Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.

"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.

Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
Labda agombee kwa chama chake,huku CCM mgombea ni mmoja tu nae ni JPM na huu ndio utaratibu tuliojiwekea wana CCM.
 
Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.
Hii michezo ya kitoto sana. Robert Green kwenye "48 Laws of Power" Law #3 anasema "Conceal your Intentions: keep people off-balance and in the dark by never revealing the purpose behind your actions".

Siamini kabisa kama kachero mzoefu kama Membe haifahamu hii basic law. Otherwise keshapitwa na game na aende akalime tu.
 
Jinsi ninavyoona hali ilivyo sasa ndani ya ccm kama Magufuli atasimamishwa na wanachama/ mwanachama yeyote kugombea uteuzi wa kugombea Urais, haitakuwa rahisi kwa yeye kushinda!! Sababu kubwa ikiwa yeye kukidharau chama na kufikiri kuwa alipata Urais kwa nguvu zake binafsi na sio kwa nguvu za chama; wenye chama sasa wanapanga mikakati ya kumuadabisha. Magufuli hajui kuwa yeye mgeni katika ccm na chama hicho kina “ wenyewe “!
 
Hii michezo ya kitoto sana. Robert Green kwenye "48 Laws of Power" Law #3 anasema "Conceal your Intentions: keep people off-balance and in the dark by never revealing the purpose behind your actions".

Siamini kabisa kama kachero mzoefu kama Membe haifahamu hii basic law. Otherwise keshapitwa na game na aende akalime tu.

Hii law inafanya kazi kwenye fair grounds, siyo kwenye grounds ambazo mmoja anapiga nyundo yeyote yule ambaye akilini mwake anadhani ni "potential" challenger!.
Kama unafuatilia vizuri Membe alikaa kimya kwa muda mrefu, mpaka Katibu Mkuu akaanza kumchimba ili na yeye asifu juhudi za Mwenyekiti, au aseme chochote cha kuonyesha hautaki Uraisi

Baada ya maji kukorogeka ilibidi aibuke Daudi wa kusema mimi nakwenda kumng'oa Goliath, na kitendo cha kuonyesha ujasiri katika wakati huu ambao wengi wameufyata kunamuongezea Credit!

Kumbuka Laws of Power inasema Conceal your moves mpaka pale utakapohisi Master yuko Vulnerable, Kwa sasa Jiwe yuko Vulnerable mno ndani ya CCM ndiyo muda muafaka wa kustrike.

Membe amefanya Good timing ila ninachomshauri ASIKUBALI KUSHAURIWA KUACHA, INABIDI AENDE TU AKACHUKUE FOMU , ATUMIE KANUNI YA COLIN POWEL KUWA KAMA HUJAAMUA KUINGIA KWENYE VITA USIBEEP, ILA UKIAMUA KUSHAMBULIA BASI SHAMBULIA KWA NGUVU KUBWA ULIYONAYO!

Njia ya kumng'oa Jiwe ni Blitzkrieg ya kisiasa, yaani Pressure kutoka ndani ya Chama chake, Pressure ya Umma, Pressure kutoka kila kona. Lazima akae!
 
Membe hawezi kuongea hivyo ,ni kiki za wanaomshabikia ..Membe mwaka 2015 alisubiri kuoteshwa je ameoteshwa 2020

Hesabu za kawaida ,membe alishindwa kushindwa 2015 JK ,Nape,Mama Salma wakiwa watu wanaompigania ,sasa hivi anamjua nani,labda kupitia upinzani
 
Hii law inafanya kazi kwenye fair grounds, siyo kwenye grounds ambazo mmoja anapiga nyundo yeyote yule ambaye akilini mwake anadhani ni "potential" challenger!.
Kama unafuatilia vizuri Membe alikaa kimya kwa muda mrefu, mpaka Katibu Mkuu akaanza kumchimba ili na yeye asifu juhudi za Mwenyekiti, au aseme chochote cha kuonyesha hautaki Uraisi

Baada ya maji kukorogeka ilibidi aibuke Daudi wa kusema mimi nakwenda kumng'oa Goliath, na kitendo cha kuonyesha ujasiri katika wakati huu ambao wengi wameufyata kunamuongezea Credit!

Kumbuka Laws of Power inasema Conceal your moves mpaka pale utakapohisi Master yuko Vulnerable, Kwa sasa Jiwe yuko Vulnerable mno ndani ya CCM ndiyo muda muafaka wa kustrike.

Membe amefanya Good timing ila ninachomshauri ASIKUBALI KUSHAURIWA KUACHA, INABIDI AENDE TU AKACHUKUE FOMU , ATUMIE KANUNI YA COLIN POWEL KUWA KAMA HUJAAMUA KUINGIA KWENYE VITA USIBEEP, ILA UKIAMUA KUSHAMBULIA BASI SHAMBULIA KWA NGUVU KUBWA ULIYONAYO!

Njia ya kumng'oa Jiwe ni Blitzkrieg ya kisiasa, yaani Pressure kutoka ndani ya Chama chake, Pressure ya Umma, Pressure kutoka kila kona. Lazima akae!

‍♀️‍♀️🤣🤣🤣 ‘LAZIMA AKAE’. Hapa mwisho pamenipa nguvu sana ya kuanza siku yangu. Mh Benard Membe ndie Rais wetu kwa 2020 - 2025.
 
Mh B C Membe, tunakuomba sana uchukue fomu ya kugombea nafasi ya Urais.
Uwe ndani ya CCM au hata nje ya CCM, uchaguzi wa awamu ijayo watanzania tuna chagua mtu wala sio chama, ni ukweli usio pingika kuwa yapo mazuri yaliyo fanywa na CCM , Ila jambo lilokero kero kubwa na ambalo limepigiwa kelele bila ya mafanikio ni mtindo wa uongozi wa kuteka watu, kupotea kwa watanzania wenzetu ambao wengi mwisho wao umekuwa ni vifo.
Kwa utafiti wa haraka haraka inaonyesha kuwa huo umekuwa ndio mfumo unao tumika na viongozi wa awamu ya tano. Hili jambo sio utamaduni wetu watanzania , na kwa sababu hiyo tumeamua kufanya mabadiliko kupitia sanduku la kura.
Hivyo tuna kusihi mh Membe ingia kwenye kinyang'anyiro utapata kura nyingi ambazo haijawahi kutokea , una kura nyingi sana kutoka ndani ya CCM lakini pia utapata kura nyingi sana kutoka kwa wapinzani.
Na ndiyo maana nasema watanzania safari hii tutachagua mtu wala sio chama, lengo kwanza ni kumpata wa kututoa kwenye haya makucha ya ukandamizaji.
 
Hii michezo ya kitoto sana. Robert Green kwenye "48 Laws of Power" Law #3 anasema "Conceal your Intentions: keep people off-balance and in the dark by never revealing the purpose behind your actions".

Siamini kabisa kama kachero mzoefu kama Membe haifahamu hii basic law. Otherwise keshapitwa na game na aende akalime tu.
Pole sana.
Kwako wewe Theories za Bwana Green unaziona Supreme & Ultimatum?
Hujaelimika vya kutosha
 
Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.

"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.

Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
Membe anazijua vizuri kanuni za CCM hawezi kutamka haya maneno wakati huu. Mnamtengenezea mazingira ya kumuengua atakapochukua form au afukuzwe uanachama kwa 'Uasi'
 
Wakati vikao vinajadili kumfukuza ccm ninyi mnaongea ujinga... ama ndiyo ninyi mnaochochea afukuzwe mapema vile mnajua anaweza kuja kuwadhuru ghafla.

#rais anayejenga kuliko wote
 
Maendeleo ya vitu si bora kuliko maendeleo ya watu,
Hata mkolomi alileta maendeleo ya vitu lakini bado tulidai uhuru,
 
Mheshimiwa Membe amekanusha hajasema atagombea 2020. Ila hajasema pia hatagombea huyu Mzee yupo safi anawaacha mbwabwaje yenu tu.
 
Back
Top Bottom