Membe akalia kuti kavu CCM

Membe akalia kuti kavu CCM

Si unakumbuka kilichomkuta kolimba? Sijui umri wako ndugu, lakini mtu yoyote over 40 lazima atalijuwa hili. CCM siyo watu wa spoti spoti.

Hahah wakimuamulia Membe aisee ni dakika tu wamemaliza kazi,utaanza kusikia tu pengo lake halizibiki sijui nini.
 
Huyo atoki Leo wala kesho anaogopa mtaani keshaharibu ataishije
Acha waparuane wenyewe ila hilo likifanikiwa basi Ccm wajiue tu jina limebadilika kutoka Chama Cha Mapinduzi = Chama Cha Magufuli.

Na kumng'oa nduli hapo magogoni iwe kwa kikatiba au kinguvu itawawia vigumu.

Pia upinzani wa majukwaa ya kisiasa i.e CDM/ACT ndiyo utakuwa kwishnehi (japo upinzani upo mioyoni) ila hakuna atakayethubutu kunyanyua mdomo.

Mi naona turufu ya wanaccm kuonesha kuwa chama kina nguvu ni kuzuia na kupinga dhuruma itakayofanyika hapo unless they are all finished na hakuna atakayekuwa salama.
 
Hawa watu wa ccm wanakuwa na nguvu tu wanapokuwa huko huko ccm lkn wakitoka tu ndio end of the game to them. Tumeona kwa wengi.

Ile dhana ya kuwa upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm mimi sikubaliani nayo kabisa kwani naona hawa wanaotoka ccm kuja upinzani ndio wanaoudhoofisha upinzani. Siku wapinzani watakapogundua hili hawatabaki hapa walipo tena.
 
🤣🤣 chama si cha demokrasia na hicho kwan mwanachama akiwa na qualification za kugombea uraisi si anaruhusiwa mbna wana hamaki namna hiyo?
 
VIKAO vya Kamati Kuu (CCM) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vinatarajia kukaa wiki ijayo, huku agizo la Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Bashiru Ally la kumtaka ofisini kwake kada wachama hicho Bernard Membe, likiwa halijatekelezwa. RAI linachambua.View attachment 966775

Ingawa haijaelezwa vikao hivyo vitafanyika Dodoma ama Dar es Salaam, tayari imeshatangazwa kuwa vitafanyika kwa siku mbilimfululizo, Desemba 17 na 18 mwaka huu.
Moja ya ajenda ya vikao hivyo imeshawekwa wazi kuwani uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar.

Ikiwa imesalia miezi 12 kufikia mwaka 2020, imeelezwa kuwa chama hicho kitawasilisha ile ya mwaka 2015 hadi 2020.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanavitazama vikao hivyo kwa sura mbili, moja ikiwa ni kutathmini mwenendo wa mambo ndani na nje ya chama hicho na pili ni kushughulikia makada wao ambao wanaonekana kwenda kinyume na matakwa ya CCM mpya.

Wapo baadhi ya makada wa chama hicho ambao pia ni wabunge wamepata kunyooshewa vidole hadharani na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Miongoni mwao ni Bernard Membe (Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), ambaye hivi karibuni jina lake liliingia kwenye mjadala mkali baada ya kutakiwa kufika ofisini kwa Dk. Bashiru ili akajieleze.

Membe ambaye bado hajatekeleza agizo hilo, ametakiwa akajieleze baada ya kuwapo kwa tuhuma za kuendesha mikakati ya kutaka kumkwamisha Rais Dk. John Magufuli.
Ilidadavuliwa kuwa nia ya Membe ni kutaka kuwania urais mwaka 2020 huku akijua wazi kuwa utamaduni wa chama hicho tangu kurejea kwa chaguzi za vyama vingi ni kuachiana kwa vipindi viwili.

Ingawa Membe hajawahi kusema chochote kuhusiana na siasa tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike na yeye kuishia kwenye hatua ya tano bora, ameingia kwenye tuhuma hizo kutokana na taarifa zilizowahi kuripotiwa na moja ya magazeti ya kila siku nchini.

Hatua ya Katibu Mkuu wa chama kumtaja moja kwa moja Membe hadharani, inatafsiriwa kama hatua ya kumweka katika kona, hatua inayoweza kuibua uamuzi wa kumvua uanachama, kama ilivyopata kufanyika kwa baadhi ya makada akiwamo Sophia Simba, ambaye amesharudishwa kundini.

Wachambuzi wa mambo ya siasa wanaamini kuwa vikao hivyo vya juu vya chama, havitaweza kupita salama bila kuwagusa makada wake wanaoonekana kwenda kinyume na matakwa ya chama, akiwamo Membe.

Membe anaingia kwenye tanuru hili huku kukiwa na kumbukumbu ya kunusurika kuvuliwa uanachama mwaka 2014 baada ya kutuhumiwa kuanza kampeni mapema, yeye na makada wengine watano.

Mwaka 2014 Membe alilazimika kukaa nje ya ulingo wasiasa kwa miezi 12, akiwa pamoja na aliyekuwa hasimu wake ndani ya CCM, Edward Lowassa, Januari Makamba, Frederick Sumaye, William Ngeleja na Stephen Wasira.
Adhabu yao ilikoma mwaka 2015 na kukutwa hawanahatia, hata hivyo kwa mwenendo wa sasa wa CCM mpya, upo uwezekano mkubwa wamwanasiasa huyo ambaye jina lake limerejea kwenye siasa za mitandaoni kwa kasi akakumbana na adhabu kali zaidi itakayomweka nje ya siasa za chama chake.

Hatua ya kuitwa kwake ambayo ilionesha kuwashangaza baadhi ya wakongwe wa chama hicho, inaibua fikra za moja kwa moja kuwa mbunge huyo wa zamani wa Mtama amekalia kuti kavu ndani ya chama chake na haitakuwa rahisi kuachwa bila kupewa adhabu ya namna yoyote ile.
Watu wa karibu na Membe walithibitisha kuwa majibu aliyoyatoa kwa Katibu Mkuu wake kupitia ukurasa wake wa twitter ni yake na ni kweli atatii agizo hilo kwa kutaka aliyetoa tuhuma hizo dhidi yake naye awepo.

MZEE MWINYI AMSIHI BASHIRU.

Wakati joto la Membe na Dk. Bashiru likiwa katika hali ya kupoa kidogo huku wafuatiliaji wa mambo ya siasa wakisubiri wawili hao kukutana, mwishoni mwa wiki iliyopita iliripotiwa kuwa Dk. Bashiru alikwenda kumjulia hali Mwenyekiti mstaafu wa pili wa CCM, Ali Hassan Mwinyi.

Safari hiyo iliibua mazungumzo mafupi yaliyogusa maeneo mbalimbali ikiwamo masuala ya chama na Serikali.
Mzee Mwinyi, aliyekuwa Rais wa awamu ya pili, akichukua kijiti cha uongozi wa chama na nchi kutoka kwa hayati Julius Nyerere, alikutana na Dk. Bashiru, nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine mazungumzo ya wawili hao, yanayoelezwa kutawaliwa na hekima na busara zaidi, yalijikita kwenye masuala ya maendeleo hasa ya chama na serikali kwa ujumla, zikiwamo pongezi.

Miongoni mwa mambo yaliyobeba sura ya kusihi pamoja na kuhusia yaliyozungumzwa na Mzee Mwinyi ni kumtaka Dk. Bashiru anahakikisha chama hicho kinaendelea kuisimamia serikali.

Mbali na suala la CCM kuisimamia serikali, lakini pia Rais huyo mstaafu alitaka kuimarishwa kwa nidhamu kwa hoja kuwa;

""Elimu isiyo na nidhamu inaweza kusababisha fujo kwa watoto, watuwazima na hata kwa watumishi wa umma"".

Katika kudadavua hoja yake hiyo imeelezwa kuwa Dk. Bashiru aliambiwa nidhamu inasaidia kujenga na kuimarisha taifa imara na lenyewatu wenye kuheshimu kanuni, utaratibu na sheria za nchi.

Katika kuonesha kuwa anapaendezwa na mwenendo wa mambo ndani ya serikali ya awamu ya Tano, Mzee Mwinyi alisema kauli mbiu ya Rais ya kuchapa kazi ambayo dhamira yake ni kuwaletea watanzania maendeleo ibebe tija ni lazima sheria na kanuni zifuatwe.

Katika mazungumzo yao imebainishwa kuwa Dk. Bashiru alimshukuru Mzee Mwinyi kwa kuendelea kutoa mchango wake mkubwa katika kuimarisha Muungano na kukuza lugha ya Kiswahili.

Aidha aliweka wazi kuwa Mzee Mwinyi ni kiongozi wanchi aliyekuwa na mchango mkubwa katika serikali zote mbili na ameendelea kuwakumbusha, kuwashauri na kuwaombea Watanzania kila anapopata nafasi.

-Rai
Uoga tu.
Hapo kosa la Membe ni nini?
Kukaa kimya au tuhuma za Musiba?
Musiba ni kiongozi au ndiye "kikao" cha CCM?
Madhara ya kumfukuza Membe uanachama yatakuwa makubwa sana.
 
Hawa watu wa ccm wanakuwa na nguvu tu wanapokuwa huko huko ccm lkn wakitoka tu ndio end of the game to them. Tumeona kwa wengi.

Ile dhana ya kuwa upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm mimi sikubaliani nayo kabisa kwani naona hawa wanaotoka ccm kuja upinzani ndio wanaoudhoofisha upinzani. Siku wapinzani watakapogundua hili hawatabaki hapa walipo tena.
Kweli aisee na wasije huku wabaki huko huko.
 
VIKAO vya Kamati Kuu (CCM) na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vinatarajia kukaa wiki ijayo, huku agizo la Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Bashiru Ally la kumtaka ofisini kwake kada wachama hicho Bernard Membe, likiwa halijatekelezwa. RAI linachambua.View attachment 966775

Ingawa haijaelezwa vikao hivyo vitafanyika Dodoma ama Dar es Salaam, tayari imeshatangazwa kuwa vitafanyika kwa siku mbilimfululizo, Desemba 17 na 18 mwaka huu.
Moja ya ajenda ya vikao hivyo imeshawekwa wazi kuwani uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho kwa serikali zote mbili ya Muungano na ile ya Zanzibar.

Ikiwa imesalia miezi 12 kufikia mwaka 2020, imeelezwa kuwa chama hicho kitawasilisha ile ya mwaka 2015 hadi 2020.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanavitazama vikao hivyo kwa sura mbili, moja ikiwa ni kutathmini mwenendo wa mambo ndani na nje ya chama hicho na pili ni kushughulikia makada wao ambao wanaonekana kwenda kinyume na matakwa ya CCM mpya.

Wapo baadhi ya makada wa chama hicho ambao pia ni wabunge wamepata kunyooshewa vidole hadharani na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho.

Miongoni mwao ni Bernard Membe (Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), ambaye hivi karibuni jina lake liliingia kwenye mjadala mkali baada ya kutakiwa kufika ofisini kwa Dk. Bashiru ili akajieleze.

Membe ambaye bado hajatekeleza agizo hilo, ametakiwa akajieleze baada ya kuwapo kwa tuhuma za kuendesha mikakati ya kutaka kumkwamisha Rais Dk. John Magufuli.
Ilidadavuliwa kuwa nia ya Membe ni kutaka kuwania urais mwaka 2020 huku akijua wazi kuwa utamaduni wa chama hicho tangu kurejea kwa chaguzi za vyama vingi ni kuachiana kwa vipindi viwili.

Ingawa Membe hajawahi kusema chochote kuhusiana na siasa tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike na yeye kuishia kwenye hatua ya tano bora, ameingia kwenye tuhuma hizo kutokana na taarifa zilizowahi kuripotiwa na moja ya magazeti ya kila siku nchini.

Hatua ya Katibu Mkuu wa chama kumtaja moja kwa moja Membe hadharani, inatafsiriwa kama hatua ya kumweka katika kona, hatua inayoweza kuibua uamuzi wa kumvua uanachama, kama ilivyopata kufanyika kwa baadhi ya makada akiwamo Sophia Simba, ambaye amesharudishwa kundini.

Wachambuzi wa mambo ya siasa wanaamini kuwa vikao hivyo vya juu vya chama, havitaweza kupita salama bila kuwagusa makada wake wanaoonekana kwenda kinyume na matakwa ya chama, akiwamo Membe.

Membe anaingia kwenye tanuru hili huku kukiwa na kumbukumbu ya kunusurika kuvuliwa uanachama mwaka 2014 baada ya kutuhumiwa kuanza kampeni mapema, yeye na makada wengine watano.

Mwaka 2014 Membe alilazimika kukaa nje ya ulingo wasiasa kwa miezi 12, akiwa pamoja na aliyekuwa hasimu wake ndani ya CCM, Edward Lowassa, Januari Makamba, Frederick Sumaye, William Ngeleja na Stephen Wasira.
Adhabu yao ilikoma mwaka 2015 na kukutwa hawanahatia, hata hivyo kwa mwenendo wa sasa wa CCM mpya, upo uwezekano mkubwa wamwanasiasa huyo ambaye jina lake limerejea kwenye siasa za mitandaoni kwa kasi akakumbana na adhabu kali zaidi itakayomweka nje ya siasa za chama chake.

Hatua ya kuitwa kwake ambayo ilionesha kuwashangaza baadhi ya wakongwe wa chama hicho, inaibua fikra za moja kwa moja kuwa mbunge huyo wa zamani wa Mtama amekalia kuti kavu ndani ya chama chake na haitakuwa rahisi kuachwa bila kupewa adhabu ya namna yoyote ile.
Watu wa karibu na Membe walithibitisha kuwa majibu aliyoyatoa kwa Katibu Mkuu wake kupitia ukurasa wake wa twitter ni yake na ni kweli atatii agizo hilo kwa kutaka aliyetoa tuhuma hizo dhidi yake naye awepo.

MZEE MWINYI AMSIHI BASHIRU.

Wakati joto la Membe na Dk. Bashiru likiwa katika hali ya kupoa kidogo huku wafuatiliaji wa mambo ya siasa wakisubiri wawili hao kukutana, mwishoni mwa wiki iliyopita iliripotiwa kuwa Dk. Bashiru alikwenda kumjulia hali Mwenyekiti mstaafu wa pili wa CCM, Ali Hassan Mwinyi.

Safari hiyo iliibua mazungumzo mafupi yaliyogusa maeneo mbalimbali ikiwamo masuala ya chama na Serikali.
Mzee Mwinyi, aliyekuwa Rais wa awamu ya pili, akichukua kijiti cha uongozi wa chama na nchi kutoka kwa hayati Julius Nyerere, alikutana na Dk. Bashiru, nyumbani kwake, jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine mazungumzo ya wawili hao, yanayoelezwa kutawaliwa na hekima na busara zaidi, yalijikita kwenye masuala ya maendeleo hasa ya chama na serikali kwa ujumla, zikiwamo pongezi.

Miongoni mwa mambo yaliyobeba sura ya kusihi pamoja na kuhusia yaliyozungumzwa na Mzee Mwinyi ni kumtaka Dk. Bashiru anahakikisha chama hicho kinaendelea kuisimamia serikali.

Mbali na suala la CCM kuisimamia serikali, lakini pia Rais huyo mstaafu alitaka kuimarishwa kwa nidhamu kwa hoja kuwa;

""Elimu isiyo na nidhamu inaweza kusababisha fujo kwa watoto, watuwazima na hata kwa watumishi wa umma"".

Katika kudadavua hoja yake hiyo imeelezwa kuwa Dk. Bashiru aliambiwa nidhamu inasaidia kujenga na kuimarisha taifa imara na lenyewatu wenye kuheshimu kanuni, utaratibu na sheria za nchi.

Katika kuonesha kuwa anapaendezwa na mwenendo wa mambo ndani ya serikali ya awamu ya Tano, Mzee Mwinyi alisema kauli mbiu ya Rais ya kuchapa kazi ambayo dhamira yake ni kuwaletea watanzania maendeleo ibebe tija ni lazima sheria na kanuni zifuatwe.

Katika mazungumzo yao imebainishwa kuwa Dk. Bashiru alimshukuru Mzee Mwinyi kwa kuendelea kutoa mchango wake mkubwa katika kuimarisha Muungano na kukuza lugha ya Kiswahili.

Aidha aliweka wazi kuwa Mzee Mwinyi ni kiongozi wanchi aliyekuwa na mchango mkubwa katika serikali zote mbili na ameendelea kuwakumbusha, kuwashauri na kuwaombea Watanzania kila anapopata nafasi.

-Rai
Nimeongea sana nasubiri jumba libomoke na watu wagawane mpaka misumari maana magufuri fikra yake anadhani wale anaokaa nao kwenye vikao ni wenzie
 
Hivi ? Ni lini Membe alitamka atagombea ? Mnamuogopa wakati hajasema kitu. Akisema je ? Hebu Bashiru ajifanye kama anajikuna aone mambo ya Membe. Ajifanye tu kama anajikuna
Hahah.. Unataka atamke wazi?
 
Sijui ni ripoti gani ya kutekeleza ilani itakayowasilishwa juu ya vipengele vya ilani vinavyotaka mambo haya yatekelezwe
1. Wasichana wajawazito waendelee na masomo
2. Kupatikana kwa katiba mpya
3. Kuendeleza Dira ya Big Results Now!

Naona Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeikana ilani yake yenyewe katika mambo hayo!
Unapokosa mpangilio wa mambo mara nyingi humplekea mtu kujikwaa mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom