The Boss
JF-Expert Member
- Aug 18, 2009
- 49,228
- 116,840
Wale ambao hawakuwepo zamani na hawajui kilichotokea kipindi hiko basi ni vizuri tukawasimulia kidogo Kuelekea uchaguzi wa mwaka 1995 CCM walikuwa na kambi mbili kubwa ya kwanza ilikuwa ya John Malecela Waziri mkuu na ya pili ilikuwa ya Horace Kolimba alikuwa katibu mkuu wa chama...
Upinzani ulikuwa mkali sana hadi Mwl. Nyerere alipoingilia kati na kutunga kitabu akiwaponda wote wawili akiwataka wajiuzulu waliposhindwa zuia hoja za serikali ya Tanganyika ,Baada ya Mkapa kuapishwa na kuanza kuongoza....Kolimba akajitokeza hadharani kuikosoa na kuiponda serikali ya Mkapa maneno yake maarufu yalikuwa 'serikali haina dira wa muelekeo'..
Alipoongea maneno hayo CCM wakamuita kumhoji Dodoma akiwa katikati ya kuhojiwa..akafariki....ndio chanzo cha maneno maarrufu 'watakukolimba' maneno haya hasa yalianzishwa na Mchungaji Mtikila ambae alisisitiza Kolimba 'alichezewa' faulo....
Baada ya leo Membe kumkosoa hadharani Magufuli kwa jinsi anavyoendesha serikali yake na baada ya leo kumuona Magufuli akiwa ndani ya uniform za JWTZ.. nimejikuta najiuliza......'Membe anamkumbuka Kolimba'?
CCM wote akiwemo Membe walisisitiza Magufuli ni chaguo sahihi ni mtu wa kufanya utumishi wa kutukuka na atakuwa Rais bora kabisa sasa mbona wanaanza kumkosoa hata miezi minne bado?
Si wamuache 'Rais wetu mpendwa apige kazi'? wanahofia nini? wameona dalili zipi? lakini je wanamkumbuka Kolimba?