Membe anapowaita wa Malawi ''Wenzetu'' maana yake nini?

Don Draper

Senior Member
May 30, 2012
176
87
Je ni maofisa wepi wa Foreign waliandika speech ya Membe Bungeni? Kuna mtu alianzisha thread humu JF na kutuelezea maofisa wa Kimalawi walivyojipenyeza mpaka ndani ya idara nyeti za serikali na inanifanya nistuke kuwa inawezekana kuwa wengine wamemzunguka waziri Membe.

Zaidi soma hii thread:

Huyu waziri wetu wa mambo ya nje na ndiye duania nzima inamsikiliza akitoa kauli lakini kwa kauli hii hapa chini aliyoitoa bungeni haonekani kama ni patriotic na bado anaendelea kuwa treat Malawi as friends/allies wakati ukweli Mali ni hostile na hii inanifanya nijiulize hivi huyu mheshimiwa ambaye anatajwa kuwa anaweza kuwania urais in 2015 anazo guts za kuwa na credentials za kuwa touch on foreign adversaries? Piakutokana na ukweli kuwa aliwahi kuwa afisa mkubwa huko Usalama wa Taifa (TISS) na kwingineko serikalini inamaana huu mgogoro unatupatia picha ya namna gani anatatua migogoro akiwa commander in Chief wa Tanzania. Bwana Membe nafahamu unatakiwa utumie diplomatic language lakini umesahau kuwa mle ni Bungeni na ulitakiwa utoe kauli ambayo inge tupatia hamasa hawa jirani na wengine kuwa karata zote tunazo na tuko tayari kuzitumia at any time na sio kuwaita hawa wamalawi ''WENZETU''

haya ndio maneno yaliyonistua kutoka kwa Membe leo Bungeni:

68. Mheshimiwa Spika, baada ya majadiliano makubwa kati yetu na Malawi, Serikali yetu iliwataka wenzetu wa Serikali ya Malawi pamoja na kampuni za utafiti au uchimbaji kusitisha mara moja shughuli zote za utafiti hadi majadiliano yatakapokamilika. Ni matumaini yetu kuwa wenzetu wa Malawiwametuelewa. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa mgogoro huu mbele ya safari kutatuliwa na Msuluhishi badala ya sisi wenyewe.

Sitaki kumrudisha shule Mheshimiwa Membe lakini naomba upate nafasi usome hiki kitabu hapo chini ili uelewe as nations we do not trust anyone na pia naomba kukujulisha kuwa huwezi ku run foreign ministry kwa mitazamo ya idealism its about time ukawa realist tena hard core realist

119564429.JPG

In short Wa Malawi sio wenzu bali they are our adversary
 
Kama hoja ni neno 'wenzetu' basi sijaona hoja nashauri ukajipange urudi tena. Wamalawi ni wenzetu kwa kila hali, ni waafrika wenzetu na pia tumeingiliana kimakabila, tunao wanyasa upande wetu na wapo pia kwao, ni wanachama wenzetu ndani ya SADC nk. Neno "wenzetu" halimaanishi kuwa hatuwezi kupishana kimaslahi nao, hata ndugu wanapishana maslahi. Nashauri ubadilishe entry point
 
In idealist world usemayo ni sawa na ni lugha za kuwafundisha watoto wa Nursery

in a realist world wao hawatuoni kama ni wenzetu if anything wao wana act on their national interest na wako tayari kufanya lolote lile ku achieve hiyo goal yao

what we needed from Membe pale bungeni was a hawkish languageili galvanise wananchi. We really needed that. sio lugha za kubembelezana. Kisha language ya diplomasia angewaachia hao maofisa wanaonegotiate na hao waMalawi.

Hiyo ingesend a strong message kwa wa Malawi na naamini wangekuwa rattled na kesho tungesoma NYASA TIMES watakavyowabembeleza watu wao watafute suluhu ya haraka na Tanzania
 
nakubaliana na OP

Membe alitakiwa aonekane ni strong on national security issues

sio kuwaita hawa jamaa WENZETU

wangekuwa wenzetu wasingeleta kibri na dharau wanayotuletea leo hii

we need strong leaders na sio blah blah za wenzetu
 
In idealist world usemayo ni sawa na ni lugha za kuwafundisha watoto wa Nursery

in a realist world wao hawatuoni kama ni wenzetu if anything wao wana act on their national interest na wako tayari kufanya lolote lile ku achieve hiyo goal yao

what we needed from Membe pale bungeni was a hawkish languageili galvanise wananchi. We really needed that. sio lugha za kubembelezana. Kisha language ya diplomasia angewaachia hao maofisa wanaonegotiate na hao waMalawi.

Hiyo ingesend a strong message kwa wa Malawi na naamini wangekuwa rattled na kesho tungesoma NYASA TIMES watakavyowabembeleza watu wao watafute suluhu ya haraka na Tanzania

Sioni sababu ya Membe kutumia lugha kaaali kwa watu ambao unaweza kuwapiga kwa wiki moja ukafika upande wa pili wa mpaka wao na Zambia. Membe alitoa kauli ya Serikali sio ya NGO au Chama cha siasa. Lugha aliyotumia Malawi wamedhaielewa. Lugha aliyotumia pale ina signal nyingi ma consumer wake ni zaidi ya audience moja. Unahitaji upeo kuelewa hilo. I kama akitumia lugha kali leo, ikifika siku ya kutangazwa vita itumike lugha gani? Tatizo vijana siku hizi vijana hamjapita jkt.
 
Mzee hao ni sikio la kufa na ni watu wenye upeo mdogo, unahangaika bure kuwaelimisha. Wanashindwa kuelewa kwamba wenzetu humaanisha counterparts wetu na sioni tatizo hapo. Ikumbukwe kwamba Membe alitoa msimamo lakini hakutangaza vita na hata angekuwa anatangaza vita bado kutumia wenzetu kusingepunguza lolote. Mkiona hamna cha kukosoa ni lazima mtumwe kuanzisha thread tasa kama hii?
 
You are missing the point
Ile ilikuwa ni platform ya kuinform taifa kinachoendelea lakini pia ilikuwa ni platform for Membe kuonyesha credentials zake kama afisa wa Usalama wa Taifa na waziri mwandamizi wa Tanzania na pia ambaye yuko tayari kuilinda tanzania na maadui wa ndani na NJE including hao wa Malawi

The so called counterpart waziri wao wa mambo ya nje aliitisha press conference na kutoa lugha kazi na vitisho kwa Tanzania kuhusu huu mgogoro. Sasa mimi sioni sababu ya wewe kuwaita hao ni wenzetu wakati what we needed was a Hawk

Nimemwelewa mleta mada kuwa what the country need now is HAWK na sio DOVES ili kulinda nchi hii

the quest ion hapa ni kuwa yuko wapi yule Membe the Hawk wa operesheni ya vita kule Anjouan?

Hiyo lugha za diplomasia angewaachia akina Malamula.

Halafu kusema kuwa katika watu milioni 45 hakuna mwenye uwezo wa kufikiria mpaka atumwe then I beg to differ na nakushauri uanze ku think outside the box. Mjibu mleta mada na sio kumtisha. Hayo mambo ya kutishana ni mambo ya kizamani na namuunga mkono kuwa hatuhitaji kuongozwa na ma-idealist kwenye dunia ambayo imejaa hostile actors kama Malawi ambao wao wanaangalia self interests zao.

Its a 101 International Relations
 
Je ni maofisa wepi wa Foreign waliandika speech ya Membe Bungeni? Kuna mtu alianzisha thread humu JF na kutuelezea maofisa wa Kimalawi walivyojipenyeza mpaka ndani ya idara nyeti za serikali na inanifanya nistuke kuwa inawezekana kuwa wengine wamemzunguka waziri Membe.

Zaidi soma hii thread:

Huyu waziri wetu wa mambo ya nje na ndiye duania nzima inamsikiliza akitoa kauli lakini kwa kauli hii hapa chini aliyoitoa bungeni haonekani kama ni patriotic na bado anaendelea kuwa treat Malawi as friends/allies wakati ukweli Mali ni hostile na hii inanifanya nijiulize hivi huyu mheshimiwa ambaye anatajwa kuwa anaweza kuwania urais in 2015 anazo guts za kuwa na credentials za kuwa touch on foreign adversaries? Piakutokana na ukweli kuwa aliwahi kuwa afisa mkubwa huko Usalama wa Taifa (TISS) na kwingineko serikalini inamaana huu mgogoro unatupatia picha ya namna gani anatatua migogoro akiwa commander in Chief wa Tanzania. Bwana Membe nafahamu unatakiwa utumie diplomatic language lakini umesahau kuwa mle ni Bungeni na ulitakiwa utoe kauli ambayo inge tupatia hamasa hawa jirani na wengine kuwa karata zote tunazo na tuko tayari kuzitumia at any time na sio kuwaita hawa wamalawi ''WENZETU''

haya ndio maneno yaliyonistua kutoka kwa Membe leo Bungeni:

68. Mheshimiwa Spika, baada ya majadiliano makubwa kati yetu na Malawi, Serikali yetu iliwataka wenzetu wa Serikali ya Malawi pamoja na kampuni za utafiti au uchimbaji kusitisha mara moja shughuli zote za utafiti hadi majadiliano yatakapokamilika. Ni matumaini yetu kuwa wenzetu wa Malawiwametuelewa. Hata hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa mgogoro huu mbele ya safari kutatuliwa na Msuluhishi badala ya sisi wenyewe.

Sitaki kumrudisha shule Mheshimiwa Membe lakini naomba upate nafasi usome hiki kitabu hapo chini ili uelewe as nations we do not trust anyone na pia naomba kukujulisha kuwa huwezi ku run foreign ministry kwa mitazamo ya idealism its about time ukawa realist tena hard core realist

119564429.JPG

In short Wa Malawi sio wenzu bali they are our adversary

"Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja". Membe na wengi wetu tulilelewa kwa IMANI hii. Mimi sikujaliwa kuwa mwana TANU ila nilikuwa kijana wa TYL. baadaye tulikuwa vijana wa CCM kabla ya vyama vingi.
Tulifundishwa upendo, uaminifu na Ulinzi.
JKT vijana wote tulifundishwa mbinu za medani. ninachotaka kusema ni kuwa: Membe kusema wenzetu hana maana ni soft ama msaliti. Wala usidhani kwamba Membe haoni au hajui uzito wa swala la Malawi kuanza chokochoko.
Hawezi kuanza kutukana ama kuwatisha wamalawi ama usingetegemea speaker awafukuze kutoka ndani ya bunge juzi. APPROACH ndiyo key word hapa. Membe yuko kwenye right track, lugha ya kibabe, ukali na matusi, haviwezi kuwafanya wamalawi au mtu yeyote akuogope. Mazungumzo na upole vina nguvu kubwa. Baada ya hapo ni KUPIGA kwa vitendo siyo maneno.

Hivyo kelele na kujitia kujua kusema haviwasaidii saana. Mjitahidi kuanzisha mijadala ambayo tutajadili in a constructive mature way siyo kukurupuka tu.
Hivi kweli we ukiambiwa leo uende kupigana na Malawi utaweza?
 
Mtu anatangaza vita ya kuja nyumbani kwako na kumbaka mkeo na kuua wanao bado unamwita mwezako?
 
Someni makala iliyoandikwa na Ndugu JAMES ZOTTO

Sakata la mpaka kati ya tanzania na malawi: POLITICS VERSUS FACTS

Ndugu zanagu, huenda mnafuatilia vizuri tatizo la mpaka wetu wa ziwa nyasa na malawi! Nilishtushwa sana na hotuba ya bwana waziri. mimi napenda utaifa wangu na uzalendo wangu. lakini napenda sana kutetea mambo yangu kwa kuukubali ukweli, kujua facts zaidi, kukubali hata zile zinazonipinga na ndipo najipanga kujenga joja.

Eneo hili nafanyia study yangu ya PhD. Sidhani kama nipo sahihi zaidi na lengo langu si kusema nani anamiliki nini! Ukweli naoufahamu, tatizo si kubwa kivile kama tunavyolifikiri kama tutachukua muda kupitia documents zote na muhimu. Tunahitaji kwenda Public Records Office-Uingereza, Colonial Archives Potsdam, ujerumani, pia malawi national archives, tanzania national archives, libraries za UDSM na Chancellor college malawi. naamini ubishi utaisha kwa kuwa documents zote zipo.

Angalizo: ziwa nyasa liligawanywa na mabeberu wa kiingereza, kijerumani na kireno. mkataba wa 1890 uitwao anglo-german agrrement unasema mpaka wa German east africa(tz bara ya leo) na nyasaland(malawi ya leo) unapita kandokando ya ziwa nyasa kutoka mto ruvuma mpaka mto songwe! huu ni mkataba wenyewe, upo ktk documents nyingi sana.....!!international law inajua hili na international lawyers wanaelewa nini nazungumza! Sehemu nyingine ilikuwa ni 1891 kati ya ujerumani na ureno, mpaka ulianzia mto ruvuma kuelekea Portuguese east africa(msumbijin ya leo) na pia ureno ikawekeana mpaka na british nyasaland(malawi)...kwahiyo, kipindi cha ujerumani, mpaaka unasomeka 'it passes along the shore of the lake(nyasa).....

Mabadiliko ya mipaka: kipindi cha kikoloni, kabla ya mjerumani kuondoka, marekebisho ya mipaka yalifanyika kati ya mjerumani na mreno kwa kuspgeza mpaka mbele 0.5 KM from the original tripartite point, na vijisiwa vya mto ruvuma vikagawanywa. mpaka leo ipo hivyo. na eneo lingine ni kati ya mwingereza na mreno, ambapo, kisiwa kilichopo eneo la malawi linamilikiwa na msumbiji mpaka leo na eneo la ardhi lililopo msumbiji linakaliwa na malawi. mhuo ulikuwa mkataba wa marekebisho na ipo hivyo mpaka leo. kwahiyo, tulivyorithi mipaka, tumerithi na mabadiliko haya na hivyo hatuwezi kugombana na msumbiji wala msumbiji hawawezi kugombana na malawi. Mpaka wetu na malawi haukurekebishwa popote pale mpaka mjerumani anatoka...

Marekebisho ya mipaka kipindi cha uingereza: sote tunajua german east africa, sisi pamoja na ruanda na urundi tuligawanywa katika sehemu mbili, ttukiwa chini ya League of nations tukiangaliwa na uingereza. Kunamabo nahitaji tuweke sawa. tukaitwa mandated territory na uingereza ni mandatory power. turudi ktk kamusi tutofautishe a an annexed colony and a mandate! Mpaka ukawekwa kati ya ubelgiji na uingereza, uliitwa the MILNER-ORTS AGREEMENT OF 1922! katika mkataba huu, mto kagera ulikatwa katikati na mpaka leo tumerithi hivyo. Hapakuwa popote pale ambapo eneo la ziwa nyasa lilirekebishwa kwa njia ya mkataba baina ya nyasaland state na tanganyika state...., isipokuwa, tofauti na mandates zote, tanganyika pekee, ilikuwa na tofauti ndogo, ambapo, mpaka wa ziwa nyasa ukapewa wanachoitwa 'wording', na hivyo, ramani ya tanganyika na official records zikaonyesha kuwa mpaka umepita katikati ya ziwa nyasa! na hapa ndipo tatizo linapoanza na sisi tumechukulia hii ndo absolute fact, hatuendi mbele kidogo. haya yapo pale national archives secreatarita files, ACCESSION NUMBERE AB 8 na AB 30! nafikiri hotuba yote ya bwana mkubwa jana imetoka ktk files hizi, ndizo walizopelekewa!!!

twende mbele kidogo, ni kweli, kama mheshimiwa alivyosema jana, ramani nyingi kuanzia 1922 mpaka 1939 zinaonyesha mpaka upo katikati ya ziwa! je, ukweli huu utatutosha pekee mbeleni tukifikishana mbali? hapana!mheshimiwa hakusema kuwa ramani zingine, japo chache muda huu huu na official reports hazionyeshi mpaka au zinaonyesha mpaka upo chini. lakini ni chache! kwanini hili?bado natafuta majibu, lakini kwa harakaharaka, unaweza ukasema kuwa uingereza ilitamani tanganyika iwe koloni lake na si mandate! na pia ilishinikizwa na wawekezaji na hata jeshi ilisema afadhari waiteke ili liwe koloni na waachane na mandate! nahitaji tuelwe maana ya mandate.

Hii yote ilitokea baada ya Donald Cameroon, governor wa tanganyika kusema kuwa tanganyika is a part of the british empire and it will remain so! hii ni siasa na si ukweli kama unaelewa maana ya kuwa wao hawakuwa wamepewa koloni kama mali yao, bali kuliangalia mapaka wananchi wapate 'akili' ili wapewe uhuru! kwa hiyo, kimsingi, kwa maana ya sheria ya kimataifa, tanganyika haikuwa part ya british empire kama yalivyo makoloni yaliyotekwa mojakwa moja na uingereza yenyewe! hapa pakatokea mvutano mkubwa sana katika house of Lords na house of commons! na hivyo basi, mtafaruku huu wa mpaka ulianzia hapa, kwa kauli hii na hivyo hata waingereza wenyewe walivutana kuhusu mpaka. ipo hivi, mwaka 1926, wajumbe wa mabaraza waliibana serikali iseme mipka ya tanganyika na ule wa ziwa nyasa! mabishano, kama haya yetu leo yalikuwa makubwa, ila si kwa kutishiana kwa kuwa walikuwa wenyewe na walitaka kuwekana sawa! ndipo secretary of state for colonies alibanwa na mjadala ulikuwa wa kisheria zaidi ukihoji status of the mandate, british empire, n.k; na kama waingereza wanamamlaka ya kujipangia kuhusu koloni waliolokabidhiwa kuliangalia(nieleweke na si kulimiliki)! mwishowe, mtu huyu mwenye dhamana alisema kwamba, hata yeye anashindwa kuelewa, 'what exactly is the sovereignty of tanganyika lying'! jamani mnamwelewa huyu mtu? kwamaana hiyo, haelwi vizuri mipaka yetu, ambayo wenyewe ndo wameirekebisha au kuipa 'wording'!! hivyo, tatizo linaanzia hapa na si muda mwingine wowot!!!

Kipi hakusema bwana mkubwa jana: kuanzia 1939, mambo yalibadilika na hawa hawa watu tunaochukua ashahidi kutoka kwao, wakafanya madudu! na ilipoisha vita ya pili ya dunia, jamani oneni haya, hawa waingereza katika ramani zao, tena nyingi mno,(kaangalieni East africana section, university of dar es salaam, sehemu ya thesis, kuna cabins 3 zimejaa ramani na bado ni mpya sana kutokana na kutunzwa na pia kutotumka sana), kuimbezinaonyesha, bila shaka yoyote, kuwa mpaka wa tanganyika na nyasaland unapita pembeni mwa ziwa na si katikati! mkuu hakusema hili. aliishia 1939! kumbe hawa jamaa walichora tena ramani zote zikionyesha mpaka upo pembeni mwa ziwa!!!! kwanini hili?natafuta majibu, lakini nkwa haraka naweza nikaspeculate mawili. mosi, karibu na vita vya pili vya dunia, ilisikika tetesi kule duniani kuwa, ujerumani inarudi na inakuja kuchukua malokoni yake. (kasome national archives of tanzania, secreatariat files zote zenye kichwa cha habari, 'the future of tanganyika in british empire'). kwa hiyo, waingereza walihofia kutimuliwa na kurudi kwa wajerumani, na hivyo, wakarudisha ule mpaka wa awali wa 1890! na pia, muda huu, baada ya kwisha vita, tanganyika ikawa chini ya UNO ambapo ilipewa trusteeship status!maana ya hii ni rahisi kuliko mandate!ilimaanisha to be granted immediate independence! maana ya neno immediate hapa ni kwamba, kwa tafsiri yangu, waingereza wlifahamu wanatimka mapema mno kwani mkataba unasema hivyo....nafikiri, wakarudisha ramani zikionyesha mpaka upo pembeni...na kitabu ch Nyasaland cha mwaka 1958, kinaonyesha mipaka ya nyasaland na ziwa lote likiwa kwao! tukitaka kuwashinda wamalawi, lazima tukisome vizuri kipindi hiki na tuelewe facts zipi zinawapa kiburi na zipi sisi tuzitumie, la sivyo, tunaweza.............!!!!!!!!!!!!! kwahiyo future of tanganyika ilikuwa contested, uncertain, etc kipindi hiki, pamoja na mipaka yake pia!! tujiulize, kwa maana ya mandate, waingereza walikuwa na legal authority 'kurekebisha' mpaka wa ziwa nyasa? na je makosa waliyofanya waingereza, ndo legal backing yetu sisi? ebu tuzame tena tutafute facts tuwashinde hawa jamaa!

Tulishindwana na uingereza kurekebisha mipaka. mwalimu alisubiri mpaka malawi iwe huru!akatoa miaka mitatu tu na asingetambua mipaka ya kikoloni(soma hansard, 1962). walipopata uhuru, kukawa na matatizo ambayo jana bwana mkubwa aliyaeleza. nampongeza ni dhahiri, 1964 cabinet crisis ya malawi na wale mawaziri kutorokea nchini kwetu kupitia ziwa, banda akaona ziwa ni infiltratio route! sera zetu za mambo ya nje zilikuwa tofauti. tulikuwa frontline state kwa ukombozi, wenzetu wakasapoti makaburu na wareno na wakawa na balozi sehemu hizo.....wakagombana na mwalimu, military show down miaka ya 1967-8; matusi na kejeli zikatawala kati ya mwalimu na banda, sisi na malawi.....kipara cha banda kinamagamba, tuliimba tukiwa jeshini, mwalimu akasema mpaka a sensible leader akitokea malawi ndipo tutajadili tena swala hili na si na kamuzu banda! tulikuwa kimy, na kuanzia 1975, hatukuwa na tatizo,lakini si kusema kuwa tulitatua tatizo la mpaka!

Tulikaa kimya!mipaka haina tatizo isipokuwa ni time bomb ambapo ikitokea spark ni explosion! Tuliirithi kupitia Article III ya OAU CHARTER ya 1964 BAADA YA DEBATES KUBWA NA WENGI WAKARIDHIA TUIRITHI, uti possidetis, ita possidetis principle (so as you exist, so may you exist), kama kawaida yetu tulidesa ya kibeberu, Westphalia principle, border inviolabiliy! hatukupata muda mwingi wa kutafakari na kuangalia kila mpaka na matatizo yake....tulirithi na matatizo na yanatutatiza leo!!!

Way forward! naikiri tuna namna tatu ya kulimaliza! moja ni kwa majadiliano ya kawaida yaani diplomacy kama bwanamkubwa alivosema jana. pili ni kupigana vita. (war is another means of diplomacy), mnataka kuniona kichaa!huo ndo ukweli, atakayeshindwa atasalimu kama ilivyokuwa kwa uganda na sis. tatu ni mahakama ya kimataifa yaani International Court of Justice! hapa ninawasiwasi. kama facts zenyewe ni zile za jana tu, sijui kama tutatoka.tutulie, tuite wataalamu wetu wajikite ndani sana. ni kweli kama alivyosema jana bwana mkubwa kwa kunukuu kesi nyingi na zilizoshinda, na kwa kusema kuwa, tukienda mahakama ile sisi ndo tutashinda!!!ninashaka....tumejipa favour ya verdict! kabla ya kesi.sijui.ninashaka kubwa!kunakushinda, kushindwa au suluhu!ninashaka tena na tena!

mimi nimzalendo,nataka ukweli kwa njia ya mahojiano na kuumiza kichwa, tutetee mali zetu tukijua tunawashinda kwa hoja.....!!!!

Wasiwasi: inasemekana kuna mafuta ziwani!!! kwahiyo mjue marekani na washirika wake hawako mbali! tujue operation ya military imperialism na huyu mama, mpwa wa kamuzu banda, anapata wapi hiki kiburi...nyuma yake kuna nini na nani!!1tuangalie haya pia.

Hitimisho. tusiwe na hoja moj tu mkononi kama ndo water-tight evidence. tujaribu kuzibishanisha hoja zetu. na hoja nzuri ni zile zinazopingana nasi na tusizozipenda, tukizielewa na kuzikubali ndipo tutajipanga namna ya kuzigalagaza. tumwelewe vizuri adui yetu.....MUNGU IBARIKI TANZANIA!ZIWA NYASA!WANYASA!WATANZANIA!

Tusing'ang'anie tu REPARIAN LAW!
 
Sioni sababu ya Membe kutumia lugha kaaali kwa watu ambao unaweza kuwapiga kwa wiki moja ukafika upande wa pili wa mpaka wao na Zambia. Membe alitoa kauli ya Serikali sio ya NGO au Chama cha siasa. Lugha aliyotumia Malawi wamedhaielewa. Lugha aliyotumia pale ina signal nyingi ma consumer wake ni zaidi ya audience moja. Unahitaji upeo kuelewa hilo. I kama akitumia lugha kali leo, ikifika siku ya kutangazwa vita itumike lugha gani? Tatizo vijana siku hizi vijana hamjapita jkt.

I hate this kind of allusion.......Watanzania bana wapi kulishindanishwa majeshi ukaona jeshi lako ni bora kuliko mengine..........
 
I hate this kind of allusion.......Watanzania bana wapi kulishindanishwa majeshi ukaona jeshi lako ni bora kuliko mengine..........

Kitinku

Huhitaji utafiti mpya maana tafiti zipo. Jeshi ll tanzania ni moja ya majeshi imara afrka na haswa kusini mwa afrika. Jeshi letu lina sifa ya ziada ya kupigana vita na kushiriki kwenye vita vingi. Jeshi la Malawi halijawahi kupigana. Aidha hata kwa upande wa vifaa pia si haba. Wamalawi wanalijua hilo na wanafahamu kilichowakuta 1967 ndio maaana hukuskkia fyoko yoyote hapo katikati kuhusu mpaka.
 
Back
Top Bottom