Melchizedek na utata unaomzunguka


Bwana Zitto Junior hebu fafanua hili la Yesu kuitwa Mzaliwa wa kwanza wa viumbe wote, hii maana yake ni nini?
(Wakolosai 1:15 )

Pili unasema Yesu ana roho wa Mungu ndani yake na unasema pia na sisi pia tuna roho wa Mungu ndani yetu, Je utofauti wa Roho wa Mungu aliyemo ndani ya Yesu na yule aliyemo ndani yetu ni nini?
 
Mkuu kabla hatujatanua mada elewa hivi.
1. Yesu anaitwa mwana wa Mungu sio sababu alizaliwa kutoka viunoni kwa mtu bali sababu ana ROHO wa Mungu ndani yake same as sisi wanadamu tukiwa na ROHO wa Mungu basi tunaitwa wana wa Mungu Johana 1:12, 1 Petro 1:23.

2. Kwa muktadha huu inaua hoja huko juu kwamba ''Yesu ana Baba kama Sisi wanadamu ila melchizedek hana Baba''.

3.Hapa tuelewane kwanza then ndio tuje why Yesu anaitwa first born

4.Kiufupi tu Yesu ndio Kivuli/copy/Kioo cha Mungu hapa duniani kupitia hilo fungu so licha ya kwamba wote tutakuwa wana wa Mungu tukimpokea ila Yesu (Ambaye alishuka duniani kama mwanadamu) anakuwa Top ya wote maana ndio kuhani wetu kutupatanisha na Mungu. Hyo ndio distinguishing factor ila kama angekuwa tu Nabii kama Nabii mwingine basi angekuwa mwana wa Mungu tu ila sio FIRST BORN..... Hii ni kwa muktadha wa hilo fungu.

5. All in all inaonyesha superiority yake dhidi ya wote waliowahi kuishi duniani
 

Sasa kama hoja ya uwana wa Mungu wa Yesu unatokana na roho aliye ndani yake kwa nini sasa aitwe GOD'S ONLY BEGOTTEN SON? (John 3:16 )

Nadhani neno Begotten unaelewa maana yake nini kwenye englishMaana yake KUMZAA)

Kwa mfano hapa tunaelezwa geneology mbali mbali kwenye biblia ya Kiingereza (Mathew 1: 6-9)kwa kutumia neno begot

David the king begot Solomon by her [a]who had been the wife of Uriah. 7 Solomon begot Rehoboam, Rehoboam begot Abijah, and Abijah begot [b]Asa. 8 Asa begot Jehoshaphat, Jehoshaphat begot Joram, and Joram begot Uzziah. 9 Uzziah begot Jotham, Jotham begot Ahaz, and Ahaz begot Hezekiah.

Sasa kama Yesu ni THE ONLY BEGOTTEN SON wewe iweje utafsiri kuwa hiyo ina maanisha kuwa ni SON SIMPLY TU KWA SABABU ANA ROHO WA MUNGU NDANI?

Hoja yako ingekuwa na nguvu kama na Sisi tungekuwa BEGOTTEN SONS WA MUNGU, hiyo tungesema kuwa uSON unaozungumziwa hapa ni huo wa Kuwa na Roho ya Mungu ndani mwetu lakini iweje YESU sasa isemwe ni THE ONLY BEGOTTEN SON?, huO uONLY huohuo maana yake nini?
 
Baba mbinguni na mama duniani,,,huyo baba wa mbinguni Alikuwa anakuja duniani kulala na huyo mama wa duniani??????

Kwa kiasi nakuonyesha ukuhani wa Yesu anza na Wakolosai 1:19~22

Zingatia maneno haya
#kufanya amani kwa damu ya msalaba

#kupatanisha
Yesu Maelezo yake yana jitosheleza sio kuhàni mkuu yesu ni mwana maana yake ana baba mbinguni pia ana mama duniani ndio maana yesu ana sema tutaketi pamoja kwa baba yangu
 
Haruni kama kuhani Mkuu wa kwanza ila aliekuwa kwenye ukuhani wa kuashiria/wa ishara alikuwa akifanya mambo ambayo hayana utofauti na yale yalio kwenye uhalisia na ndio Maana Unaweza pata picha ya Melkizedech na role yake kwenye ukuhani

Hesabu 18:8~32
 
Wewe ndio umenyoosha maelezo mkuu. Wengine wanazunguka.
 
Melkizedeki sio jina rasmi la mtu, bali ni jina la sifa aliyokuwa nayo huyo mtu. Alikuwepo kuhani aliyetajwa kwa hilo jina katika kitabu cha mwanzo, aliitwa hivyo ikimaanisha kuhani mkuu, kuhani mwaminifu, na ndio maana kwenye kitabu cha Ebrews Yesu anatajwa kuwa kuhani mkuu mfano wa Melkizedeki, utofauti ni kwamba Yesu anatajwa ka sifa za kiungu za kutokuwa na baba wala mama nk, ila bado anaitwa Melkizedeki yaani kuhani mkuu.
 
Siku ukielewa kuwa Agano la kale ni kivuli cha Agano jipya utafunguka ufahamu. Hata hivyo nakushangaa wewe kwa sababu Melkizedeki kaandikwa wazi kwenye Biblia. Unakwama wapi?
 

Hakuna mahali kwenye bible Yesu anatambulishwa kwa sifa ya uungu, hii ni theolojia ya kuunga unga tu kama hii ya kujaribu kumfananisha Yesu na Melkizedeki, lakini theolojia hiyo imebase kwenye logical inferences tu badala ya maandiko!, yaani imebase kwenye watu kuconnect dots badala ya kauli thabiti ya Yesu mwenyewe

Mathayo 24:36 Yesu mwenyewe kwa kauli yake anasema anasema, "hakuna ajuaye saa wala muda wa siku ile SI MALAIKA WALA MWANA AJUAYE ILA BABA PEKE YAKE (3“But concerning that day and hour no one knows, not even the angels of heaven, nor the Son,[a] but the Father only. ")
hili andiko peke yake linakuonyesha kuwa Yesu yuko limited in knowledge, hajui mambo yote na siri zote za ulimwengu huu, na hiyo peke yake ni ushahidi kuwa siyo Mungu
 

Hii ni mojawapo ya masomo ambayo nimeyapitia kwa undani kidogo. Sijui kama kuna nafasi ya kutosha. Lakini kwa ufupi niseme tu Mwandishi wa Waebrania, wa Zaburi na yule wa Mwanzo wote wanamzungumzia mtu yule yule; Yesu Kristu. Kumbuka Waebrania ina mstari mmoja muhimu sana Waeb. 13.8 ambayo inasema "Yesu Kristu ni yule yule, Jana, na leo, na hata milele". Na kama unakumbuka katika unabii wa Isaya kuhusu kuzaliwa kwa Yesu tunaambiwa kati ya majina yake mengi mojawapo ataitwa "Mfalme wa Amani"... Mfalme wa Amani ni Mfalme wa Salemu (Salemu ni "amani").

Hii ndio sababu Ibrahim alipokutana na Melkizedek alimpa fungu la kumi (kumbuka hii ilikuwa kabla ya zaka kuingizwa katika sheria za wayahudi). Ukitaka kuelewa hili rejea maneno ya Yesu ambayo anawaambia Wayahudi kuwa "Ibrahim baba yenu aliitamani kuiona siku yangu, aliiona na akafurahi (Yoh 8:56). Na utaona kuwa Yesu hamuiti Ibrahimu "baba yetu" bali "baba yenu"... Lakini pia alitoa dai moja sehemu nyingine (mistari miwili tu chini) ambalo nusura wayahudi wampige. Alisema katika mstari mwingine maarufu "Kweli kweli nawaambia" Yesu akasema, "kabla Ibrahim hajazaliwa mimi Niko" (Yoh 8:58).

Basi hapo kwa ufupi tu; ni sehemu ya tafiti yangu moja ndefu sana; labda siku moja ikimpendeza Mungu nitawashirikisha.
 
Ahsante Sana umeleza vizuri mno
 
Natamani ungeendelea tupate uelewa zaidi,maelezo mazuri
 
Kumbe kabla ya Bikira Maria yupo mwanamke mwingine aliyewahi kumleta Yesu duniani!

Maana Melkizedeki hakuibuka from nowhere lazima kwa maisha ya hapa duniani alizaliwa, hakudondoka from the sky!

Na ukuhani zama zake ulikuwa ni kwa koo, hii inamaanisha watu waliokuwepo enzi za Melkizedeki walikuwa wanaujua ukoo wake vizuri tu!

Guys let me tell you one thing:
Tatizo lilikuwepo hapa ni baadhi ya Wakiristo kuhijack mafundisho ya Kiyahudi na kujaribu kuyaposses na kuyaangalia katika miwani ya theolojia ya Ukiristo. Hata kwa yale maandiko yasiyomhusu Yesu, wanasema yanamhusu Yesu

Ni kweli kwenye Agano la kale kuna utabiri juu ya Yesu, lakini baadhi ya zile prophecy watu wanazozitumia kumhusisha Yesu wala hazimhusu Yesu kabisa

Ni watu wanajaribu kutumia akili zao tu, kutumia logic zao tu kuungaunga vitu ambavyo wala havihusiani

Ishu ya Melkizedeki na sifa alizopewa ni figurative zaidi lakini watu wanachukulia kuwa ndivyo ilivyo literary

Kwa mfano kwa nini udhani Melkizedeki ni YESU lakini siyo FATHER?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…