Meli ya Tanzania yangundulika kusambaza Silaha nchini Libya. Je, Nasi tutawekewa Vikwazo na Mabeberu?

Ulichojibu hapo unaonesha una upungufu wa akili ubongoni mwako... Only mjinga na mpumbavu ndio atakuelewa...
Sasa nikupe mifano Miwili tu ninayowapa wapumbavu like you.
1. Mtu aseme hali nyama ya Nguruwe sababu ni Haram lakini ikipikwa na Mchuzi anaunywa huyo ana akili kama wewe.
2. Gari aina ya Toyota Land Cruiser likitoka Japani ukalinunua wewe na likaandikishwa Jina lako na ukapata kibali cha nchi husika and then Ukaenda fanyia Magendo likakamtwa na walinda Sheria utaruka kuwa sio lako ni la Toyota Japan? Maisha ya sasa Mjinga ataendelea kuwa Mjinga tu.
 

Kama meli hiyo ni ya Serikali, hapo tunatakiwa kutoa ufafanuzi wenye maarifa, lakini kama ni meli binafsi, suala zima linabaki kuwa ni wamiliki wa meli hizo na mamlaka sawa na waliokuwa wameenda kujiunga na makundi ya kigaidi vile wanashughulikiwa katika ngazi binafsi.

Kwa taifa, kuna sababu ya kuregulate vizuri hizi meli binafsi ili kuhakikisha hawachafui jina la nchi kupitia ushiriki katika masuala ya uvunjaji wa sheria za kimataifa. Unaweza kuelewa nini kipo kati ya serikali ya uturuki, libya na wamiliki wa meli wa hapa.

Lakini pia kuna uwezekano wa bendera yetu kutumika katika vyombo vya biashara haramu ili kupoteza dira na focus kwa mamlaka sahihi. Kwamba washughulike na Tanzania kwa kuwa Bendera imeonekana, na kuwaacha wahushika halisi bila kushukiwa. Hili ni suala la wizara yetu ya mambo ya nje kufuatilia ili kubaini uhalisia wa hili jambo. Ni hatari kuacha tuchafuliwe bila taarifa wala utetezi kama ilivyo kuwaacha watu wetu watupake matope kwa kufanya umafia.
 
Mlaleo achana na huyo mtu. Hajui kitu na hajui kwamba hajui.
 
siyo mara ya kwanza meli hizi kuleta aibu kwa nchi huwa zinapata tu usajili hapa ila huwa ni za waarabu naskia zanzibar ndipo kuna loop hole za kusajili meli za aina hii, ni aibu na hatari kwa nchi yetu
Mkuu,kwani unafikiri nini kifanyike katika swala hili?
 

Jamii Forum ni kama kijiwe cha kahawa. Kila mtu ana uhuru wa kuongea.

Lakini, binadamu tumeumbwa na aibu. Huoni aibu wewe? Labda ukacheze taarabu ambako kila mtu hata juha ni mjuaji. Jamkani, naogopa kwamba JF kumbe unaweza kuwa unapoteza muda ukadhani hueleweki kumbe unaongea na ............

Nenda kasubiri ngoma .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…