Membe umefaulu mtihani wa kwanza, songa mbele!

Membe umefaulu mtihani wa kwanza, songa mbele!

Bwana jela,
Tofauti ya Lowasa na Membe ni kwamba

1. Membe sasa hivi hana chama, yuko huru kwenda chama chochote wakati Lowasa alijiondoa mwenyewe CCM kwa hiyari na hivyo amerudi kwa hiyari yake

2. Pili Membe hajawahi kuwemo kwenye list of Shame ya Mafisadi. Lowasa alikuwemo kwenye List of shame iliyosomwa na CHADEMA pale Mwembeyanga.

Membe ni mtu safi
Man, beat it!
Membe haakuwa na nguvu kubwa ndani ya CCM, umeona press yoyote ya wana CCM wenzake wakitoa malalamiko yao kuhusu Membe kutotendewa haki?
Umeona kundi lolote likivimbisha msuli kwa CC au kwa mwenyekiti wao kwamba wana imani na Membe zaidi ya Menyekiti wao?

Mambo ya kwenye mitandao ya kijamii yasikuongepee, huyo Membe ana nguvu nje ya nchi kuliko ndani ya nchi.
Membe hafikii 50% ya uungwaji mkono kama wa Lowassa.

Membe acheze na kanisa kama wapinzani wa DRC na upande mwingine mabeberu anaweza kutoboa lakini hivi hivi ndio kaisha hivyo.
Waswahili wanasema "nguvu ya mamba kumai" wakimaanisha nguvu ya membe ni ndani ya maji tu.
Akiwa nje ya maji anakuwa nyanya.
 
Msema kweli ni kipenzi cha Mungu.

Membe na Kinana wameonewa, na hali Makamba Snr., kilichomzuia ni hatma ya mwanae kisiasa, KM na MK wa CCM, wametumia siasa za BLACK MAIL kwa mzee makamba, tubu ama mwanao atakiona.

Mie maoni yangu Laiti Mzee Kinana angekuwa ana nia ya Uraisi na akaamua kuwa mpinzani wa Magufuli, nadhani hapo ndipo pangekuwa na Ngoma ya Karne.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa siasa za nchi hii, hili ndio la msingi zaidi. Alichosema Nape ndio ukweli halisi, unless mambo yakibadilika mbeleni.

Kwenye siasa ni kosa kudhani kuwa lolote haliwezi kutokea.
Tumeona vyama dola vingi tu ndani ya afrika vikianguka, na vile vilivyoshupaza shingo vikiishia kuwaletea watu wake umasikini wa kutisha na kuanza kukosa legitimacy

Ni kosa kudhani kuwa kwa kuwa mtu ameshika mpini na ana command ya vyombo vya kijeshi basi hawezi kuwa challenged.

Wakati mwingine watu powerful huanguka na miti yote huteleza.

CCM kisiasa ni chama dhaifu sana, na hawa solution yao ni pressure ndani na nje ya nchi, hii ndo inaweza kuwafanya waachane na udhalimu wao.

Sasa ili pressure ya ndani ya nchi iweze kufanikiwa lazima wawepo watu wenye msimamo thabiti, wasio waoga, wenye dhamira isiyoyumba na wanaojua mambo.

Membe ni mtu makini sana anafaa kuwa kwenye coalition pana ya kuing'oa CCM
 
Mkuu;
Umeandika mada ndefu bila kujua kuwa majibu ya mada yako yalishatolewa na kijana wa ''Membe''!

Mwaka 2012, Nape Nnauye aliwahi kusema kwenye kipindi cha Jambo Tanzania, TBC kuwa, "Samaki ukimtoa majini hana nguvu, CCM ni taasisi na ina nguvu, ukitaka kuwa na nguvu inabidi uwe ndani ya CCM, bila CCM mwanasiasa huwezi kuwa na nguvu, tutawatoa majini hawa samaki".

Na baada ya uchaguzi mdogo wa Igunga kum-replace Rostan 2011 (nadhani) alinukuliwa akisema.

"Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni CCM"

Huyo jamaa alikuwa amejisahau sana zama zake!
 
Na baada ya uchaguzi mdogo wa Igunga kum-replace Rostan 2011 (nadhani) alinukuliwa akisema.

"Nchi hii ina wenyewe na wenyewe ni CCM"

Huyo jamaa alikuwa amejisahau sana zama zake!

Siyo CCM hii yenye kununua wapinzani na kuwahonga vyeo maana imeishiwa ajenda
 
Huu mchezo tu wa kuigiza wakikutana maeneo wanagonga cheers ni swala la muda tu , Ccm wamecheza Karata Zao vizuri kuanzia kwa Lowasa na Vibaraka wake. Ndio wameufikisha upinzani hapo.
Sio kila siku njia hio hio upinzani wameshajifunza
 
Badala ya maneno meeeengi ambayo kimsingi hayana maana, ungemshauri kuwa kwakuwa sio mwana CCM tena na 'anapendwa' sana na Watanzania, basi ajiunge na chama kingine hasa Chadema au ACT Wazalendo ili akagombee urais huko. Kuendelea kumnasibisha Membe na CCM ilhali sio mwana CCM tena ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu!
 
sina njaa hizo babu, na siyo mfuasi wa huko unakofikiria, we ndo unaishi kwa kuwaandikia watu ili mkono uingie mdomoni, mi niko solo, na ukweli ndo huo, upinge kwa hoja siyo viroja, hilo ni jibu la mtu aliyeishiwa hoja ndo anayeona kila anayeandika kilicho kinyume na wazo lake ni mfuasi wa mtu fulani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, samahani. Sikuwa namaanisha ni wewe. Hapa nilikuwa nafanya rejea ya hao unaosema wamemtelekeza membe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6. Unao uungwaji mkono
Ndugu Membe, kutokana na hali ya kinchi na kutokana na ujasiri wako wa kusimama kidete na kusema pale wengine walipoufyata, umejipatia heshima kubwa mbele ya umma. Kutokana na hilo rightfully umejikusanyia mtaji wa imani ya wananchi mkubwa sana. Na napenda nikwambie, kama utaamua kusimama kidete na kugombea, nchi hii itazizima!. Watu wamechoka kaka, watu wanaugulia maumivu braza. Njoo waziwazi utangaze nia uone nchi itakavyozizima!. Sasa hivi wananchi wanasubiri mtu mzito, jasiri wa kujitokeza na kutamka kuwa yuko tayari kusimama kwenye uchaguzi kumng'oa huyu bwana.
Hapa unamdanganya tu
 
Badala ya maneno meeeengi ambayo kimsingi hayana maana, ungemshauri kuwa kwakuwa sio mwana CCM tena na 'anapendwa' sana na Watanzania, basi ajiunge na chama kingine hasa Chadema au ACT Wazalendo ili akagombee urais huko. Kuendelea kumnasibisha Membe na CCM ilhali sio mwana CCM tena ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu!
Wanaweweseka hao,walijipa moyo kwamba Membe atawasaidia kuimega ccm
 
kitu ambacho umesahau kuandika na kumshauri ni kwamba Membe alikuwa tishio kwenye social media na siyo ndani ya ccm, ona alivyotoswa, hana hata mfuasi mmoja wa ccm wa kumuongelea tena, tofauti nabule upande mwingine, wewe ukiwa mmoja wao wa kumuona kuwa alikuwa ni tishio, wamemwacha mwenyewe na vijana wake aliowatuma kwenye social media,

hata yale mabandiko humu jf ya twende na Membe 2020 yameishia njiani amebaki na msemaji wake tu Zitto Kabwe....usisahau ni namva five 2015, yaani ndo alikuwa wa mwisho kwa wale wagombeaji watano. Mwisho nina uhakika angepitishwa kugombea kwa tiketi ya ccm wewe ni mmoja wa watu ambao wangemkana kuwa hafai, hapa mnampamba tu kwa uongo na nyie ndo mmemharibia hadi akajiona mkubwa kuliko chama chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umejitahidi.

Lakini ngoja nikupe dodoso moja tu.

Kulikuwa na lazima ipi ya kumfukuza kama sio tishio ndani ya chama?

Yaliyotokea 2015 unaweza ukawa uko sahihi; lakini hii ni 2020.

Aliyepo sasa, 2020 ambaye hakujulikana kuwa na baadhi ya sifa alizoonyesa hadi sasa watu wamejua ubovu wake, na hata yeye anayo hofu kubwa.

Ndiyo sababu yeyote anayejaribu kujitokeza mbele, hata awe hafifu kama huyu Membe tunayemwandikia hapa anaonekana kuwa ni tishio kubwa, na inalazimu ashughulikiwe haraka.

Kama ulilijua hili na bado ukaandika uliyoandika hapo juu..., utakuwa 'in denial'.
 
Kwa miaka ishirini ijayo ni vigumu kupata mtu mwenye Nguvu za kisiasa Tanzania km Lowasa
Sijui hii nayo umeitoa wapi? "...nguvu za kisiasa" alizokuwa nazo Lowassa ni zipi, za 'kiufisadi'?

Hali ilivyo sasa hivi haihitaji mtu kuwa na "nguvu za kisiasa", kama naelewa vizuri unachoandika hapa.

Ondoa hao polisi kwenye siasa na hakikisha waTanzania wanapata fursa sahihi ya kuchagua wenyewe viongozi wanaowataka wao bila ya mizengwe; halafu uje baada ya hapo tujibishane kuhusu hizo "nguvu za kisiasa".
 
Utambeba mwisho utamchoka kwa kumwandikia THREADS za kumpamba humu. Jk kambeba sana mwisho wa siku kambwaga.

Lowassa alienda monduli,mbona Camillius aendi Mtama?
 
Kwa jinsi JPM alivyoharibu uchumi, kuharibu mifumo ya haki nchini na kuharibu demokrasia.

Mtu wa Calibre ya Membe akianza kuzunguuka kwa wananchi kuwakumbusha jinsi vyuma vilivyokaza katika utawala huu basi JPM anapigwa chini fasta.

Tunajua, almanusura ya JPM na CCM ni jeshi, usalama wa Taifa na Polisi. Lakini siku miti yote ikiteleza hata hivyo vyombo havitakuwa msaada wake kwenye siasa na ndiyo maana ipo haja kutomwachia bucha jwenye ulingo wa kisiasa kwa kuhofia vyombo hivyo.

JPM inabidi awe confronted politically in all fronts, huenda akatepeta au akacompromise vitu kadhaa kama vile katiba mpya etc
 
Bwana jela,

Laiti ungalijua...
Kuongezea kidogo tu hapo;
1. Katika siasa za CCM, kinachotakiwa siyo ushawishi kwa Watanzania, bali ushawishi kwa "Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM!
Rais Magufuli amejivuruga sana kiasi kwamba Wajumbe wote wanalia njaa.

Nje ya kulitumia Jeshi la Polisi na Kijana wake DPP Biswalo Mganga wa ' Kesi za kutakatisha fedha', Magufuli hana nguvu zo zote kisiasa.

2. Ndani ya CCM katika nchi nzima, sauti pekee iliaayo nyikani ni ya Bernard Membe.
Sauti yake ni kama zumari itoayo mlio wa wimbo ulio bora.

Kwa hali hiyo, woga wa Magufuli umedhihirika kwa kumchinjia baharini Bwana Bernard Kamillius Membe.

3. CCM kimedhihirisha kuwa Chama Cha Magufuli, badala ya Chama Cha Mapinduzi.

Itawezekanaje kwa Chama Cha Mapinduzi kiwe na uoga wa kiwango cha juu kabisa cha mawazo na maono ya mwanachama wake mmoja mpaka kiamue kumuua kwa kumnyonga shingo mpaka afe kabisa?

4. Hili la mwisho ni swali: Uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM haukatiwi rufaa ndani ya CCM?

Hizo Kanuni za CCM zinazotajwa bila kunukunuliwa, (ili sisi wote tuzione na kuzisoma), zinasemaje?
Kwa nini hizo Kanuni hazibandikwi hapa tukazisoma?
 
Kuongezea kidogo tu hapo;
1. Katika siasa za CCM, kinachotakiwa siyo ushawishi kwa Watanzania, bali ushawishi kwa "Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM!
Rais Magufuli amejivuruga sana kiasi kwamba Wajumbe wote wanalia njaa.
Nje ya kulitumia Jeshi la Polisi na Kijana wake DPP Biswalo Mganga wa ' Kesi za kutakatisha fedha', Magufuli hana nguvu zo zote kisiasa.
2. Ndani ya CCM katika nchi nzima, sauti pekee iliaayo nyikani ni ya Bernard Membe.
Sauti yake ni kama zumari itoayo mlio wa wimbo ulio bora.
Kwa hali hiyo, woga wa Magufuli umedhihirika kwa kumchinjia baharini Bwana Bernard Kamillius Membe.
3. CCM kimedhihirisha kuwa Chama Cha Magufuli, badala ya Chama Cha Mapinduzi.
Itawezekanaje kwa Chama Cha Mapinduzi kiwe na uoga wa kiwango cha juu kabisa cha mawazo na maono ya mwanachama wake mmoja mpaka kiamue kumuua kwa kumnyonga shingo mpaka afe kabisa?
4. Hili la mwisho ni swali: Uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM haukatiwi rufaa ndani ya CCM?
Hizo Kanuni za CCM zinazotajwa bila kunukunuliwa, (ili sisi wote tuzione na kuzisoma), zinasemaje?
Kwa nini hizo Kanuni hazibandikwi hapa tukazisoma?
Swadakta kaka, umegonga nyundo nzito sana
 

Ndugu Membe,

Nakusalimia kwa salamu ya uzalendo.

Nichukue nafasi hii kukupa pole kwa misukosuko na mihangaiko ya kila siku ya maisha lakini pamoja na hayo nakupa pongezi tena pongezi za dhati kabisa kwa kusimama kidete kusema ukweli na kuutetea ukweli ukiwa ndani ya chama cha mapinduzi kwa ujasiri mkubwa kabisa. Katika nyakati hizi ambazo watu ndani ya chama cha mapinduzi wamejikunyata kama vifaranga vya kuku kwa uoga kwa bwana mkubwa na wapambe wake, wewe umesimama kidete kutaka utawala bora, kutaka demokrasia nchini, kutaka pasiwepo matendo ya kunyanyasa wananchi kisiasa.

Kutokana na hayo ningependa kuzungumza na wewe yafuatayo:

1: Mahasimu wako wanakuogopa, ndiyo maana wamekuchezea faulo kukutoa mchezoni
Ndugu Membe, walioko nyuma ya faulo uliyochezewa ndani ya CCM wanajua kuwa, kama mkisimama kwa vigezo vya ubora iliwemo uadilifu kwa taifa letu, kwa uzoefu wa uongozi, kwa exposure, kwa mipango mkakati ya kupambana na umasikini, kwa imani ya demokrasia pana katika nchi, kwa kuchukia rushwa, kwa utaalamu wa kuanalyse mambo mtambuka ya kinchi kisiasa, kiuchumi na kijamii na uwezo mkubwa wa diplomasia, hawa watu wanaujua uwezo wako, wanajua kuwa wewe ni tishio katika nafasi zao kwa sababu wanajua kuwa ukichukua fomu basi bwana mkubwa hana chance.

Wewe unajua vizuri tu kuwa bwana mkubwa kukalia kile kiti ni kwa sababu ya ugomvi wako wa kisiasa na mheshimiwa Lowasa, kwa hiyo aliokota dodo chini ya mnazi. Nje ya hapo mwaka 2015 mgombea kwa tiketi ya chama cha mapinduzi alikuwa ama uwe wewe au Lowasa, hilo analijua wazi na ndo maana kambi yake imejawa hofu baada ya wewe kuonyesha msimamo, wakaamua uchezewe figisu mapema kabla hujaingia uwanjani

2: Usikubali kusikiliza kelele za kukutaka ubwage manyanga
Ndugu Membe, baada ya tukio lilitokea la kufanyiwa figisu, wamejitokeza wale wanaojiita 'watoa ushauri', wanasema eti ukae kimya, usiongee, uachane na ndoto za kugombea urais. Mimi ningependa kukwambia kuwa usiwasikilize hao, hao ni watu waoga, fear mongers, hao ni quitters, hao ni appeasers wa madhalimu, hawana utofauti na Neville Chamberlain mwanasiasa wa uingereza kipindi cha vita kuu ya dunia ya pili aliyetaka Uingereza ifanye compromise fulanifulani na kiongozi wa Third Reich ya Ujerumani na kwamba Uingereza isimpinge na wala isimconfront. Laiti Winston Churchill angeusikiliza ushauri huo, huenda kule Birmingham wangekuwa wakiongea kijerumani sasa.

Ninachotaka kusema ni kwamba usisikilize kauli za hawa wanaotaka uiache azma yako adhimu ya kugombea uraisi ili uweze kuwakomboa watanzania waondokane na utawala wa kiimla, sera mbovu za kiuchumi, diplomasia inayofeli, siasa chafu za kununua watu, watu kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi kwa sababu za kisiasa, Matumizi mabaya ya madaraka na umasikini wa kutisha.

3. Taifa linakuhitaji sana
Ndugu Membe, kama ulitaka kugombea uraisi kwa ajili yako binafsi basi achana na ndoto hiyo, ila kama kwa dhati ya moyo wako kwa ndani kabisa unadhani kwa dhati kabisa kuwa unataka kugombea uraisi kwa ajili ya wananchi wa Tanzania, kwa ajili ya kutengeneza serikali inayoheshimu Katiba, kwa ajili ya kutengeneza serikali inayoheshimu haki za watu wake kwamba wananchi wana haki za kuchagua viongozi wao bila kulazimishiwa kama tulivyoshuhudia katika uchaguzi feki wa serikali za mitaa uliopita.

Kama unaamini katika umoja na mshikamano wa kitaifa kuwa nchi hii ni yetu sote na kwamba kuwa na mawazo mbadala wa mawazo ya kisiasa siyo dhambi, kama unaguswa na umasikini wa watu wetu na unaamini kabisa katika kuheshimu bunge na mahakama bila kuziingilia basi Taifa linakuhitaji sana. Na kutokana na kwamba wewe tangu ukiwa kijana ulikula viapo vizitovizito vya kuitumikia nchi yetu kwa vipahi na akili zako zote, basi nakuomba sana mheshimiwa Membe uendeleze azma yako ya kugombea Uraisi ili uweze kutumia vipawa vyako vikubwa kuinusuru nchi kutoka katika hii free fall tunayoishuhudia inayoipeleka nchi katika shimo refu lenye kiza kinene

4: Uraisi hutoka kwa Mungu, usiache kuutafuta
Ndugu Membe, Mungu akitaka kukupa uraisi anaweza kukupa ukiwa ndani ya CCM au nje ya CCM.
Kwa hiyo usiache nia yako na azma yako njema kabisa ya kugombea uraisi eti kwa sababu mahasimu wako wamekuchezea faulo, kikubwa ni kuwa unapaswa kuutaka uraisi, unapaswa kuutafuta uraisi na unapaswa kuhakikisha hubwagi manyanga chini. Kama unavyojua, vitu vyenye thamani vinahitaji juhudi na kutokata tamaa, basi nakushauri uendelee kuutafuta uraisi hata nje ya CCM kwa ajili ya kulinusuru Taifa letu. Taifa letu liko njia panda, unaliachaje achaje?. Kama ipo ipo tu.

5. Wamekutosa kwenye Tanga, Piga mbizi kapande Jingine
Mahasimu wako wamekutosa baharini kwa sababu unautaka unahodha, wasichojua masikini ni kwamba wewe ndiye unayeijua njia bora, nahodha wanayempigania anawapeleka kwenye mkondo bahari ambapo wasipokuwa makini chombo chao kitapigwa dafrao na kuzama. Laiti wangalijua.

Ndugu Membe, wewe una uzoefu wa zaidi ya miaka 45 kwenye bahari ya uongozi, umeona mengi, unajua mengi, wamekutosa lakini kupiga mbizi unajua. Sasa ni wakati wa kupiga mbizi kuliwahi Tanga jingine la watu wanaojitambua ili kwalo uweze kushirikiana ili safari iendelee salama salmini.

6. Unao uungwaji mkono
Ndugu Membe, kutokana na hali ya kinchi na kutokana na ujasiri wako wa kusimama kidete na kusema pale wengine walipoufyata, umejipatia heshima kubwa mbele ya umma. Kutokana na hilo rightfully umejikusanyia mtaji wa imani ya wananchi mkubwa sana. Na napenda nikwambie, kama utaamua kusimama kidete na kugombea, nchi hii itazizima!. Watu wamechoka kaka, watu wanaugulia maumivu braza. Njoo waziwazi utangaze nia uone nchi itakavyozizima!. Sasa hivi wananchi wanasubiri mtu mzito, jasiri wa kujitokeza na kutamka kuwa yuko tayari kusimama kwenye uchaguzi kumng'oa huyu bwana.

7. Aluta continua victory Asceta
Mwisho nimalizie, kwa kauli ya mwanaharakati aliyepotea, ndugu Ben Saanane, aliyekuwa akipenda kuitumia, akimaanisha victory is certain, na mimi napenda kukwambia, Ushindi upo basi utafute

2020 Twende na Membe

Ni mimi Missile of the Nation (Kombora hatari kabisa la Ulinzi wa Taifa)
Mlisema hivyo hivyo kwa mzee Mrema, Lowassa, Maalim Seif. Lakini mwisho wa siku wakabaki peke yao.
Tuache kuchuuza wenzetu.............
 
Back
Top Bottom