Meja Jenerali Muhidini Kimario(Kamanda Mbogo) afariki dunia

Meja Jenerali Muhidini Kimario(Kamanda Mbogo) afariki dunia

Ukwaju

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
13,384
Reaction score
11,285
Kimario.jpg

CC7F0054-E0D1-42E8-86F9-73BC2F11D7F5.png

EFA37B7A-D459-424B-8C47-F82CA73DE0EE.jpeg

5CAF24A2-5CB4-4954-9502-7CAF156AAB42.jpeg


Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam, Brigedia aliyeongoza majeshi yetu kuuteka Mji wa Kampala, Mbunge wa Moshi Mjini, Mzee Muhidin Kimario amefariki Dunia huko India alikoenda kwa matibabu.

Kwa sasa alikuwa akiishi Manispaa ya Dodoma na makazi mengine yakiwa Manispaa ya Moshi.

Taratibu za mazishi naona zitazingatia Itifaki.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI
 
Ooooh masikini Mzee Muhidini Kimario, RIP
He was a kind gentleman, Tanzanians will remember you.
I knew him personnally.
 
Poleni wafiwa wote, rip generali muhidini kimario, mwenye historia yake fupi tafadhali!
 
[h=1]Meja General Muhidini Kimario[/h]Watanzania watamkumbuka kwa uzalendo wake kwa matukio machache niyakumbukayo
Wakati wa vita vya Kagera mwaka 1978 - 1979. Marehemu alitumwa na Mwalimu Nyerere akiwa kama waziri kuja kuwaaga wapiganaji waliokuwa wanaenda mstari wa mbele vitani.

Akiwa katika uwanja wa michezo wa Nyamagana walipokuwa wanaagwa wanajeshi, katika hatua isiyo ya kawaida Kimario alilia mbele ya wanajeshi na wananchi waliokuwa anawahutubia.
Huku akilia alimwagiza mkuu wa Mkoa wa Mwanza amwandikie Telex , Nyerere kuwa amejivua Uwaziri na anakwenda mstari wa mbele vitani.
Alipofika mstari wa mbele alianzisha kitu kinaitwa Operesheni chakaza, akiaanisha kila kitu kilicho mbele wanajeshi wakishambulie. Na mafanikio ya Operesheni hiyo ni siku chache Tanzania iliiteka Kampala.
Tukio la shujaa huyo la mwisho ni kipindi Wanzibar walipoteka ndege kwa silaha bandia, Kimario alimnasa kibao mtekaji mmoja na akawezesha mlango wa ndege kufunguliwa.
RIP Kamanda
 
Rest In Peace Maj. Gen. Kimario.
 
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa mamlaka ya Ustawishaji Makao makuu Dodoma,Waziri wa Mambo ya Ndani,Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam,Brigedia aliyeongoza majeshi yetu kuuteka Mji wa Kampala,Mbunge wa Moshi Mjini
Mzee Muhidin Kimario amefariki Dunia huko INDIA alikoenda kwa matibabu.

Kwa sasa alikuwa akiishi Manispaa ya Dodoma na makazi mengine yakiwa Manispaa ya Moshi.

Taratibu za mazishi naona zitazingatia Itifaki.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI

R.I.P Meja General Kimario.
 

Attachments

  • Brig-Gen-Kimario.jpg
    Brig-Gen-Kimario.jpg
    12.7 KB · Views: 3,375
  • a4.jpg
    a4.jpg
    15.7 KB · Views: 302
Back
Top Bottom