Inasemekana kampuni inayomiliki meli hiyo imekuwa na uhusiano wa kitalii na Haiti kwa miaka mingi na uamuzi huo ulifanywa na kampuni. Nadhani ilikuwa stop-over iliyokuwa kwenye schedule kabla ya tetemeko. Hivi serikali ya Haiti imeishia wapi, tumeshamuona Raisi (siku ya kwanza tu), lakini mawaziri, meya wa Port-au-Prince na viongozi wengine wameishia wapi? Nadhani wangesaidia kusimamia mambo kama haya.