Meli za machinga zasababisha kupungua meli bandarini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,992
Kuna meli za machinga ambazo huzurura baharini na mizigo ya bei poa iwe mafuta,simenti,sukari,nguo nk wakitafuta mnunuzi na bandari ya kuipakua (Mingine ikiwa ya wizi wamekwapua nchi za watu).

Mizigo hiyo mingine huwa hata haina documents na meli zenyewe huwa ni zile ambazo zingine hata usajili hazina lakini kutokana na ukubwa wa bahari huzurura baharini wakitafuta wateja wakipata huhonga huingia bandarini kinyemela hushusha mizigo na kutimua mbio.

Bandari zinazoendekeza sana rushwa hizi meli za machinga hupenda sana hizo bandari.Hivyo husaka mizigo ya magendo popote duniani kuipakia na kuileta kuiuza kwenye hiyo bandari ya wala rushwa.

Serikali ya Tanzania baada ya kubana barabara bandarini meli za machinga zimeyeyuka haziji.Na wafanyabiashara waliozoea kununua mali za magendo kutoka hizo meli kwa bei poa wameanza kufilisika kwa kuwa hawakuwa wafanyabiashara wa halali.

Sasa hivi meli zinazokuja ni zile tu za kihalali zilizosajiliwa kihalali na mizigo ya kihalali iliyo tayari kulipiwa kodi zote.

Kwangu naona ni sawa ni heri kupata meli tatu kwa mwezi zinazolipa kodi stahiki meli zenyewe na mizigo yenyewe kuliko kuwa na meli elfu moja ambazo zinajaa bandarini hazilipi chochote na mizigo wanayoshusha hailipiwi kodi kontaina zinayeyuka kimya kimya.
 
Mkuu YEHODAYA Ondosha hilo neno machinga

ha ha ha.Lugha ya kiswahili inakua kwa kasi.Machinga ni neno la kiswahili linalomaanisha mtu yeyote anayetembeza biashara mitaani.Iwe mitaa ya ndani ya nchi au nje ya nchi.Muda si mrefu utaliona kwenye kamusi ya kiswahili.Halina maana ya mtu wa eneo fulani!!!!
 
Daah hili swala limemgusa kaka yangu....alikuwa ananunua magar na vifaa vya ujenz kwa bei poa sana .....
 
Hujaona simba aliyechoka wewe........na pia hujaona jemani shefadi aliyeshiba..........
Wote nimewaona lkn wataendelea kuretain identity zao...we ulishakuta simba anaitwa mbwa...kila siku yanga anamfunga simba...lakini bado wanajikakamua kuendelea kuitwa simba
 
Back
Top Bottom