Baazigar
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 1,129
- 1,100
Kama mkristo, hapa ndio hua naumiza kichwa. Watu kadhaa wenye elimu ya dini wameshindwa kunipa jibu sahihi nikaridhika..!Unachanganya mambo unaposema kuwa KRISTO NDIYE MUNGU
Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu
Yesu alimwabudu Mungu na wala Mungu hakumwabudu Yesu [" Akaenda kwenye bustani ya Gethsemane kuomba, Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, siyo kama mimi nitakavyo bali wewe Utakavyo.."]
Yesu hajui muda wala Saa ya Siku ya Mwisho, Bali Mungu anajua[ Yesu alisema " Hakuna aijuaye saa wa la siku ile si malaika wala mwana bali BABA peke yake"]
Yesu alichosikia kwa Mungu ndicho alichofundisha na wala mafundisho yake hayakuwa kwa utashi wake [Yesu alisema "Nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo na hukumu yangu ni ya haki...."]
Wote wanaomkubali Yesu, ni Mungu ndiye aliyemjaalia wampokee na wamkubali wala si kwa uwezo wake binafsi watu hao kupokea mafundisho yake [Yesu alisema "Baba ulionipa sikumpoteza hata mmoja"]
Yesu anatambua kuwa BABA ndiye Mungu wa pekee [Yesu alisema "Na uzima wa Milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa KWELI na wa PEKEE na Yesu Kristo uliyemtuma"]
Yesu anakiri BABA ni mkuu kuliko yeye [Yesu alisema "BABA yangu ni Mkuu kuliko Mimi"]
Mungu wa Yesu ndiye Mungu wetu, Na Mungu huyo Yesu alipenda kumuita BABA (Yesu alisema "Ninakwenda kwa Baba Yangu naye ni Baba Yenu, MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU")
Utukufu wa Yesu ni BABA ndiye aliyempa wala Yesu hakujipa Mwenyewe [Yesu alisema "Baba Ningependa hawa ulionipa wawe nami nitakapokuwa, wauone utukufu wangu, Utukufu ULIONIPA kabla ya kuumbwa kwa dunia"]
Sasa wewe unaleta habari za Yesu kuwa Mungu wakati maandiko all the time yanakuonyesha kuwa kuna ALIYE JUU YA YESU KIMAMLAKA!
Au unataka kutwambia BABA ni Mungu Mkubwa mkubwa na YESU ni Mungu Mdogomdogo?
Kwa mujibu wa maandiko huwezi kumuequate FATHER (JEHOVAH) na SON (JESUS) yaani utakwama, maandiko hususan Kauli za Yesu mwenyewe zitakukatalia.
Tukubali tu kuna Mungu Mmoja ambaye YESU alikuwa akimuita BABA
Na tukubali tu kuwa Yesu alitumwa na Mungu kuwafunza watu wamjue BABA ili wapate Salvation
Na tukubali tu kuwa Yesu naye ana Mungu, na Mungu mwenyewe ndiye yule alikuwa akimuita BABA
Hili tatizo la kuconnect dots ndo limeharibu sana mafundisho halisi ya Kristo: Badala ya kutwaa mafundisho ya Kristo kama alivyofundisha, watu throughout centuries wakaanza kutengeneza nadharia kuwa "ooh, Yesu ndyo Baba lakini hakujifunua tu, Wengine wanasema hapana BABA na MWANA ni Separate entities lakini wote ni sawa(CO-EQUAL), Wengine wanasema BABA na MWANA ni Walewale tu ila kila mmoja ana role tofauti
Logic/Falsafa/ Nadharia na kuconnect dots kwa baadhi ya watu kumedilute na kupoteza muelekeo halisi wa Mafunzo aliyofundisha Kristo mwenyewe na kuyapeleka so far out of context!
Kristo mwenyewe anasema MY FATHER IS GREATER THAN I (Baba yangu yu Mkuu kuliko mimi), lakini wanakuja watu centuries later wanasema FATHER na SON ni CO-EQUAL and CO-ETERNAL!. hii CO-EQUAL wameipata wapi? wamejitungia wenyewe tu ili kuconnect dots kwao kuweze kumakes sense kwa mujibu wa akili zao za kupenda falsafa!