Membe akwama kutangaza nia

Membe akwama kutangaza nia

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2008
Posts
10,942
Reaction score
437
* Hotuba ilibadilishwa uwanjani

* Makonda aficha kwapani hotuba

Kweli alipangalo Mungu sio alipangalo mwanadamu na siku zote mipango sio matumizi. Hii imekuja kujidhirisha katika tamasha la pasaka lililofanyika jana ambapo lengo mficho la tamasha limeshindwa kutimia.

Tamasha hilo ambalo lilifanyiwa promosheni ya nguvu liliishia kupata watu kidogo, hali iliyopelekea mgeni rasmi kuchelewa kuingia uwanjani badala ya kuingia saa 9 aliingia saa 11 jioni.

Mgeni rasmi ambaye alikuwa Waziri Membe alipanda jukwaani saa 11 na robo badala ya saa 10 kamili kama ilivyokuwa imepangwa kwenye ratiba.

Vituko vilijitokeza wakati wa kumuita mgeni rasmi jukwaani ambapo aliitwa mgeni rasmi Membe na wakati huo huo kukiendelea na maonyesho ya sarakasi ambapo watu waliishia kuangalia sarakasi na hivyo kumlazimu mgeni rasmi Membe kusimamishwa kwa zaidi ya dakika 20 jukwaani bila ya utaratibu wowote.

Mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi kwa mgeni rasmi Membe ambaye aliambatana na Dc wa kinondoni, Paul Makonda kwa kutoshangiliwa wakati wakitambulishwa hali iliyomlazimu Membe kubadili mwelekeo wa dhamira mficho wa shughuli hiyo.

Membe alishauriwa na Makonda asitishe zoezi lake la kutangaza nia na hapo ndipo Membe alipoamua kubadilisha hotuba yake na kubuni ya amani kwa vijana badala ya ile ya kutangaza nia na kuishia kula keki ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kujipongeza kwa tukio la kutangaza nia lililo gonga ukuta.

Kitendo kile cha kushindwa kutangaza nia kutokana na uwepo wa watu wachache uwanjani pamoja na kukosekana kwa shangwe nyingi kwa Membe uwanjani vilimnyima sana raha Membe na wakati wote alikuwa amepooza na mwenye msongo wa mawazo hadi kushindwa kwenda kuungana kucheza na mwimbaji wa kimataifa Rebecca Malope kama alivyokuwa akiombwa mara kwa mara na mc wa shughuli hiyo.

Membe alitumia jumla ya Tsh. milioni 30 kwa tamasha hilo ili aje atangaze nia lakini akagonga ukuta na haijajulikana ni lini tena atapanga kutangaza nia kwani mpaka sasa upepo wa kisiasa sio mzuri kwake.
 
Aite press conference. Membe hawezi kuwa raisi wa yeyote zaidi ya ccm. Na ccm hatuwappi nchi tena!.
 
poleee sana mh membe kwa kukosa watu daaah siasa kweli mchezo mchafu
 
Samahani katika team Lowassa ukiposti taarifa kama hii ya kumponda Membe unalipwa shilling ngapi?
 
Habari hii imekaa kiudaku sana japokuwa ni wazi Membe alikuwa kwenye kampeni zake za Urais ndani ya CCM.
Vipi kuhusu kundi la vijana wa Lowassa lililoandaliwa kumzomea Membe na kuripotiwa na magazeti jana?
 
Mleta Uzi ni team 4u movement ya mafisadi. Kwani membe hajui kuwa ccm muda Wa kampeni bdo mpaka aende pale kutangaza Nia?
 
Jana hadi wapambe wake akina Richard Kasesela (mshika mikoba), Nape na Issa Gavu wote walimkimbia na kumwacha mpweke kiwanjani. Kweli kwenye shida haumuoni hata ndugu yako
 
uzi umekaa kimbea.ila jamaa hafai kuwa mkuu wa kaya hatuhitaji tena diplomat kuwa kiongozi tumechoka na maxcm
 
​siipendi sisiem lakini mleta mada umeonyesha ushigongo..........hebu lete wwe hiyo hotuba ya kutangaza nia tuione kwanza
 
Hilo tamasha naona hata coverage ilikuwa poor naona ITV Na channel 10 walilipotezea. Team wamma wataendelea kuchina siwapendi magamba ila Wama ni zaidi
 
Jana hadi wapambe wake akina Richard Kasesela (mshika mikoba), Nape na Issa Gavu wote walimkimbia na kumwacha mpweke kiwanjani. Kweli kwenye shida haumuoni hata ndugu yako

Hivi lile basi alilopeleka dayosisi ya Tabora lilipokelewa?
 
​siipendi sisiem lakini mleta mada umeonyesha ushigongo..........hebu lete wwe hiyo hotuba ya kutangaza nia tuione kwanza

Akina Msalani wapo kazini. Halafu maji yakizidi unga watakuja ooh Bavicha!!
 
mleta uzi ingependeza ungeweka hapa copy ya hiyo hotuba ya kutangaza nia ili watu waamini kile ulichoandika. Wachangiaji wengi wanaona kama hii habari ni umbeya Fulani toka kwa team nyingine ya mgombea. Ungeondoa huo utata kwa kuweka copy ya hotuba iliyowekwa kwapani
 
Mleta maada kweli hata hujui kubuni umbeya. Membe sidhani ni mwehu kiasi kile akatangaze nia kwenye tamasha la Pasaka. Kama ndicho mlikua mnakingoja basi mliteleza
 
Mleta Uzi ni team 4u movement ya mafisadi. Kwani membe hajui kuwa ccm muda Wa kampeni bdo mpaka aende pale kutangaza Nia?
Kwani walipopewa adhabu na chama chao walikuwa hawajui kwamba muda wa kampeni bado?
 
Back
Top Bottom