Meli tano zapigwa marufuku Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meli tano zapigwa marufuku Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by mdau wetu, Sep 27, 2011.

 1. m

  mdau wetu JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 548
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MAMLAKA ya vyombo vya baharini Zanzibar, zimesimamisha huduma za meli tano kutokana na meli hizo kutokidhi viwango vinavyotakiwa kusafirisha abiria na mizigo.

  Meli zilizositishwa safari ni Mv Serengeti, Nura, Buraq One, Buraq Two pamoja na Mubarak kutokana na usajili wa meli hizo ulikuwa ni kusaidia kuvuta meli baharini (tagi) na siyo kubeba abiria.

  Akitoa taarifa hizo kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi wa Mamlaka wa Vyombo vya Bahari Zanzibar, Haji Vuai Ussi alisema kukatishwa kwa safari kwa vyombo hivyo kumetokana na kukosa usalama wa uhakika kwa abiria wake.

  Aidha, alisema ingawa meli hizo zilianza kazi za kuchukua abiria kwa muda mrefu, lakini zilishindwa kujisajili kwa kazi hiyo, jambo ambalo limekuwa likienda kinyume cha taratibu za vyombo vya bahari.

  Vuai alisema meli hizo pia zilikuwa zikihudumiwa na wafanyakazi wasiokuwa na sifa wala taaluma ya ubaharia pamoja na kushindwa kutoa taarifa za usalama kwa wasafiri wakati wanapokuwa safarini.

  Alisema Mamlaka imebaini tatizo kubwa katika meli hizo baada ya kufanya ukaguzi na kugundua kuwa meli zote hizo zimekosa mfumo mzuri wa mawasiliano pale linapotokea tatizo la kiufundi.

  Akizungumzia kuhusu usalama wa vyombo vya baharini kwa ujumla, alisema mamlaka imegundua pia matatizo lukuki kwa manahodha wa meli hizo kwa kuondoa meli bila kujua taarifa za usalama wa abiria wao.

  Mkurugenzi huyo alisema mamlaka yake imejipanga upya kuhakikisha kuwa wanachukua hatua za kisheria kwa nahodha ye yote ambaye atabainika kuondoa meli bila ya kuwa na taarifa sahihi za abiria.

  Hivyo amewataka wamiliki wa vyombo vya baharini kutoa ushirikiano kwa mamlaka.
   
 2. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,704
  Likes Received: 2,384
  Trophy Points: 280
  Nashindwa kumuelewa huyu mkurugenzi wa mamlaka husika, anazisimamisha mpaka zipate kibali au ni hatua moja kuelekea kuwashtaki kwa kukiuka sheria ya usafirishaji? Nini maana yake anapotoa taarifa kuwa sheria imevunjwa kwa muda mrefu na wao walikuwa wapi?Na wenye meli hizo waendapo ku renew registration zao lazima meli ikaguliwe na mamlaka hii ndiyoinayo husika hapa wanatumbia nini? wadau naomba nisaidiwe kuelewa hapa!
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  CCM bwana.....
   
 4. j

  junior05 Senior Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nchi hii kwa vituko,yani mbwembwe nyingi badala ya kujibu hoja ya uwajibikaji wa ajali iliyotokea,unataka tuamini unafanya saana kazi ah wapi!
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wanakumbuka shuka kushakucha! asara...
   
 6. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Natumai Haji Vuai Ussi hajaanza pilikapilika za kutafuta "Plot" na kuanza ku-browse latest model ya Toyota Landcruiser.

  .....kufa kufaana ndio taratibu zetu za maisha.
   
Loading...