Membe: Vita ya Ivory Coast itakuwa halali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: Vita ya Ivory Coast itakuwa halali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 13, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Membe amesema Gbagbo ataondolewa kijeshi ili kumpisha rais halali Alassane Outtara. Amewataka watanzania kutambua kuwa vita itakayotokea nchini humo ni halali na yenye lengo la kupigania demokrasia kutokana na kitendo cha mtu mmoja kutaka kuchukua madaraka kinyume na uamuzi wa umma.

  Kwa upande wake rais Gbagbo amesikika akipinga vikali mapendekezo hayo na yuko tayari kwa lolote.

  My take:

  Ni nani mwenye uwezo wa kuamua kuwa hivi vita ni halali kupigania demokrasia, ni wananchi au ni kikundi cha watu watano ambao hawatahusika moja kwa moja endapo vita vitatokea, na ni mara ngapi vita vimekuwa suluhisho la matatizo ya wananchi.

  Si haki hata kidogo kubariki vita kwa sababu yeyote ile, amani inayohubiriwa na CCM siku zote kuwa ikipotea itasababisha umwagaji wa damu isiyo na hatia, ni amani ile ile wanayoitaka watu wa Ivory Coast. Endapo vita vitatokea IC Tanzania ijiandae kunawa damu ya wana Ivory Coast itakapoanza kuililia nchi yetu.
   
 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  13th March 2011  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe


  Tanzania imetoa tamko la kumtambua rasmi Alassane Outtara kuwa Rais halali wa Ivory Coast, na imemuonya Rais anayeng'ang'ania madaraka Raulent Gbagbo kuondoka haraka Ikulu kabla ya hatua ya kuondolewa kwa nguvu haijachukuliwa.
  Tamko hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe, wakati akiongea na waandishi wa habari, ambapo alisema Gbagbo ataondolewa kijeshi ili kumpisha rais halali kuingia Ikulu.
  Hata hivyo, Membe aliwataka Watanzania kutambua vita itakayotokea nchini humo ni halali na yenye lengo la kupigania demokrasia kutokana na kitendo cha mtu mmoja kutaka kuchukua madaraka kinyume na uamuzi wa umma.
  Alisema, maamuzi hayo yamechukuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Nchi za Afrika (AU) baada ya jopo la marais wa nchi tano za Afrika kutoa ripoti yao, ambapo ilionyesha kulikuwepo na ukiukwaji wa wa utaratibu uliofanywa na Baraza la Katiba la nchi hiyo kumtangaza Gbagbo kuwa Rais, kinyume na matokeo halisi ya kura iliyoonyesha Outtara alikuwa akiongoza kwa idadi kubwa ya kura.
  Membe alisema, kundi la marais hao kutoka Mauritania, Tanzania, Afrika Kusini na Chad, liligundua Outtara alishinda kwa kura 2,448,164 juu ya Gbagbo aliyepata kura 2,107,055 kitu ambacho Baraza la Katiba liliamua kufuta matokeo ya majimbo saba ili kumfanya Gbagbo ashinde.
  "Baada ya kuona hali hiyo, Umoja wa Afrika na Baraza la Usalama liliamua kumtambua Outtara kuwa Rais na limemtaka Gbagbo kupima mwenyewe na kuiacha Ikulu au kuondolewa kwa nguvu kwa kutumia jeshi," alisema Membe.
  Alieleza jukumu la kumuandaa Outtara kurejea Ivory Coast na kuongoza nchi limeachiwa Jumuia ya uchumi wa nchi za Afrika Magharibi (Ecowas) na tayari Outtara amewasili katika jiji la Abuja nchini Nigeria kwa ajili ya kazi hiyo.
  "Uamuzi huu unaweza kuleta vita, lakini nawaomba Watanzania kutambua vita itakayotokea ni halali na yenye lengo la kupigania demokrasia, sio vizuri mtu aliyeshindwa katika kura kutaka madaraka kwa nguvu," alisema Waziri huyo.
  Utata wa nani Rais katika nchi hiyo uliibuka mara baada ya uchaguzi wa Novemba 28, mwaka jana, ambapo Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Outtara kuwa Rais na kupingwa na Baraza la Katiba lilomtangaza kwa nguvu Gbagbo kuwa Rais na hivyo kufanya nchi hiyo kuongozwa na marais wawili.
  Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete, ametoa salamu za rambirambi kwa Waziri Mkuu wa Japan Naoto Kan, kufuatia nchi hiyo kukumbwa na tetemeko la ardhi na kusababisha Tsunami.
  Rais alisema tukio hilo limeleta maafa makubwa kwa nchi hiyo na alimpa pole kwa watu waliopoteza maisha pamoja na mamia ya watu waliojeruhiwa katika maafa hayo.
  Hata hivyo, Membe alisema pamoja na Rais kutoa rambirambi hiyo, hakuna Mtanzania aliyeripotiwa kukumbwa na janga hilo na amewataka Watannzania wote wanaoishi nchini humo kuendelea kufuata utaratibu unaotolewa na viongozi wa nchi hiyo kuepukana na maafa zaidi.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Kama tofauti ilikuwa ndogo kiasi hiki, sidhani kama itakuwa Busara kumwondoa Gbagbo kwa nguvu kwa sababu wanaomwunga mkono siyo wachache pia,, zaidi kitakachotokea ni vita tena kali tu.. Naanza kupata mashaka kwamba wenye chuki binafsi na Gbagbo (westerners) waliyapika haya matokeo ili kumwondoa jamaa kwenye system!
   
Loading...