Membe asaini mkataba bila kuusoma nchini China, mwakilishi aja juu, rais Kikwete amtetea!

Na hiyo clip ninayo bro inaskitisha sanaaaaaaa kum depress mwenzako huyu membe hafai kuwa rais wa nchi hii na kama ccm watampitisahaa natangaza wazi wazi kura yangu inaenda kwa slaa
 
cc tunaotumia opera mbona hatuwezi kuiangalia? Tunaomba tuwezeshe kwa njia nyingine, au ukiingia youtube inaitwa video gani?

[h=1]kwenye youtube search kwa title hii: Kamati ya Maridhiano Six: MAONI YA WAWAKILISHI KWA TUME YA KATIBA; 14/10/12; Part 8[/h]
 
alifanya nini haswa hadi ukamtoa mtimani?

mmh....naona hata boss wake mwenyewe hamuamini.....asingekuwa anazurura namna hiyo wakati yeye yupo....inaelekea hata yeye hamuamini......
 
Mh, kwa hali hii ya viongozi maslahi hatufiki kokote, halafu eti anataka tumpe nchi,
si atatuuza kwa mikataba kama ile ya kina chifu Magungo!...
Tukimchagua Membe tutakuwa tumemchagua Jaa la Kaya jingine!! hawa ni ndugu wa Damu!! Kwa ufahamisho wenu Huyo ndiye aliye nyuma ya kufungiwa Mwanahalisi, Membe alikuwa TISS iliyogeuka Uhasama wa Raia. Ukichagua Membe umechagua TISS na Zoka na Ighondu!! tutapona kweli!!??
 
mikataba mingi ya hii nchi watakuwa wame sign bila kuisoma,huo mmoja tu ndo umeshtukiwa
viongozi wenyewe hawako makini kila mtu anatafuta pakulia!!
 
Huyu bwana kama walivo viongozi wengi wa CCM wanaona watu wengne ni kama misukule. Haya alifanya Karamagi kule London sasa na huyu kafanya kuna haja ya mikataba yote kabla ya kusainiwa ichapishwe magazetini angalau tuone jinsi tunavyodhalilishwa nakuhujumiwa labda wengne tutapinga.
 
Membe anagombea awe rais wa nani? sijawahi ata mara moja kusikia mtu akimsifia Membe, labda Kikwete tu! kama Membe angekuwa rafiki yangu wa karibu sana ningemshauri aachane kabisa na swala la urais.
 
Kichwa cha habari na video ni tofauti. Ungesema tu kuwa Naibu waziri wa Zanzibar anataka kuwa sawa na waziri kivuli wa JMT

Hahahahahaaaa! Hapo ndo ninapokupendea, kwa jambo linalokinzana
na mtazamo/maslahi yako ni lazima ubishe tu, tena kwa stamina ya ubishi...
 
Kuna siku nimewaza sana kama hiyo nchi yetu inahitaji viongozi au tungeweza kuwa better off without viongozi

Kila siku mimi nnashauri tuunde baraza la utawala hapa, kutoka nyanja mbalimbali za jamii (vyuo vikuu, mabaraza ya vijana, makanisa, misikiti etc..)..Tulipe baraza jukumu la kututeulia country CEO baada ya kufanya screening kama ya ajira ya kawaida,,sina shaka mtu kama Hu-Jin Tao ama Kagame (baada ya kustaafu Rwanda) wangeweza kutupelekea hii nchi pale ilipo Dubai in just 10-20 years...

Too bad wananchi wengi hawana uwezo wa kusoma katiba mpya,,,seuze kushauri mabadiliko ya vipengele vyake.
 
Malalamiko ya watanzania kwamba viongozi wanasaini mikataba bila kusoma sasa yamethibitishwa wazi na mwakilishi wa Dimbani zanzibar Bw.Mwinyi Haji Makame(CCM) kwa Bw. Bernad Membe ktk kile kuonyesha kuwa careless kwa kufikia kusaini mkataba ambao hakutakiwa kusaini ambapo mwakilishi anadai kwenye video hiyo iliyoko ndani ya youtube.

Mwakilishi huyo alipokuja juu mbele ya JK kwamba kwanini waziri wake amesaini Mkataba ambao si wake? JK kama kawaida yake ya kutetea uzembe alimuombea amsamehe kwamba hayo ni makosa ya kibinadamu tu.

Kwahiyo watanzania kilio chenu cha miaka mingi cha kulalamikia mikataba kusainiwa bila kusomwa sasa kimedhibitishwa wazi na Bw. Mwinyi kuwa viongozi ni watu wasio na huruma na nchi hii tunakupandisha ndege hadi China tunakulipa Posho za kukatana na shoka halafu still hufanyi kazi yako tunayokulipa nafikiri baada ya kuangalia video wale wote mliokuwa mnawaza labda Bw. Membe anafaa kuwa rais wa nchi hii mtabadili mawazo yenu. waandishi tusaidieni kumuuliza ilikuwaje asaini mkataba bila kusoma kwanza anachosaini??

Angalia video hii:

[/QUOTE

Foreign affairs is amongst the Union Matters (Constitution of URT, 1977 1st Schedule), and the person in charge of them is Membe! He was right, huyu jamaa wa SMZ hana locus stand in the presence of the Minister for Foreign Affairs for URT.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom