Membe na Lowassa waungana kuelekea urais 2015... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Membe na Lowassa waungana kuelekea urais 2015...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Juma Hamis, Aug 12, 2012.

 1. J

  Juma Hamis Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika hali ambayo si yakutengemea kwa wana C.C.M,hususani viongozi wa ngazi za juu za chama hicho tawala nchini wamejikuta wakiwa wamengawanyika sana katika masuala yanayohusu uchaguzi wa umoja wa vijana UVCCM,hii inatokana na waziri wa mambo ya nje na mwana C.C.M kutoka jimbo la tama mh.Membe,kuamua kuungana na mh.Lowasa ili kuandaa safu ya uongozi wa vijana UVCCM.

  Ni ukweli usiopingika kuwa wawili hawa hapo awali walikuwa ni mhasimu wakuu wa kisiasa hususani katika kutafuta uungaji mkono ndani ya chama na kwa wananchi ili kuupata Urais baada ya JK 2015,kwa hali ya sasa wawili hawa wameungana na kuunda kambi moja itakayokuwa na ushawishi mpana ndani ya C.C.M kwa kuhakikisha kuwa wanaunda vikosi viwili hahususi vitakavyo simamia mchakato uchaguzi kuanzia ngazi ya wilaya,mikoa na taifa.Vikosi hivi ni;

  i.Kikosi kinachoongozwa na H.Bashe na Fredy Lowasa-ambacho mwasisi wake akiwa mh.Lowasa

  ii.Kikosi kinachoongozwa na Gottani-ambacho mwasisi wake ni mh.Membe.

  Taarifa kutoka ndani ya vikosi hivi zinaonyesha kuwa kwa sasa vinafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa safu ya uongozi wa UVCCM inakuwa ni ili wanayoweza kuipa maelekezo kuelekea 2015.Kwa sasa wamekamilisha mkakati wa kuhakikisha kuwa uongozi wa kitaifa wa UVCCM hususani ni mwenyekiti na makamu wenyekiti kuwa wafuatao wanashinda kwa njia zozote zile;
  1.JAMARI-M/kiti.
  2.ANTONY MAVUNDE-Makamu m/kiti

  Na kwamba H.Bashe amezungukia umoja huo kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa anawaweka sawa makatibu wa UVCCM,ikumbukwe kuwa makati wa UVCCM walipokuwa Dodoma mwaka huu walikutana na BASHE Dodoma hoteli na kuwanunulia chakula,rushwa ya 50000 na kugharimia gharama zote za vyumba walivyofikia.GOTTANI naye amekuwa mstari wa mbele katika kutoa pesha kwa wagombea katika ngazi zote.Lakini pia wanaendesha kampeni kwa sasa kinyume na taratibu za uchaguzi wa UVCCM.

  Lakini,pia kugawanyika kwa viongozi wakubwa wa C.C.M wamendelea kuwa na maswali yaliyokosa majibu kama vile;

  1.Je?Membe alikuwa anatumiwa na Lowasa ili kufuatilia nyendo za SITTA,MWAKYEMBE na kundi lao la wapambanaji kwa ajiri ya urais 2015.

  2.Je?Membe amekubali kuanza kupiga jelamba la uwaziri mkuu 2015,akiwa chini ya LOWASA kama rais wake.

  3.Je?Membe na Lowasa wanategana ili kufanikisha malengo ya mmoja wao au mmoja anatumiwa vibaya na mwezake.

  Katika hali kama hii UVCCM inajikuta tena kwenye vimbi lingine ambalo laweza kuhakikisha kuwa unasambalatika au unateka wa wenye fedha.UVCCM na wadau wake wote lazima wasikubali kutumiwa na kupewa rushwa na kuiacha tasisi ikivujika mchana kweupe kumbukeni kuwa uchaguzi huu ulenge kuwapata viongozi na si wala rushwa maana watashindandwa kufanya siasa zidi ya vyama vya upinzani kama vile CHADEMA.

  Source,katibu wa UVCCM-MKOA
   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​nape nae kachangia kuvujisha habari sababu tayari woga umemjaa akisikia lowasa anaelekea ikulu
   
 3. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Good for them...

  Don't misinterpret my personality and my attitude, the former is who I am, and the later depends on who you are
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Lowassa lazima awagaraze garaze hao wote kwanza anatokea kaskazini
   
 5. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  umechemka bwana mdogo.
  majina umekosea na hujui nini wasema
  Anthony Mavunde ni mgombea na wala hausiki na Membe wala Lowasa
  Yanini kujihusisha na Lowasa wakati hata 2015 kufika kwake ni bahati nasibu?
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Lowassa na Membe bado mahasimu. Wote bado wanautaka urais 2015.
   
 7. M

  Matunyengule JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 701
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  ss ulichopinga ni nn? Mbona umerudia yale yale aliyosema mleta uzi.
   
 8. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwani ukiwa waziri wa nje wa ccm ni lazima ugombee urais?
   
 9. Facilitator

  Facilitator JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,288
  Likes Received: 802
  Trophy Points: 280
  Swali zuri. Kwa sababu wana dimples..
   
 10. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,377
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Waruke ruke tu ila 2015 nchi ni yakwetu CHADEMA!
   
 11. z

  zamlock JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  wanaangaika sana nchi inakwenda mikononi kwa dk slaa hv hata awasomi alama za nyakati? Badala wajiandae waje chadema wale wasafi mtu kama bashe badala ajiandae akachukue jimbo lake nzega kwa tiketi ya chadema ana angaika na ni mwanasiasa mzuri sana nilibahatika kukaa naye akawa anazungumzia maswala ya siasa nilimpenda sana jamaa uwezo wake wa kujenga hoja pliz bashe fanya kampen za mzee ila kumbuka wana nzega wanakuhitaji sana kwa tiketi ya chadema
   
 12. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,288
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Duh kumbe Membe ana nguvu kiasi cha kuifanya JF na wapinzani wake kuweweseka siku hadi siku?

  Kwa jinsi jina lake linavyovuma kwa mabaya ya kulazimisha naanza kuomba huyu bwana aoteshwe ili tupate upinzani wa kweli 2015. Sidhani debe tupu linaweza kuvumishwa kama Membe anavyovumishwa JF na magazetini.
   
 13. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Sie tunafurahi, pale mwisho wa Siku watakaposalitiana.
   
 14. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,805
  Likes Received: 2,577
  Trophy Points: 280
  This time around bila kusimamisha mteule Mzanzibari CCM itaua thana nzima ya usawa ndani ya muungano ie muungano as a partnership of equals. What is that fancy phrase? Yes! sisi yetu macho.
   
 15. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,226
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Acha washikane uchawi! mwisho wa siku chadema ikulu.
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,563
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Mkuu Simplemind, the last chance ya Mzanzibari kuwa rais wa JMT, ilikuwa 2010 kupitia Dr. Salim, CCM lost the chances and will never come again!.

  CCM imekuwa ikichaguliwa kwa kupendwa/kuaminiwa na kwa mazoea, sasa CCM haipendwi tena kivile, haiaminiki na wale wa mazoea wameanza kuamka, hivyo CCM has lost the mandate to rule from peoples hearts, as a result, wenyewe, wenye nchi yao, wameamka, sio watu tena wa kupelekwa pelekwa kwa kuwaletea Mzanzibari kuwatawala!.

  Japo CCM ingependa sana kusimamisha Mzanzibari ili kuwapooza Wanzanzibari na hasira za muungano, Mzanzibari pekee aliyepo as of now ni Dr. Shein, but very unfortunately, kwa wabara hauziki, hivyo CCM hawawezi kufanya kosa hilo!.

  Nionavyo mimi, hakuna tena nafasi kwa Mnzanzibari mwingine yoyote, kushika urais wa nchi yetu, no.. never..!.

  Niiteni mbaguzi, but this is a fact!, kama wapiga kura wengi ni wabara, tumechoka na tutasema no!.

  Cha muhimu ni Wazanzibari, waitumie fursa hii adhumu ya mabadiliko ya katiba, katiba itamke wazi kuwa urais nao upishanwe rasmi kati ya bara na visiwani, vinginevyo kwenye urais, Wanzanzibari wataishia kuusikia kwenye bomba tuu!.


  Pasco.
   
 17. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,795
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280


  is that a threat or what??
   
 18. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Urais wa JMT lazima uwe wa kubadilishana miaka 10 kila upande,katiba iseme wazi(kama muungano utakuwa bado upo)...pia katiba iseme wazi waziri mkuu na waziri kiongozi mipaka yao wapi?tuichukue katiba ya zbar na kuiangalia pia maana rais wa zanzibar ndie amiri jeshi mkuu wa zbar (majeshi yake yajulikane) na pia akiwa ndani Muungano ataweza tangaza vita?Makamu wa rais je?na kazi zake pia!!
  Natamani sana 2015 ifike nikiwa hai nione mchakato mtamu sana kwenye siasa za Tanzania na demokrasia yake,ndio kukomaa huko CCM wasiogope changamoto wala kupoteza viti vingi vya ubunge!

  Muungano wa BM na EL sidhani kama utadumu maana watageukana sasa hivi baada ya mmoja wapo kuitwa na mkuu na kupewa fitna kwa siri,watagombana hapo hapo maana BM anaona ana fit kabisa kuwa President ajaye,ila hajajua kabisa EL kiapo chake na JK.Labda kama JK atawaita wote haao na kuwapa somo kali na kuwaomba wakubali kuwa kitu kimoja kwa maslahi ya taifa na chama..(Unafiki umo lakini)
   
 19. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,795
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  Hivi watu mnaomfikiria Lowassa kuwa rais wa JMT huwa mpo serious kabisa kwa dhati zote au huwa ni some sort of jokes? Yaani kwa kashfa iliyomn'goa uwaziri mkuu bado mnampa credit ya urais? wengine mnasema alionewa au kusingiziwa lakini mbona miaka yote hiyo hajasimama kueleza kwa dhati nini hasa ukweli kuhusu richmond! Membe naye ni joke nyingine! Ameshalifanyia nini taifa la Tanzania hadi kuwaza kumpa urais? au ni cheap popularity? hana tofauti na Vasco alikuwa waziri wa mambo ya nje Watanzania kwa kuangalia umaarufu aliopewa na vyombo vya habari tukampa urais bila kurudi nyuma na kuchimba utendaji wake tangu alipoingia kwenye utumishi wa umma hadi kwenye ulingo wa siasa! Siamini kama tunataka kurudia makosa yale yale! Wapo Watanzania serious wenye maono na uchungu na taifa letu hebu tuumize vichwa kumpata rais wa 2015 tusiongozwe na vyombo vya habari tena kufanya maamuzi!
   
 20. J

  JF-MBUNGE JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sikio la kufa halisikii dawa......wote wanao pewa promo ccm ni wanamtandao wa serikali hii kwahiyo hakuna mabadiliko yeyote
   
Loading...