzako kwa mitizamo ya kiushindani wa Kibiashara basi tarajia kupata laana ya Walalahoi tuliowengi ndani ya Nchi yetu, tumechoka kusikia kila uchao nyimbo hii ya UFISADI Sisi tuliowengi tunasubiri kuona hatuwa dhidi yao zikichukuliwa harakiza kwenda Mahakamani hivi sasa ili haki itendeke na ionekane kuwa inatendeka.
Mkurugenzi mtendaji wa IPP Bw Reginald Mengi amewaponda Jeshi la Polisi, Takukuru, kamati ndogo ya usalama wa taifa kwa kumuhoji na kumwagiza apeleke ushadi juu ya mapapa aliowataja katika kituo chake cha Tv cha ITV, vile vile amewaponda Sophia Simba kwa kumkejeli kuwa amechemka na Bw Mkuchika kwa kumuita kuwa ni racist, amehoji ni nani yuko juu ya sheria baada ya waziri mkuu kutoa tamko la kwamba mahakama iachiwe ifanye kazi yake.
Mzee mengi si mjinga kama wengine humu wanavyofikiri kirahisirahisi, yuko timamu anajipanga vema tu kabla haongea kitu.
wakuu,
televesioni ya itv ilikuwa ikitanganza (since monday) kuwa jana usiku wangeonyesha kipindi maalum, but kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao "ghafla bin vuu" wakasitisha kukionyesha!
kwa walio na rekodi huru na sahihi ni nini hasa kilichotakiwa kuonyeshwa na ni kwa sababu gani wakasita ghafla?
Ninyi ndio mnaoipeleka Tz bapaya kwa uwoga wenu. Biblia inasema heri mtu mmoja kufa na wala sio taifa zima kuangamia wewe bado unaendekeza mambo ya kijinga na upumbafu, kwani matatizo/ kifo si ameumbiwa mwanadamu. Mengi sio mjinga kuzungumza bila data. Nchi hii inahitaji ujasiri wa KIPALESTINA NA TAMIL TIGERS wa kuvaa mabomu na kulipuka na watu kama afanyavyo Mhe Mengi
Labda walitaka kurusha live ile ya moshi...marangu huko alipoenda kuomba msaada wa kusaidiwa na kuonewa huruma na waumini ............kupitia jukwaa la kanisa....mmm mbona RA walimponda hadi kanisa likatoa tamko???mbona yeye amekwenda kusemea huko..???
kuna mvutano mkubwa sasa hivi kati ya mengi na serikali na ndio maana serikali inafanya mpango wa kuleta sheria mpya itakayo mfanya mtu hasimiliki zaidi ya chombo kimoja cha habari.hapa serikali inajaribu kujiandaa na uchaguzi kwa kuwanyamazisha watu sana sana mengi .sasa kufungia vyombo vya habari hapa serikali wanashindwa kufikiria kwamba watanzania watapoteza kazi zao? au hilo kwao hawafikirii? je tatizo ni kuwa na vyombo habari vingi au tatizo ni habari zinazotelewa na hivyo vyombo vya habari? manake kama unafungia chombo cha habari kwa vile kinaandika habari ya ufisadi hata chombo kimoja cha habari atakacho miliki huyo mtu ataweza kuandika hio habari.serikali inafanya makosa kwa hilo swala ni je hio habari ni ya ukweli au sio ya kweli? kama chombo cha habari kimetoa habari ya uongo kwanini usiende mahakamni kushitaki habari hio?
na je hio sheria ya kila mtu amiliki chombo kimoja cha habari ni kwa watu binafsi tu au na wao serikali? manake serikali ina vyombo vingi tu vya habari.je hii ni haki au ni ubabe wa serikali kama kawaida yao?