Membe: Tutachagua mabalozi vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe: Tutachagua mabalozi vijana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 6, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  na Lucy Ngowi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema kuwa, muda mfupi kuanzia sasa, kutakuwa na mabalozi vijana ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani, baada ya waliokuwapo kustaafu.


  Membe alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa anagawa vyeti kwa maofisa wa wizara yake wanaofanya kazi hapa nchini na kwenye balozi mbalimbali nje ya nchi, baada ya kuhitimu mafunzo ya wiki tatu waliyoyapata katika Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam.

  Alisema kuanzia mwaka ujao kuna mabalozi mbalimbali wanaotarajiwa kustaafu, hivyo nafasi zao zitachukuliwa na maofisa vijana wanaofanya kazi ubalozini kwa kuwa wanazo sifa zinazotakiwa.


  Aliongeza kuwa mafunzo hayo ya wiki tatu waliyoyapata watumishi hao wa wizara yake, ni ya promosheni ya kuwatoa hapo walipo na kuwapandisha daraja jingine.


  Pia alisema mafunzo hayo yaliyotolewa ni muhimu kwa kuwa yanawawezesha wanadiplomasia hao kuielewa nchi yao na mambo yanayoendelea ulimwenguni hivi sasa.


  Naye Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Dk. Mohamed Maundi, alisema kuwa madhumuni ya kozi hiyo iliyotolewa kwa maofisa hao ni kuwapatia njia mpya ya kuelewa shughuli zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ndani na nje ya nchi.

  Alisema kwa kuwa wengi wao wapo nje ya nchi, mafunzo hayo yatawasaidia kuwapatia mbinu mpya ya kuboresha masuala ya kidiplomasia.

  Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi aliyeko nchini Uingereza, Amosi Msanjila, aliipongeza wizara yake na chuo hicho kwa kuwapatia mafunzo hayo, kwa kuwa hivi sasa wanastahili kupandishwa daraja kutoka hapo walipokuwa.

  “Kwa miaka 16 iliyopita mafunzo haya yalikuwa hayatolewi, hivyo kwa upande mwingine watu waliweza kupanda vyeo bila kupitia kozi hizi,” alisema Msanjila.

  Alisema wahitimu wote walipata fursa ya kuzungumza na watu kwenye taasisi mbalimbali ili kujua changamoto zilizoko kwenye maeneo muhimu ambazo Watanzania ama raia wa nchi nyingine wanazipata wanapotaka kuja Tanzania ama kwenda katika nchi nyingine.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kuna thread nimeona inasema kuwa wanaofanya kazi kwenye balozi zetu ni watoto wa vigogo. Ina maana Membe anatueleza kuwa tutachagua mabalozi ambao ni vijana wa vigogo kwa vile wao ndio wenye sifa zinazotakiwa?
   
 3. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Its time tubadili sheria mabalozi wawe wanapitishwa na Bunge sio kama zawadi kwa marafiki wa vigogo.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nadhani anachosema Membe ni kuwa watoto wao (watoto wa vigogo) wamekuwa na sasa wanataka kuwafanya mabalozi. Foreign Affairs imejaa majina yale yale! Na ndio maana sasa hivi sifa ya Tanzania kimataifa inashuka maana hatuna wana-diplomasia tena, ila tuna genge la 'surnames' linawakilisha maslahi ya familia zao. I hope one day magezti ya Tanzania yataandika orodha ya maofisa walioko kwenye balozi zetu nje na hata hawa hapa Dar es Salaam. Jina moja baada ya jingine.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Na Bunge liwekewe vigezo kwua watakaotakiwa kupitishwa ni wale tu ambao watawezaa kutekeleza sera yetu ya nje kwa ufanisi, umri isiwe kigezo kikubwa sana
   
 6. v

  valid statement JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  wataendelea kuchagua watoto wao hao. Hawana jipya, mtu wa kawaida mpaka uonekane na uchaguliwe balozi wa nje ni lazima uwe ushajikomba saaana.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Nov 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Binafsi nina wasiwasi na vetting inayofanyika kupeleka badhi ya watu nje, ila tuna baadhi ya vjana wazuri sana kwenye balozi zetu, wengine... Mungu dnio anajua
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe utakua lini. Habari zako zimekuwa ni za kuunga unga tu! Mnakaa mnajazana maneno halafu mnayakimbizia humu jamvini. Ni watoto gani hao unaowasema?
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kama unaamini katika unachokiandika kwa nini wewe usitaje hayo majina ya vigogo badala ya kusubiri yaandikwe na gazeti, sijui lini! Majungu hayatakupa mtaji wewe!
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Sitashangaa mabalozi hao vijana wakiwa watoto wa vigogo. utasikia majina ya sijui Kikwete, Msekwa, Kawawa, Mkapa, nk.

  itakuwa tabu tupu. Dawa nikuingia msituni!
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Don't take it personally kama zinakuuma. Hata kuuliza tuu swali inakuuma?
   
 12. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #12
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Muhimu ni watu watao deliver siyo umri. Naona jamaa anaanza gawa vyeo kwa uvccm. Maana juzi tumemsikia Beno Malisa akidai kwamba kuna wanasiasa ndani ya CCM wanaotaka kugombea urais 2015 wanapita wakiwaahidi vijana ukuu wa wilaya pindi wakiingia IKulu. My take. Wakati tuna mjadala wa kama hivi vyeo vya ukuu wa mikoa na wilaya vina umuhimu wowote ktk mazingira ya sasa,kuna wanasiasa wa magamba wanaendelea wapromise vijana kupewa u-DC.
   
 13. z

  zamlock JF-Expert Member

  #13
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ah ah ah waende zao uko hizi balozi zetu wamejazana watoto wa vigogo na kuna baadhi ya balozi ambazo nimeshakaa kwenye hizo inchi watoto wa vigogo wamejazana ni bora ipitishwe sheria bunge letu ndilo liwe linawapitisha mabalozi
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  kwenye hii thread yako ipi ni point yako ya maana.
  Unaweza kusoma thread kama si kiwango chako unaweza kusepa, siyo kujaza upumbavu humu na wewe!
   
 15. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Katika hafla mbalimbali nilizoona nje ya nchi zilizokutanisha mabalozi wa nchi nyingi sija bahatika kuona balozi yoyote kijana!
   
 16. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #16
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  usiwe mkali kiongozi, yanayosemwa yanawezekana yakawa na ukweli ndani yake: kwa vile na wewe umemaliza kwa kuuliza swali kwamba ''ni watoto gani hao.....?'' ina maana kwamba UJUI hivyo basi hunabudi kuchunguza kuchunguza kabla ujawapalamia wenzio kwa ukali, humu jamvini hatujazani maneno tu bwana.
   
 17. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #17
  Nov 6, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Mbopo mimi nawafahamu watoto/ndugu wa vigogo waliopo foreign affairs; however siwezi kudhibitisha walipatiwa hiyo nafasi kwa upendeleo kwasababu sifahamu candidates wengine walio-apply hizo nafasi wakashindwa. Pamoja na hayo ni ukweli kwamba sijawahi sikia nafasi za kufanya kazi "foreign affairs" zikitangazwa so hilo nalo linaongeza mashaka kwa watu wanaochaguliwa. Baadhi yao ni: Mindi Kasiga huyu ni mtoto wa mdogo wa Anna Mkapa (yeye ni Afisa Uhusiano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Caroline Chipeta (UK foreign office) huyu ni ndugu na Jaji Chipeta (not sure kama bado ni jaji), Joseph Sokoine (Canada Foreign affairs)- huyu anafahamika, Kuna mwingine alikuwa ofisi ya DC nafikiri ni ndugu na Fatma Saidi Ali (anaweza kuwa amehamishiwa ofisi nyingine), Mke wa William Malecela nafikiri huyu bado yuko NY-office. January Makamba alishawahi kufanya foreign affairs huko nyuma kabla ya kuwa mbunge. Na wengine muwamalizie; Angalizo: Sisemi kama hawa wamechaguliwa kwa upendeleo kwasababu sifahamu kama kuna candidates walio-apply wakakosa; however sijawahi kuona nafasi za kazi foreign affairs zikitangazwa pia hili nalo nilakuliangalia. Nafahamu pia wengi wanaochaguliwa kuwa mabalozi ni kama "asante fulani" hivi mfano balozi Peter wa UK huyu alikuwa mfanyakazi wa kawaida kabisa Ikulu lakini alikuwa kijana "mwaminifu" a lot of "ndio mzee's etc" Balozi Maajar naye ni shukrani yakufanya kampeni kwa ushindi mkubwa- huyu ali-invest her own money kwenye kampeni kama vile Lowassa etc. Kuna wanajeshi wastaafu waliopewa ubalozi pia kama shukrani so I guess labda tuambiwe appart from "ujana" balozi au mfanyakazi wa foreign affairs anatakiwa kuwa na sifa gani hasa?
   
 18. k

  king kong Senior Member

  #18
  Nov 6, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi za tanzania sitaki mimi wapeane tu coz zote mpaka uwe na refa.
  Watoto wa vigogo wamekaba kama inchi yao peke yao. HARAMU
   
Loading...