Meli ya thamani inateketea, wanamsaliti Nyerere

Oct 27, 2017
92
94
Umasikini ukizidi hazaa waasi wenye uzalendo~ alisema babu yule. Hakika meli ikipoteza dira mwisho wake sio mwema labda iokolewe na wasamalia wema na vipi Kama wasamalia huonekana ni waasi.

Taifa langu Tanzania~ Namkumbuka Zitto Kabwe akiwa BBC aliwahi sema ni vyema wanafunzi wajawazito wapewe nafasi ya kusoma Tena, aliekuwa raisi wakati huo alilipinga Hilo na spika wa bunge wakati huo alimuita Zitto Ni msaliti na amefanya uhaini. Hakika Zitto alionekana mbaya leo Spika huyo huyo na waziri wa juu anaunga swala Hilo nini tunajifunza hapo?

Gesi inachimbwa mtwara inasafirishwa mpaka Dar es salaam hatujaweza kuitumia kwenye mitungi kwasababu ni nyepesi mno na grade ya juu swali ni kwamba ni kweli natuwezi kuja na mfumo wa kuweza tumia gesi ile kwenye mitungi au mpaka mataifa ya nje yakaichakate huko nje wake watuuzie Tena. Kitaalamu gesi naijua na designing naifahamu nadhani hatujawekeza vya kutosha kulitatua hili na huenda hata ambao wana nafasi ya kufanya hili hawataki sumbua vichwa vyao kwani mshahara unaingia.

Mbeya Kuna madini ya niobium ambayo hutumika katika utengenezaji wa rocket, jet engine na Mambo mengine, mpaka Sasa nahakika kampuni iliyoshika kufanya kazi ile Ni ya muingereza na si Tanzania. Swali ni kwamba watalamu tulionao Tanzania wa madini Ni mwengi, kwanini Taifa hili lisiwatumie lichimbe lenyewe liuze kwa mataifa mengine?
Hakika Nyerere aliesema wazawa wasome wakomboe Taifa mnamsaliti halafu tunasherehekea uhuru, uhuru wanini?

Tunapanga kusomesha wenye Mimba ilihali Kuna sehemu Hakuna shule za msingi kwa watoto, tunadakia hili tunarukia lile. Taifa halina dira.

Kuna haja ya watu wenye uchungu na nchi hii kuangalia namna ya kufanya japo huenda ukaitwa Mhaini.
Kiwanda Cha general Tyre kiko wapi?

Kwenye dhahabu tunapigwa, gesi tunapigwa, niobium tutapigwa, mikopo ya riba tunapokea na tunatumia hovyo tutafika.

Nawambia mtaani kuna njaa Kali ikizidi Kuna kundi la Simba litatafuna kondoo wanaoongoza.

Naomba viongozi wawe na uchungu na nchi hii na ipo haja ya kuwa na mpango wa Taifa wa miaka kumi au kumi na mitano sio Kila mwaka mnapanga bajeti na Kila kiongozi anakuja na dira yake. Meli ya thamani Hakika inazama.

Siku moja njaa itazaa chuki na chuki itazaa waasi. Tuipende Tanzania.

Pumzika Mwl. Nyerere
 
Haya ndio mawazo ya kizalendo, na sio mtu kujiita mzalendo kisa kapewa V8 ya umma. Kulitakiwa kujengwe viwanda ili vitoe ajira kwa vijana, na sio serikalini kujaa magari ya bei kubwa huku wananchi wanateseka kwa kukosa ajira.
 
Poole sana ndugu. Wenye uelewa wa mambo, wataalam, wa namna mambo yanavyopaswa kwenda, huumia zaidi pindi wanapoona hayaendi ndivyo visivyo. Kwenye eneo la matumizi ya Vito vyetu pamoja na gesi nadhani kama nchi ilipaswa kujenga uwezo wake wa ndani wa namna ya kutumia vitu hivi. Vinginevyo ni unufaishaji wa nchi za magharibi tu badala ya wazawa!
 
Poole sana ndugu. Wenye uelewa wa mambo, wataalam, wa namna mambo yanavyopaswa kwenda, huumia zaidi pindi wanapoona hayaendi ndivyo visivyo. Kwenye eneo la matumizi ya Vito vyetu pamoja na gesi nadhani kama nchi ilipaswa kujenga uwezo wake wa ndani wa namna ya kutumia vitu hivi. Vinginevyo ni unufaishaji wa nchi za magharibi tu badala ya wazawa!
Mkuu kwenye nchi za dunia ya 3 specifically africa mambo yanafanyika kwa sababu kuna kundi dogo la watu wananufaika..hakuna kitu inaitwa wazawa kwenye vichwa vya hilo kundi dogo.
 
Tafuta chakula cha wanao achana na hizi alinacha. Huijui biashara ya dunia
 
Poole sana ndugu. Wenye uelewa wa mambo, wataalam, wa namna mambo yanavyopaswa kwenda, huumia zaidi pindi wanapoona hayaendi ndivyo visivyo. Kwenye eneo la matumizi ya Vito vyetu pamoja na gesi nadhani kama nchi ilipaswa kujenga uwezo wake wa ndani wa namna ya kutumia vitu hivi. Vinginevyo ni unufaishaji wa nchi za magharibi tu badala ya wazawa!
Unajengaje uwezo wa ndani bila Mwekezaji mzungu? Kwani kabla ya mzungu kuja na vyombo vyake ulijua kuwa kuna gesi Mtwara?

Kabla ya Williamson kununua almasi pale mwadui, kuna mtu alikuwa anajuwa kuwa Ina thamani? Mbona wasukuma walikuwa wanachezea nao la kete?

Tuwe wakweli, mzungu ndiye mwenye teknoloji na ndiye mwenye soko. Mzungu ndiye mwenye elimu na ndiye anatufundisha. Hamna kitu kitakuwa na thamani asiposema yeye.

Akiamua kuwa takataka za dampo ni thamani, bado utajicheka tena kuwa kwa nini mpaka mzungu.
 
Mkuu umesema ukweli na wengine sasa hivi tukisema tunaambiwa sukuma gang lakini nchi hii imejaa wanafiki wengi sana hata sijui hawaoni hata aibu kinacho niuma wengine ni watoto wa kiume ndo maana mashoga wanaongezeka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom