Membe akiri serikali ya CCM kufanya ujinga

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,225
Wakati akihojiwa na mwandishi wa TBC kuhusu maoni yake baada ya kutembelea chuo cha ufundi huko singapore katika ziara ya Rais kikwete leo hii, amekiri serikali kufanya ujinga kwa kubadilisha vyuo vya ufundi kuwa vyuo vikuu,
"Tumefanya ujinga saana, tusifanye hivyo tena, makosa tuliyofanya huko nyuma yanatosha" mwisho wa kunukuu.

katika ziara hiyo imeelezwa kuwa wanafunzi asilimia 75 nchini singapore wanajifunza masomo ya ufundi, na asilimia 25 ndo wanaosoma masomo ya kawaida, katika chuo hicho asilimia 99 ya gharama za masomo zinalipiwa na serikali.

source TBC 1 habari
 
Prince Tumbo

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
910
0
Tanzania haiwezi kulipia gharama za masomo kiasi hicho, hakuna viongozi wenye maono, ccm huandaa taifa la wajinga kwa kuwa ndio mtaji wake,fedha nyingi hufisadiwa na zingine kwa ajiri ya safari za rais...very awkward
 
ziara za Rais kikwete ni utalii tuu, hakuna cha kujifunza
 
Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,000
Unajua tungewekeza kwenye Sayansi sahizi tungekuwa tunaongea kitu kingine si Siasa tena. Wezentu wako mbali sana na wanaheshimika kuliko sisi tuowekeza kwenye midomo ya watu
 
Master plan

JF-Expert Member
Dec 24, 2012
3,669
2,000
Kwa kifupi hajazungumzia uongozi wa serikali ya kuanzia 05-015 kapga majungu na serikali iliyopita
 
mdeki

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
3,304
1,225
Ndiyo anajua leo umuhimu wa hivyo vyuo?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kinauche

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
7,685
2,000
Wakati akihojiwa na mwandishi wa TBC kuhusu maoni yake baada ya kutembelea chuo cha ufundi huko singapore katika ziara ya Rais kikwete leo hii, amekiri serikali kufanya ujinga kwa kubadilisha vyuo vya ufundi kuwa vyuo vikuu,
"Tumefanya ujinga saana, tusifanye hivyo tena, makosa tuliyofanya huko nyuma yanatosha" mwisho wa kunukuu.

katika ziara hiyo imeelezwa kuwa wanafunzi asilimia 75 nchini singapore wanajifunza masomo ya ufundi, na asilimia 25 ndo wanaosoma masomo ya kawaida, katika chuo hicho asilimia 99 ya gharama za masomo zinalipiwa na serikali.

source TBC 1 habari
Siku zote alikuwa hajui? Sasa ana mpango gani? Wa mgombea binafsi au?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,218
0
Kwani hilo Na mengine mengi hawakuyajua hadi muda wao wa kuachia madaraka unapokaribia?

Kwani tunapowapigia kelele Na kuwasema kwa kuendekeza ufisadi Na kuua taifa letu kwa kufawa rasilimali zetu kwa wageni na kuua elimu wanatuonaje?

Basi wamechekewa, wajiandae tu kuondoka
 
G. Activist

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
482
250
Wakati akihojiwa na mwandishi wa TBC kuhusu maoni yake baada ya kutembelea chuo cha ufundi huko singapore katika ziara ya Rais kikwete leo hii, amekiri serikali kufanya ujinga kwa kubadilisha vyuo vya ufundi kuwa vyuo vikuu,
"Tumefanya ujinga saana, tusifanye hivyo tena, makosa tuliyofanya huko nyuma yanatosha" mwisho wa kunukuu.

katika ziara hiyo imeelezwa kuwa wanafunzi asilimia 75 nchini singapore wanajifunza masomo ya ufundi, na asilimia 25 ndo wanaosoma masomo ya kawaida, katika chuo hicho asilimia 99 ya gharama za masomo zinalipiwa na serikali.

source TBC 1 habari
Watalaamu waliyaona haya na kuyapigia kelele, mafundi mchundo ingali wanahitajika sana nchini, hasa katika nchi hizi zinazoendelea lkn wanasiasa kama ilivyokawaida wakaziba masikio na kuruhusu hilo ili kujijengea historia..

Na bado sana kunamengi tu watajua yaliyofanyika yalikuwa madudu!! tz inashangaza..
 
Farudume

JF-Expert Member
Jan 10, 2013
3,955
2,000
Sasa kama wanawekeza kwenye Siasa unategemea nini.Spika anateuliwa kwa Kigezo cha Jinsia na Sio Uwezo wa Kiuongozi alionao.Nayo Tume ya Katiba inataka kila Jimbo awepo Mbunge Wakike na Kiume.Sidhani kama tutafika kwa Mwenendo huu.
 
Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,572
2,000
Kuna kitu kiko kichwani kwangu kua Raisi wa nchi hii anahujumiwa na walioko chini yake!
 
sir.ben

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
388
170
Kuna miccm humu rais akisema tumeweza waambien na wengine inakuja huku kushabikia, ijifunze kufikiri, watazame marais wakimaliza muda au kukaribia,kaul zao hubadilika leo kikwete kakiri ubovu wa ccm, mkapa anatuambia jins ccm ilivyo mbovu, ni nyerere pekee aliyekubal kuna mapungufu akasema tuchukue hatua,leo tunaona ,wakina-sita,lowasa,kikwete n.k wanakir rushwa ipo ccm lakin kwa ushabiki wakina mgeja wanapinga na kudai kama lowasa kaona rushwa awapeleke mahakaman,vp kuhusu kikwete. Naomben msitumiwe jaman,msikurupuke jf kutetea ujinga,panapo hak toa hak.
 
sir.ben

JF-Expert Member
Feb 14, 2013
388
170
Dodoma kuna shule zilikuwa na vifaa vya ufundi mpaka uselemara,kutengeneza vifaa vya umwagiliaj(maken),kibatar,visu,majiko,masufuria,ushonaj,kilimo n.k vilifundiswa.wakat huo nikiwa darasa la 1 (1997), leo wiz tu hata spare ya cherehan hakuna, ilikuwa madawat yakivunjika, kupitia somo la ufund yalitengenezwa, leo shule hizo kwa jins zilivyokuwa na majengo meng nying wamegeuza kuwa sekondar mfano shule ya mpunguz dodoma, sasa angalia shule walipohamishiwa wanafunz wa primary chekechea wanakaa chin na mara nying nje, ndipo serikali inapotupeleka,lazima tuwe na kauli ya kusema hapana.
 
ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
325
0
Huyu hana jipya anapiga siasa...Urais 2015 hawezi kuupata kwa cheap politcs kama hizi anazopga wenzake walishajenga adi shule za swekondari nchi nzma anaongelea VETA za nyerere leo
 
Top Bottom