MEI 11, KATIKA HISTORIA TANZANIA.

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
416
439
Tukitaka uchumi Wetu ukue lazima tubadili mambo yale tuliyokuwa tukifanya kwa utaratibu ule ule kwa wakati wote, ili Uchumi ukue ni lazima pesa zitoke katika shughuli ndogo na kuwekezwa katika shughuli kubwa za uzalishaji.

Lazima Akiba tunayoiweka izalishe kuongeza mali zaidi akiba inatakiwa kuwekezwa kwenye shughuli za uzalishaji ili kukuza uchumi.

Uwekezaji ni njia muhimu sana kwako kufikia uhuru wa kifedha. Yapo maeneo mengi ambayo unaweza kuwekeza, na moja ya maeneo hayo ni kwenye HISA.

Siku zote pesa hazitunzwi bali zinazungushwa ziongezeke hakuna aliyewahi kutunza pesa na akawa tajiri siku zote pesa inazungushwa katika biashara huwezi kuishiwa, Popote utakapoiweka pesa itakatwa gharama za utunzaji.

Biashara ya Hisa ni ngeni kwa Tanzania lakini ndiyo biashara yenye Faida duniani ijapokuwa kuna changamoto zake. Mwanzoni niliitazama biashara hii kwa jicho la Tatu ni namna gani naweza kuzitunza pesa zangu mahali salama.

Kupitia kampuni ya Vodacom wameweka hisa zake sokoni kwangu Mimi hii ni hatua mahususi kupata sehemu sahihi kuhifadhi pesa zangu.

hii ni kwa mara ya kwanza kampuni hii kuweka hisa zake sokoni ni Fursa kwa wale ambao tunapenda kufanya uwekezaji katika soko la mitaji wa Hisa.

Bei iliyofikiwa kwa kila Hisa moja ni shilingi 850 tu kwa kuzingatia ushindani wa soko, Gharama hii ni Initial Public Offer (Vodacom IPO) kwa hisa zinazokwenda kuuzwa sokoni.
kampuni inaweza kuongeza mtaji kupitia existing shareholder au kuuza nyongeza ya hisa sokoni
na ndo kitu ambacho Vodacom wamekifanya..

Hisa zitakazonunuliwa zimewekewa malengo ya kutekeleza kikamilifu mipango ya kukuza na biashara na kutumia fursa zilizopo kuhakikisha wanaendelea kushika namba moja kwenye sekta ya mawasiliano.

Imebaki siku ya leo kununua hisa za awali za kampuni ya Vodacom fanya maamuzi sahihi katika namna ya kuweka Akiba ya fedha zako.

[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG]
[HASHTAG]#PowerToYou[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom