Meli za kivita za Urusi 'kukwepa' Uhispania

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,880
Manowari za Urusi, ambazo zilikuwa zimetarajiwa kusimama Uhispania kuongeza hazina ya mafuta, hazitasimama nchini humo tena kutokana na wasiwasi wa mataifa wanachama wa Nato.

Urusi inaripotiwa kuondoa ombi lake la kutaka meli hizo za kivita zitie nanga katika bandari ya Cueta.

Wizara ya mambo ya nje ya Uhispania amekiri kwamba meli hizo hazitasimama katika pwani yake.

Uhispania imekuwa ikishinikizwa na mataifa wanachama wa shirka la kujihami la nchi za Maghafibi, Nato, kutoruhusu meli hizo zinazoelekea Syria kuongezwa mafuta kwenye bandari zake.

Kundi la meli za kivita za Urusi zimekuwa zikielekea bahari ya Mediterranean kusaidia kutekeleza mashambulio dhidi ya waasi wanaopinga Rais Bashar Assad.

Urusi ilikuwa awali imepewa ruhusa ya kuingiza meli tatu bandari ya Cueta kati ya 28 Oktoba na 2 Novemba.

Chanzo :
BBC
 
Dunia inapozungukwa na Vyombo vya kiitikadi kwa malengo ya watu fulani kwa kueneza ujinga!! BBC walipaswa kutoa taarifa kwa ufafanuzi zaidi hichi kichwa cha Habari kinakusudi la kuonyesha Urusi wanafanya mambo kiujanja ujanja wakati si kweli: Taarifa za kweli ni kwamba Urusi kupitia Ubalozi wake nchini Hispania walipeleka ombi kwa serikali ya Hispania kuruhusu msafara huo kutia nanga kwaajili ya kujaza mafuta na mahitaji mengineyo katika mji wa Ceuta ambao ni mji unaokaliwa kimabavu na Uhisopani kwani mji huo upo Bara la Africa ukipakana na Morocco (Sehemu hiyo Uhispania unaimiliki na hivyo ni sehemu ya Muungano wa Ulaya). CEuta is One of the Poorest towns in Hispania. Ikumbukwe Meli za urusi zimekuwa zikitia nanga katika mji huo kwa suala la kujaza mafuta pamoja na huduma nyinginezo tokea miaka ya 2000. Baada ya Urusi kutuma maombi hayo kwa nchi ya Hispania, ndipo Viongozi wa Umoja wa Ulaya na waandamizi wa NATO wakaipelekea Onyo kali uhispania endapo itaruhusu meli hizo kutia nanga katika mji huo wa Ceuta kama Urusi ilivyoomba, malumbano hayo yalikuwa kabla ya siku ya jana. Urusi kuona nafasi ya Hispania katika malumbano baina ya wahusika wa muungano wa Ulaya..Jana Balozi wa Urusi akaiandikia Barua serikali ya Hispania kuwaeleza mabadiriko ya Msafara wa meli hizo za Urusi na hivyo hazitatia nanga tena Ceuta na kuondoa ombi waliloipelekea serikali ya Hispania la kutaka kutia nanga katika mji huo. Hoja ya Umoja wa Ulaya kuishinikiza Hispania isitoe ruhusa kwa Meli za Urusi kutia nanga katika mji huo ni kwamba Meli hizo zinakwenda kufanya mashambulizi nchini Syria kwa lengo la Kuwashambulia raia wasio na hatia. Source: the guardian, TAS, Telegraph, RT...
 
Nnafikiri hili suala la Urusi Vs. US/NATO members (ulaya) lipewe jukwaa maalum hapa JF.
 
Trump alisema akichaguliwa kuwa rais wa USA atakaa meza moja na Putin kuzungumzia mgogoro wa syria,lakini HCrinton alin'gaka sana huku @weakliks wakiweka hadharani email za HC kuhusu vita ya libya!!wanaompinga Al-Hasad ni mamluki wa marekani hivyo mrusi lazima alinde maslahi yake huko syria,haitakua rahisi kama ilivyokua libya
 
hivi hao ISIS ndo wengi kiasi hicho inaonekana kama Mrusi anapigana na mataifa flani pale Syria apart of ISIS.

Zaidi ya Mafuta pale Syria nini kingine muhimu sana Mrusi anabenefit maana naona kama hii vita imekua over extendend

Au ndo hilo soko la silaha?

Wenyekujua zaidi kuhusu hii vita watujuze?

na hakuna agreement yaweza patikana zaidi ya vita?
 
Dunia inapozungukwa na Vyombo vya kiitikadi kwa malengo ya watu fulani kwa kueneza ujinga!! BBC walipaswa kutoa taarifa kwa ufafanuzi zaidi hichi kichwa cha Habari kinakusudi la kuonyesha Urusi wanafanya mambo kiujanja ujanja wakati si kweli: Taarifa za kweli ni kwamba Urusi kupitia Ubalozi wake nchini Hispania walipeleka ombi kwa serikali ya Hispania kuruhusu msafara huo kutia nanga kwaajili ya kujaza mafuta na mahitaji mengineyo katika mji wa Ceuta ambao ni mji unaokaliwa kimabavu na Uhisopani kwani mji huo upo Bara la Africa ukipakana na Morocco (Sehemu hiyo Uhispania unaimiliki na hivyo ni sehemu ya Muungano wa Ulaya). CEuta is One of the Poorest towns in Hispania. Ikumbukwe Meli za urusi zimekuwa zikitia nanga katika mji huo kwa suala la kujaza mafuta pamoja na huduma nyinginezo tokea miaka ya 2000. Baada ya Urusi kutuma maombi hayo kwa nchi ya Hispania, ndipo Viongozi wa Umoja wa Ulaya na waandamizi wa NATO wakaipelekea Onyo kali uhispania endapo itaruhusu meli hizo kutia nanga katika mji huo wa Ceuta kama Urusi ilivyoomba, malumbano hayo yalikuwa kabla ya siku ya jana. Urusi kuona nafasi ya Hispania katika malumbano baina ya wahusika wa muungano wa Ulaya..Jana Balozi wa Urusi akaiandikia Barua serikali ya Hispania kuwaeleza mabadiriko ya Msafara wa meli hizo za Urusi na hivyo hazitatia nanga tena Ceuta na kuondoa ombi waliloipelekea serikali ya Hispania la kutaka kutia nanga katika mji huo. Hoja ya Umoja wa Ulaya kuishinikiza Hispania isitoe ruhusa kwa Meli za Urusi kutia nanga katika mji huo ni kwamba Meli hizo zinakwenda kufanya mashambulizi nchini Syria kwa lengo la Kuwashambulia raia wasio na hatia. Source: the guardian, TAS, Telegraph, RT...
Kama marekani mwanaume kweli hazizuie basi hizo meli
 
Putin ana siasa za kitoto, huwezi kuelewa ninachosema

Nchi kubwa kama russia haitakiwi kufanya anayofanya sasa

Nakupa mfano mdogo tu, fatilia meli ya kivita ya usa iliposhambuliwa na iran, usa alisovu vip tatizo lake ufananishe na hao russia

Urusi anafanya propaganda za kitoto tu

Juzi apa meli yake ya kivita imepita kwenye maji ya uingereza bila sababu yeyote

Labda km unafatilia nusu nusu

Unaonekana mtupu sana siasa za kimataifa Mkuu,mbona nakuheshimu.Hakuna siasa za kitoto huko ni MASLAHI YA NCHI TU,HATA TANZANIA INGEKUWA POWERFUL INGEWEZA KUFANYA HAYO.Maslahi ya Urusi yanawekwa rehani Syria afu unataka Urusi akae Moscow anakunywa Vodka.
 
Victor wa happy mrusi hajapitisha meli pale kiuchokozi,ndio njia yake hiyo hamna njia yeyote kutoka kule juu kupita ili ufike syria,au unataka tukuwekee ramani?,
walichofanya wa magharibi ni kulikuza jambo makusudi ili ionekane mrusi kafanya uchokozi.

Lengo la marekani na wenzake ni kuprolong vita wakati russia anajaribu kuimaliza
 
Putin ana siasa za kitoto, huwezi kuelewa ninachosema

Nchi kubwa kama russia haitakiwi kufanya anayofanya sasa

Nakupa mfano mdogo tu, fatilia meli ya kivita ya usa iliposhambuliwa na iran, usa alisovu vip tatizo lake ufananishe na hao russia

Urusi anafanya propaganda za kitoto tu

Juzi apa meli yake ya kivita imepita kwenye maji ya uingereza bila sababu yeyote

Labda km unafatilia nusu nusu
Naona unaandika kitoto Kwa Kuwa hujui...na hutajua unachoandika.
 
Back
Top Bottom