Ugweno, Mwanga
Kilimanjaro
Tanzania
View: https://m.youtube.com/watch?v=0cM3JTfPQpc
Ugweno Mwanga milimani mkoani Kilimanjaro wafungua Makumbusho maalum kuhifadhi historia. Katika Makumbusho hiyo ya kata ya Kifula Ugweno wilayani Mwanga, Tanzania hiyo kuna pia kumbukumbu ya meja jenerali Benjamin Noah Msuya.
MEJA JENERALI MSUYA NI NANI?
Mwaka 1979, Jenerali Msuya aliongoza operesheni maalum majeshi ya TPDF / JWTZ ya Tanzania kuingia nchini Uganda wakati wa vita vya Kagera.
Chini ya uongozi wake wa operesheni mojawapo ya jeshi la JWTZ kati ya nyingi vilizofanywa na jeshi la Tanzania katika Vita ya Kagera, aliudhibiti mji wa Kampala na kumuondoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo, jenerali Idi Amini Dada.
Siri ya meja jenerali Benjamin Msuya kubeba mkuki aliouchukua bila kuuweka chini baada ya kuuchukua kutoka kwa familia ya wana wa mkoa wa Kagera walioathirika na uvamizi wa nduli Iddi Amin Dada waelezewa kwa kina, na mkuki huo ulibeba ujumbe gani katika vita hiyo ya Kagera
Baada ya Idi Amini kukimbia, Meja Jenerali Msuya alitawala Uganda kwa siku tatu akisubiri kumwapisha Yusuf Lule kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Yusuf Lule hakwenda sawa katika utawala, Msuya alitakiwa kumtoa na kumwapisha Godfrey Binaisa na baadaye Paulo Muwanga ndipo Msuya aliporejea nchini.
Meja jenerali Benjamin Noah Msuya aliyezawadiwa nishani kadhaa za kijeshi, baada ya utumishi wa muda mrefu uliotukuka alistaafu utumishi wake katika jeshi kwa mujibu wa sheria mwaka 2001.
Kilimanjaro
Tanzania
HISTORIA YA SHUJAA WAUGWENO WILAYA MWANGA, ALIYEITUMIKIA TANZANIA