Melchizedek na utata unaomzunguka

Unachanganya mambo unaposema kuwa KRISTO NDIYE MUNGU
Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu

Yesu alimwabudu Mungu na wala Mungu hakumwabudu Yesu [" Akaenda kwenye bustani ya Gethsemane kuomba, Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, siyo kama mimi nitakavyo bali wewe Utakavyo.."]

Yesu hajui muda wala Saa ya Siku ya Mwisho, Bali Mungu anajua[ Yesu alisema " Hakuna aijuaye saa wa la siku ile si malaika wala mwana bali BABA peke yake"]

Yesu alichosikia kwa Mungu ndicho alichofundisha na wala mafundisho yake hayakuwa kwa utashi wake [Yesu alisema "Nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo na hukumu yangu ni ya haki...."]

Wote wanaomkubali Yesu, ni Mungu ndiye aliyemjaalia wampokee na wamkubali wala si kwa uwezo wake binafsi watu hao kupokea mafundisho yake [Yesu alisema "Baba ulionipa sikumpoteza hata mmoja"]

Yesu anatambua kuwa BABA ndiye Mungu wa pekee [Yesu alisema "Na uzima wa Milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa KWELI na wa PEKEE na Yesu Kristo uliyemtuma"]

Yesu anakiri BABA ni mkuu kuliko yeye [Yesu alisema "BABA yangu ni Mkuu kuliko Mimi"]

Mungu wa Yesu ndiye Mungu wetu, Na Mungu huyo Yesu alipenda kumuita BABA (Yesu alisema "Ninakwenda kwa Baba Yangu naye ni Baba Yenu, MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU")

Utukufu wa Yesu ni BABA ndiye aliyempa wala Yesu hakujipa Mwenyewe [Yesu alisema "Baba Ningependa hawa ulionipa wawe nami nitakapokuwa, wauone utukufu wangu, Utukufu ULIONIPA kabla ya kuumbwa kwa dunia"]

Sasa wewe unaleta habari za Yesu kuwa Mungu wakati maandiko all the time yanakuonyesha kuwa kuna ALIYE JUU YA YESU KIMAMLAKA!

Au unataka kutwambia BABA ni Mungu Mkubwa mkubwa na YESU ni Mungu Mdogomdogo?

Kwa mujibu wa maandiko huwezi kumuequate FATHER (JEHOVAH) na SON (JESUS) yaani utakwama, maandiko hususan Kauli za Yesu mwenyewe zitakukatalia.

Tukubali tu kuna Mungu Mmoja ambaye YESU alikuwa akimuita BABA

Na tukubali tu kuwa Yesu alitumwa na Mungu kuwafunza watu wamjue BABA ili wapate Salvation

Na tukubali tu kuwa Yesu naye ana Mungu, na Mungu mwenyewe ndiye yule alikuwa akimuita BABA

Hili tatizo la kuconnect dots ndo limeharibu sana mafundisho halisi ya Kristo: Badala ya kutwaa mafundisho ya Kristo kama alivyofundisha, watu throughout centuries wakaanza kutengeneza nadharia kuwa "ooh, Yesu ndyo Baba lakini hakujifunua tu, Wengine wanasema hapana BABA na MWANA ni Separate entities lakini wote ni sawa(CO-EQUAL), Wengine wanasema BABA na MWANA ni Walewale tu ila kila mmoja ana role tofauti

Logic/Falsafa/ Nadharia na kuconnect dots kwa baadhi ya watu kumedilute na kupoteza muelekeo halisi wa Mafunzo aliyofundisha Kristo mwenyewe na kuyapeleka so far out of context!

Kristo mwenyewe anasema MY FATHER IS GREATER THAN I (Baba yangu yu Mkuu kuliko mimi), lakini wanakuja watu centuries later wanasema FATHER na SON ni CO-EQUAL and CO-ETERNAL!. hii CO-EQUAL wameipata wapi? wamejitungia wenyewe tu ili kuconnect dots kwao kuweze kumakes sense kwa mujibu wa akili zao za kupenda falsafa!
Kama mkristo, hapa ndio hua naumiza kichwa. Watu kadhaa wenye elimu ya dini wameshindwa kunipa jibu sahihi nikaridhika..!
 
Kama mkristo, hapa ndio hua naumiza kichwa. Watu kadhaa wenye elimu ya dini wameshindwa kunipa jibu sahihi nikaridhika..!

Huna sababu ya kuogopa ndugu Baazigar, wapo wakiristo mamilioni duniani wasiomchukulia Yesu kuwa ni Mungu, Hawa ndiyo wapo kwenye haki, hawa ndiyo wapo kwenye ukweli katika suala hili, Hawa wanaitwa UNITARIAN CHURCH (Yaani Kanisa la Upekee wa Mungu), mfano mmojawapo wa waliowahi kuwa waumini wa Kanisa hili ni Sir Isaack Newton (Genius wa Physics), Hawa wamebase Theolojia yao kwenye Mafunzo ya Yesu mwenyewe na kauli za Yesu mwenyewe siyo kauli za Wanafalsafa wa kidini waliokuja baadae na kujifanya wanaconnect dots kumbe ndo kwanza wanakwenda mbali na kauli halisi za Yesu mwenyewe!

Nakushauri bwana Baazigar, mpe BABA haki yake maana yeye ndiye YEHOVA, hakuna kama Yeye, Yeye anatuma wala hatumwi. Yeye ndiye Mungu wa Kweli na wa Pekee

Na YESU mwana wa Maria mpe haki yake anayostahili maana yeye ni MWANA WA MTU , ni KRISTO wa nyumba ya Daudi, Ni NABII lakini siyo Mungu. Maana kama Hajui muda wala saa ya siku ya mwisho basi huyo siyo Mungu bali ni mtu
 
Kama nilivyojaribu kuelezea Mara moja pale juu.
Kwamba Yesu Kristo yupo mara moja na yote ni sahihi kwani si vema kulazimisha Dhana moja.

Kwanza Kuna Binadamu Yesu Kristo, Mtoto wa Yusufu, mtoto wa Yakobo Mtoto wa Matani, Mtoto wa Eleazari, mtoto wa Eliudi, Mtoto wa Akimu, mtoto wa Sadoki, Mtoto wa Azori hao ni vizazi vya Ibrahimu.
Yesu hiyo ni Mwisraeli na alijishighulisha na kazi za Fundi seremala na kuhubiri Imani ya watu wake,na mwishowe akafa ana akazikwa Kama Binadamu wengine.

Pili Yupo Yesu Kristo Masihi Mwana wa Mungu.
Huyo Hana Mwanzo Wala Mwisho, na alijiita kuwa ni Alfa na Omega.
Maandiko yote ya Imani Yana mtaja kuwa huyo Yesu yupo hazaliwi wala hafi.
Yanasema kuna kipindi alikuja duniani alihubiri Imani kwa watu wake na hatimaye alirudi Mbinguni kwa kupaa angani.
Alipokuwa dunia aliweza kufufua wafu, na kusamehe watu dhambi, mambo ambayo hayajawahi wala hayatawahi kufanywa na Binadamu.
Maandiko yanasema atarudi tena duniani kuja kuutawala ulimwengu.

Nabii Isaya anajaribu kumwelezea kidogo kwa kusema.
Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume,
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake, Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa amani.

Sasa hapa naona wengine wanajaribu kumwelezea Yesu wa kwanza kwa usahihi kabisa na wengine wanamweleza Yesu wa pili kwa ufasaha kabisa.
Na wengine wanamweleza Yesu kwa kutomjua Yesu katika dhana zote mbili.
 
Huna sababu ya kuogopa ndugu Baazigar, wapo wakiristo mamilioni duniani wasiomchukulia Yesu kuwa ni Mungu, Hawa ndiyo wapo kwenye haki, hawa ndiyo wapo kwenye ukweli katika suala hili, Hawa wanaitwa UNITARIAN CHURCH (Yaani Kanisa la Upekee wa Mungu), mfano mmojawapo wa waliowahi kuwa waumini wa Kanisa hili ni Sir Isaack Newton (Genius wa Physics), Hawa wamebase Theolojia yao kwenye Mafunzo ya Yesu mwenyewe na kauli za Yesu mwenyewe siyo kauli za Wanafalsafa wa kidini waliokuja baadae na kujifanya wanaconnect dots kumbe ndo kwanza wanakwenda mbali na kauli halisi za Yesu mwenyewe!

Nakushauri bwana Baazigar, mpe BABA haki yake maana yeye ndiye YEHOVA, hakuna kama Yeye, Yeye anatuma wala hatumwi. Yeye ndiye Mungu wa Kweli na wa Pekee

Na YESU mwana wa Maria mpe haki yake anayostahili maana yeye ni MWANA WA MTU , ni KRISTO wa nyumba ya Daudi, Ni NABII lakini siyo Mungu. Maana kama Hajui muda wala saa ya siku ya mwisho basi huyo siyo Mungu bali ni mtu
Hawa wanatumia bible tofauti na zilizo sambaa kitaa?.
 
Yohana : Mlango 1
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Tangu kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo Mungu anayeongelewa ni Yesu.
Tofauti ya Yesu wa Agano la kale na Yesu wa sasa ni jinsi alivyojifunua kwetu.
Biblia nyingi zina vitabu 66 na miongoni mwa hivyo hakuna kitabu cha Enoch (hivyo siwezi kucomment lolote juu ya hiyo hadithi). Melchizedek na sifa zake kwanza alikuwa "kuhani milele, hana wazazi, hana mwanzo/mwisho wa siku, n.k." mwenye sifa hizi zoote ni Mungu (Yesu) ila kwavile agano la kale Yesu alikuwa hajafunuliwa lakini katika kukamilisha agano Mungu alilolifunga na Ibrahim ili kupitia kwa Ibrahim Yesu azaliwe kutokana na vizazi vyake ilitakiwa pawepo uduma ya ukuhani na kupokea sadaka ili ambariki kuweza kukamilisha mpango wa Mungu. Bila hiyo baraka ya kikuhani ya melchizedek Ibrahimu asingefika popote mbele ya Shetani anayejua mpango mzima (Wafilipi : Mlango 4
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu). Kwahiyo huyo Melikisedeck alikuwa Yesu. Kumbuka Yesu anajifunua kama "Yehova, Mungu mwenyezi, n.k.)
Kwa ufahamu wangu naishia hapa mjadala uendelee!
umejibu vizuri sana mkuu
 
Kwamba Yesu ana relation na melkisedeki au....?
Maana hapo naona neno KWA MFANO wa melkisedeki...
Issue naona ni sifa alizopewa zinafanana na Yesu mf; Mfalme wa amani....

Otherwise ungetusaidia je Melkizedeki ni nani hasa hadi aishi milele, sijui hakua na baba wala mama.

Who was this mysterious figure?
 
Ivi kwa nini lakini hawa waandishi walitumia lugha ya mafumboo..!!??
Vichwa panzi hapa unatoka kapaaa...!!

But why?...Whyyy??
Mambo yapo Hadharani hakuna kilichofumbwa ila ukiingiza imani kuyachambua yanakuwa na utata kulingana na unachoamini.
 
Habari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.

Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni

UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.

Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH

View attachment 1176929
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.

Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki

Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??

Je huyu melchizedek ni nani hasa?

UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.

Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???

Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!

Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.

Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.

HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.

Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??

Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??

Je historia yake ni ipi??

Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?

Karibuni....
icho kitabu cha ENOCK kinapatikana wapi..kama unayoPDF Send me @johnsamwelelias@gmail.com
 
Melkizedeki hakuwa "Kuhani Mkuu" bali "Kuhani wa Mungu aliyejuu sana". Kumbuka wakati huo Mungu aliye juu sana hakuwa amefunuliwa kwa Musa na wala Ukuhani haukuwepo. Lakini tunadokezwa tu kuwa huyu Melkizedeki tayari alikuwa anamtolea sadaka El Elyon (Mwenye Enzi)


Swali zuri sana; itabidi turudi kwenye text yenyewe. Lakini kiufupi ni kuwa Ibrahim alimpa heshima kubwa Melkizedeki na ndio pointi ya baadaye kwenye Waebrania. Kuwa kama Ibrahim alitoa fungu la kumi kwa Melkizedeki ina maana kiwadhifa au hadhi Melkizedeki alikuwa juu yake.



Hili ni swali zuri. Na hapa ndio wengi wanachanganyikiwa. Je, Yesu alikuwepo kabla ya Bikira Maria; au alianza kuwepo baada ya kuzaliwa? Dokezo kidogo ni kuwa katika ile inayojulikana kama "Sala ya Kikuhani" ya Yesu kwenye Yohana 17 tunakutana na ombi hili kwa babake "Na sasa Baba, nitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu" (Yoh. 17:5). Na mistari kadhaa chini anasisitiza hili (Yoh. 17:24). Ukisoma mistari hiyo lazima ujiulize? Yesu alikuwepo kabla ya misingi ya ulimwengu? Na kama alikuwepo kuzaliwa kwake na Bikira Maria basi kuna maana gani?
Safi Sana!

Kristulojia inakujakuwa maarifa muafaka humu JF...

Inaweza kuwa mapana ya somo na visomo bora kuliko yote humu JF.

Humu nimeona mengi na nimeona wengi ambao uwezo wao kuja kufanyika 'Walawi' wa siku za leo ni mkubwa.

Tutamulika kuhusu hili la Melkizedeki, Mungu Aliye Juu Kabisa, Miungu, Malaika, Uumbaji, na Viumbe watu --mahala fulani muafaka katika uzi wa 'Kusafiri Kiwakati 101...'

Kwa kuwa haya yote ya Melkizedeki ni mfano wa mengi yaliyo ni mafundisho yalivunjikavunjika katika biblia kuhusiana na Roho, nafsi na mwili...

Haleluya!
 
Labda sijaelewa ndugu! Biblia inasema, Ebrania 7:2-3, kuwa TAFSIRI YA JINA LAKE! Siyo kwamba hakuwa na baba wala mama....ila ni TAFSIRI ya jina lake!
 
Mkuu nmekuelewa sana hoja yako nzito ila labda ningejibu hili swali.

Mwandishi kutojulikana hakudisqualify ila nlijaribu kuweka facts straight maana mkuu hapo juu anasema "mwandishi aliandika"!! Kana kwamba ana taarifa zake nyingi sana...

However, mwandishi kutojulikana kunaweza punguza credibility maana hujui alieandika alikua na nia gani?? Alitoa vyanzo vyake wapi? Hivyo kunaweza kuwepo opotoshaji ila ukimjua muandishi unaweza pima kazi zake nyingine na kuona kama alitambulika na waandishi wa kipindi hiko kama credible source

Imagine leo Historia ya Nyerere iwe imeandikwa na mwandishi ''asiyejulikana'' si tutaiamini tu ila vipi ingeandikwa na Idd Amin?? Si tungeisoma kwa umakini na tahadhari kuu.

Hivyo kwangu mimi facts ni bora kuliko mwandishi ila Credibility/Uhalali wa maandishi hutegemea na Alieandika ni NANI!
habari ndugu,

japo nimechelewa kusoma uzi huu naomba nikujibu kwa ninavoelewa. kabla sijaandika chochote naomba niwie radhi kama maelezo nitayoyaandika yalishatolea na mdau mwingine maana ndio niko page ya pili kati ya nyingi za hii page. huenda ushajibiwa.

muandishi wa waebrania ni nani na kwa nini hajulikani?

kama unavyojua waebrania/ hebrews ndio waisraeli wenyewe waliyemsulubisha Yesu. Hiyo ilikuwa clear sign kuwa hawamtaki hata kidogo na wanafunzi wake wengi walikua prosecuted. Imagine wewe ni mwebrania, je ungesign your name kwenye manuscript ambayo walengwa wanaweza kukupiga mawe mpaka ufe? exactly...

kumbuka hata kwenye bible Yesu alikuwa na wanafunzi wengi wa siri ikiwemo baadhi ya mafarisayo na kuhani kama kina nikodemo kama sijakosea. yeyote anaweza kuandika hiki kitabu.

Muandishi mwingine anayesadikika kuandika ni paul. kama unaijua historia ya huyu mwamba ni obvious asingeweza kuandika jina lake. Paulo alikuwa jasiri hakuogopa kuuawa ila wayahudi hawakumkubali hata kidogo. walimuona farisayo aliyeasi, kumbuka alijiita farisayo wa mafarisayo, myahudi wa wayahudi myahudi kweli. hii betrayal ingefanya kitabu kisiwe credible kwa wengi. Wengi walimjua kama muderer na some of them walimuexperiance kwa udhalimu mkubwa aliofanya hapo awali.

mwandishi mwingine inasemekana alikuwa ni mwanamke. kitabu kilichoandikwa na wanawake kisingebeba uzito mkubwa. Hata vile vya agano la kale kina ester havikuandikwa na wanawake ila na waandishi ambao walipenda historia za wanawake hawa zisipotee.


kuhusu kitabu chenyewe. ebwana ni kitabu kitamu sana jamaa yangu ukikisoma utaona mambo makuu sana ya Mungu yalioandikwa kwa undani kidogo kwani waliandikiwa kitabu hicho walikuwa wataalamu wa agano la kale. huandiki tu kizembe zembe ndio maana kulikuwa na references nyingi sana za matukio agano la zaman na jipya.

food for thought:

1) je wajua kuwa waebrania ndio kitabu pekee kilichoandikwa kwa ajili ya watu ambao tayari wanaijua agano la kale? vingine vyote vilikuwa ni kwa gentiles, na gentiles hawakuwa expected kuwa wamesoma torati na manabii. in other words unaweza kumuamini Yesu na kwenda mbinguni bila torati. just faith.

2) inasemekana kabla ya umri wa miaka saba watoto wakiebrania wote walikuwa wameshakariri torati yote.

3) makuhani wa agano la kale walikariri vitabu vyote vya sheria na manabii.

ahsante.
 
Mzee context ndio kila kitu.

ukisoma biblia angalia imeandikwa na nani, wakati gani na kwa nani?

Yesu ni mwana wa Mungu kweli, Mungu ni baba yake kweli kabisa. Ila context inasemaje? Je Mungu ni baba yake Yesu kama ilivyo wewe na baba yako wa duniani? Unajua wenzetu wa upande wa pili wanakwama wapi? wanachukulia mahusiano haya yakireproduction ambayo siyo kweli.

unapoambiwa Melkizedeck hakuwa na mama wala baba anamaanisha kwa jinsi ya kibinadamu. Sperm haikufertilize egg ili yeye apatikane.

unajua kwa nini wayahudi walimsulibsha Yesu? kwa sababu alijiita yeye ni mwana wa Mungu, kwa jinsi hiyo hiyo unayowaza wewe. kwao hawakuona kuwa Mungu anaweza kuwa na mtoto.
 

Similar Discussions

35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom