Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.

Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.

"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.

Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."

Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
 
Siamini kama kasema hivyo

Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
 
"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho


Ilikuwa kwa simu!!
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
 
Back
Top Bottom