Meneja wa Diamond, Babu Tale mbaroni

Meneja wa Diamond, Babu Tale mbaroni

Achukuliwe hatua kali kwa kuidhalilisha familia ya Nandy, ila sio Nandy, maana Nandy alijidhalilisha mwenyewe pindi alipojirekodi akiwekwa vidole sehemu mbaya
ha Haas sehemu mbaya wapi !? mkuu sie wengine hatukuiona
 
Naona Ruge anasimamia kucha kabisa bifu lao clouds media na wasafi media....

Hawatoweza...
 
Naijua video ya nandy na billnas ambavyo ilipostiwa na page nyingi tu insta. Why ilete matatizo kwa babutale? alichoandika babutale ndo sikijui
Babu Tale ndio inasemekana alimpa huyo kijana aisambaze baada ya kubakwa ataje aliyempa
 
Inasemekana babutale na sallam ndio waliompa udakutz aisambaze insta nadhan ni mwendelezo wa kukomoana kati ya clouds na wasafi
Naijua video ya nandy na billnas ambavyo ilipostiwa na page nyingi tu insta. Why ilete matatizo kwa babutale? alichoandika babutale ndo sikijui
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale maarufu Babu Tale, ametiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Babu Tale amekamatwa kufuatia amri iliyotolewa Februari 16, 2018 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda Maalum, Wilbard Mashauri iliyoelekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale.

Amri hiyo pia, ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine.

Hata hivyo, Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama hiyo ikatoa amri nyingine kama hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa wakitafutwa bila mafanikio hadi jana alipokamatwa.

Mahakama hiyo iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh250 milioni, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Baada ya kutiwa mbaroni leo alifikishwa mahakamani saa tisa alasiri kwa ajili ya hatua zaidi. Hata hivyo, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, aliyetoa amri ya kumkamata hakuwepo. Kufuatia kutokuwepo kwa msajili huyo Taletale amerudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi hadi kesho asubuhi atakapopelekwa tena mahakamani hapo kwa hatua zaidi.

Hukumu hiyo iliyomwamuru Babu Tale na nduguye kulipa kiasi hicho cha fedha, ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18,2016 katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde kutokana akiwalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
 
Baada ya Uchunguzi kukamilika kitengo cha Uhalifu wa makosa ya mtandaoni kimemkamata Meneja wa msanii Diamond maarufu kwa jina la Babu Tale kwa kuhusika kusambaza video ya udhalilishaji kwa msanii wa kizazi kipya Nandy.

Habari ya Awali: Babu Tale, Sallam SK na wahalifu wa mitandaoni wasakwa na Jeshi la Polisi
acheni uongo
BABU TALE ARUDISHWA MAHABUSU KISA MIL 250
May 23, 2018 by Global Publishers

Babu-Tale.jpg

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam, Hamis Taletale.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, jana alikamatwa kwa amri ya mahakama na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo, alirudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ili kufikishwa tena katika mahakama hiyo leo.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi hicho baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
 
Back
Top Bottom