MEDUSA: Malkia wa Damu

MEDUSA: Malkia wa Damu

NYEMO CHILONGANI
MEDUSA: MALKIA WA DAMU
SEHEMU YA 03

Mzee Hussein akashtuka kitandani, akaupeleka mkono wake pembeni kwa lengo la kumgusa mke wake, akashtuka baada ya kuona amegusa mto na si kiuno cha mkewe kama ilivyokuwa siku zote.
Akaangalia vizuri kwa kuhisi labda alisogea pembeni ya kitanda kile, mke wake hakuwepo, alikuwa peke yake kitandani, akajiinua na kuangalia mlango wa chooni, ulifungwa na hamukuwa na taa iliyokuwa ikiwaka.
Hilo likamfanya kuinuka kabisa kitandani, kwa uchovu akaanza kuelekea bafuni kwa kuhisi msichana huyo alikuwa humo, alipofika, hakumuona kitu kilichoanza kumtia hofu moyoni mwake.
Haraka sana akalisogelea kabati la nguo na kulifungua, begi la msichana huyo lililokuwa humo siku zote nalo halikuwepo. Hilo likamtia shaka na kuhisi mke wake alimkimbia akiwa hotelini.
Moyo wake ukamuuma mno. Alimpenda sana Nasria, alikuwa mwanamke mzuri, aliyevutiwa naye ambaye alitaka kuwa naye maishani mwake mwote lakini jambo lililomsikitisha sana, msichana huyo hakuwemo humo ndani.
Akachukua simu yake kwa lengo la kumpigia, simu haikuwa ikipatikana, alijua aliizima kwa kuwa hakutaka kuwasiliana naye, moyo ukazidi kuchoma.
Moyo wake ukamwambia awasiliane na wazazi wa msichana huyo na kuwaambia kilichokuwa kimetokea, ilikuwa ni usiku wa saa saba lakini ilibidi afanye hivyo kwani ni lazima kuwataarifu ili wajue kilichotokea.
Akaanza kumpigia simu baba yake Nasria, ikaanza kuita, akainuka tena kitandani na kuendelea kuangalia huku na kule, Nasria aliondoka na kila kitu, akafungua tena kabati kujiridhisha.
Ni kweli hakuacha kitu.
Ila ghafla macho yake yakatua kwenye chupi ya msichana huyo. Mpango wake wa kuwapigia simu wazazi wake ukaishia hapo, akaikata na kutulia kitandani.
Akaichukua kutoka kabatini na kuishika, akaipelekea puani na kuinusa, ilikuwa ikinukia harufu ya manukato ya msichana huyo, aliiangalia vizuri, taswira yake ilikuwa ikionekana kichwani mwake, hakika alitamani kuwa na mkewe.
“Amenikimbia! Kwa sababu gani? Kwa nini hakuniambia kama hanitaki?” alijiuliza.
“Nitamkomesha...” alijisemea.
Hakutaka kumwambia mtu yeyote kuhusu tukio hilo, alijifanya kama kutokutokea kitu chochote kile, alikimbiwa, endapo angewambia wenzake hakika wangemuonea huruma lakini nyuma ya pazia wangekuwa wanamcheka tu.
Sasa mwanamke anakukimbiaje?
Una pesa!
Una majumba ya kifahari.
Una kila kitu.
Halafu umekimbiwa.
Hakika ingekuwa ni aibu ya mwaka.
Siku iliyofuata hakutaka kubaki Zanzibar, aliogopa kutembelewa na marafiki zake na kutaka kumuona mke wake, akaamua kupanda ndege na kwenda jijini Dar es Salaam ambapo hapo akapanda ndege na kurudi nchini Oman.
Ndani ya ndege alikuwa akimfikiria Nasria, alimpenda sana msichana huyo, kwa kile alichomfanyia hakika alihisi kutokustahili hata kidogo, kama kweli hakuwa akimpenda, basi angemwambia, aachane naye kwa kuwa kuoa kwake haikuwa na ulazima sana.
Kitendo cha kukimbiwa kwake kilionekana kama dharau fulani ambayo hakuwahi kuifikiria maishani mwake mwote. Kwa kipindi hicho moyo wake uligawanyika sehemu mbili, upande mmoja ulimwambia ni lazima amfanyie jambo baya Nasria na upande mwingine ulimwambia kuachana naye.
Alikaa katikati, hakujua ni upande gani alitakiwa kuongozana nao. Alifikiria kwa dakika kadhaa na uamuzi ambao aliamua kuuchukua ni kumkomesha msichana huyo mrembo.
Akaanza kuiona safari ikiwa ndefu kufika, alikuwa na moyo uliojawa na hasira mno, kwa kile alichofanyiwa alikuwa na uhakika angemwambia mtu yeyote yule angemcheka na kumuona mpumbavu kwa kuamini mwanaume mwenye pesa hakutakiwa kukimbiwa bali wewe ndiyo ulitakiwa kumkimbia mtu.
Ndege ilichukua saa nyingi angani na hatimaye ikaanza kutua kwenye uwanja wa ndege huko. Akateremka na abiria wengine na kuelekea nje ya jengo hilo, alipitia vizuizi vyote vya uangalizi na alipotoka ndani na kwenda nje, macho yake yakatua kwa marafiki zake.
Kwa jinsi walivyomuona tu, walijua kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Hussein hakuwahi kuwa kwenye hali hiyo hata mara moja, alionekana mnyonge tofauti na siku zote, alikuwa mole kupita kawaida.
Wenzake wakamuuliza, hakutaka kuwapa ukweli wa kile kilichotokea, aliwadanganya kwa kuwaambia hapakuwa na tatizo lolote lile bali alikuwa akijisikia vibaya hivyo walitakiwa kumuacha apumzike kwanza.
“Pole sana! Nilifikiri ishu ya mwanamke, manake nawajua sana wanawake wa Kiafrika, huwa wanazingua sana, na wewe mzee mwenzangu unavyopenda wanawake, nikajua washafaya yao,” alisema rafiki yake, mzee mwenzake kwa utani.
Kwa kile alichokisema japokuwa kilikuwa ni utani lakini kiliingia moyoni mwake na kukaa vilivyo. Alizungumza ukweli kabisa, kama wanawake wa Kiafrika walikuwa mizinguo, basi mmojawapo alimzingua.
Alitamani kumwambia lakini hakufanya hivyo, bado hakutaka kuchekwa, kwenye kitu kilichokuwa kikimtesa moyoni mwake kilikuwa hicho, yaani hakutaka kuthubutu kuufumbua mdomo wake na kumwambia mtu yeyote yule jambo hilo.
Gari lilichukua dakika kadhaa hatimaye likafika nyumbani kwake. Akateremka na kuelekea ndani. Bado alikuwa kwenye hali ileile na hata wafanyakazi wake walivyomwangalia, wakahisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kimetokea.
Kuangalia mandhari ya nyumba yake ilimuumiza moyoni mwake, akaanza kumkumbuka Nasria, msichana huyo alitakiwa kwenda kuishi humo, yaani kila kitu kilichokuwa humo kingekuwa mali yake.
“Ila hapana! Hivi kweli msichana akikuacha inabidi umloge? Lakini si amekosa mapenzi tu kwangu!” alijisemea.
“Kumloga ni sawa na kutaka kumlazimisha kuwa nami kitu ambacho hataki. Halafu mapenzi ni jambo la kawaida tu, si la kumlazimisha mtu hata kidogo,” alijisemea.
Hilo ndilo alilolifikiria, kumfanyia jambo baya Nasria haikuwa na maana yoyote ile, mapenzi yalikuwa ni kitu cha kawaida, kila mtu alikuwa na uhuru wa kumpenda mtu fulani na kutokumpenda fulani.
Kwake, msichana huyo hakutaka kuishi naye na ndiyo maana aliamua kuondoka, yeye kama mwanaume alitakiwa kumtafuta mwanamke mwingine na kuachana na Nasria.
Aliyafikiria hayo kwa dakika kadhaa, akajiambia kweli alitakiwa kuachana naye na kufanya mambo mengine. Usiku ulipofika, akalala, japokuwa alikuwa akimfikiria sana msichana huyo lakini muda huo alitakiwa kuachana naye, afanye biashara zake kama kawaida.
Siku iliyofuata akaondoka na kuelekea ofisini kwake, alikuwa na mambo mengi, kulikuwa na mizigo aliyokuwa akiisubiri kutoka nchini Uingereza, ilikuwa ni lazima kufanya kila liwezekanalo afike salama na kuangalia uwezekano wa kwenda kuichukua mahali ambapo kila siku huichukua.
Majira ya saa sita mchana wakati akiwa ofisini huku akipigwa na kiyoyozi, akapigiwa simu na mhasibu wake na kumpa taarifa mbaya kwamba kulikuwa na kiasi cha dola elfu hamsini kilichokuwa kimehamisha kutoka kwenye akaunti yake ya kibiashara.
Kwanza akashtuka, hakuamini alichokisikia hivyo akamuita mhasibu huyo kwenda ofisini kwake. Kwa kawaida akaunti yake ya biashara ndiyo ilikuwa ileile yake binafsi, alifanya hivyo kwa kuwa nchi nyingi za Uarabuni kipindi hicho hawakuruhusu watu kuwa na akaunti zaidi ya moja, hata kama ulikuwa na biashara, ilikuwa ni lazima utumie akaunti moja.
Baada ya dakika moja, mhasibu akafika ofisini humo, kwa jinsi alivyoonekana, naye alichanganyikiwa, alichojua ni kwamba yeye ndiye aliyesababisha upotevu wa pesa hizo hivyo alikuwa akijifikiria ni kwa namna gani angemwambia bosi wake huyo.
Akakaa kwenye kiti na kumuonyesha, Hussein akachukua na kuangalia, kweli pesa hizo zilitolewa kwa kuhamishiwa kwenye namba nyingine. Akaanza kuangalia namba hiyo.
“Ni namba ya wapi?” alimuuliza.
“Nilivyoangalia ni namba ya Tanzania, akaunti inaitwa Nasria,” alimjibu.
Alipolisikia jina hilo, akashtuka, hakuamini alichokisikia. Nasria yuleyule ambaye aliamua kumsamehe kwa kile alichokifanya kumbe alimuibia pesa zake na kutokomea zake. Yaani alilichukua penzi lake kisha kuchukua pesa zake.
Zile dharau alizohisi mara ya kwanza zilionekana kama kuzidi, kama alikuwa na lengo la kumsamehe msichana huyo, sasa hakutaka kufanya hivyo tena. Alichomwambia mhasibu aende kupumzika, suala hilo angedili nalo kwani alikuwa akilifahamu.
Sasa akabaki peke yake ofisini.
Alimchezea sharubu, hakumfanya kitu.
Alimshika makalio, napo hakumfanya kitu.
Akamtekenya, napo hakumfanya kitu.
Alipomuona hafanyi lolote, sasa akaamua kumpanda kichwani. Hakika kwake kilikuwa kitu kibaya na kilichomfanya kuhisi kama hakuwa mwanaume aliyekamilika.
Alitamani kurudi nchini Tanzania na kumtafuta msichana huyo lakini akaona kama kujisumbua tu. Kwanza baada ya kufika huko angetumia pesa nyingi mpaka kumpata. Polisi wa Kiafrika wangehitaji pesa kumpa ushirikiano, na kwenye hilo hakuwa na uhakika wa kumpata, kama alikomba dola elfu hamsini ilimaanisha aliondoka na kwenda kuanzisha maisha yake.
“Acha nifike nyumbani kwanza. Kumbe hajui kama mimi ni ukoo wa Kaifah,” alijisemea huku akiwa na hasira kooni mwake.
Alivumilia mpaka muda wa kurudi nyumbani ulipofika, akarudi na kitu cha kwanza baada ya kufika huko kilikuwa ni kutulia chumbani kwake, alitulia kwa dakika kadhaa huku akimfikiria Nasria, alitamani kumuua lakini hilo lisingekuwa suluhisho hata kidogo, alitakiwa kufanya jambo jingine tofauti na hilo.
“Nimtese! Nimtese tu kwa kufanya mambo ambayo hataki kufanya,” alijisemea.
Hilo ndilo lililokubalika kichwani mwake, hakutaka kuendelea kusubiri, akainuka na kuelekea katika chumba kingine. Hicho kilikuwa chumba cha siri, hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiruhusiwa kuingia humo zaidi yake.
Chumba hicho kilitawaliwa na mwanga mwekundu, kulikuwa na tunguli chache na mashuka mekundu. Pembeni kulikuwa na chungu, yaani kwa kifupi chumba hicho kilikuwa kinatisha si kawaida.
Akaanza kufanya uchawi wake, alivua nguo zake zote, akachukua mdoli mmoja wa kike na kuuandika Nasria Abdul na kuufunika kwa chupi ile ya Nasria aliyokwenda nayo na kunyunyizia damu juu yake. Alifanya hayo yote huku akiongea maneno ambayo kusingekuwa na mtu yeyote yule ambaye angeyaelewa.
Alikaa ndani ya chumba hicho kwa saa mbili, alitokwa na jasho japokuwa kiyoyozi kilikuwa kikipiga sana. Kazi aliyokuwa akiifanya, aliifanya kwa hasira sana kwani muda wote wa kazi hiyo alikuwa akimfikiria msichana huyo.
Alipomaliza, akaichukua chupi ile na kuiweka juu ya ubao mmoja, akachukua msumali na kuigongelea juu yake na kuiacha hapohapo huku yale matone ya damu yakiendelea kuonekana kwa ukaribu kabisa.
Baada ya kufanya hayo yote, akatoka, mwili wake ulilowanishwa na jasho lililokuwa likimto akwa wingi, akaamua kwenda bafuni na kuoga kisha kutoka na kurudi chumbani kwake.
“Huwa sibabaishwi hata kidogo,” alijisemea na kutulia kitandani mwake. Sasa akataka kuona kile ambacho kingetokea baadaye, ilikuwa ni lazima kumkomesha msichana huyo iwe fundisho, si huyo tu, bali hata kama kulikuwa na mtu alihusika kwenye kulitekeleza hilo, naye alikuwa ndani ya hilo kundi.

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Alhamisi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cha mtu huliwa na mtu ...
 
NYEMO CHILONGANI
MEDUSA: MALKIA WA DAMU
0718069269

SEHEMU YA 04.

Zuhura ambaye alikuwa ni rafiki yake Nasria alikuwa akiendelea na maisha yake huko Zanzibar, moyo wake ulikuwa na furaha tele baada ya rafiki yake kuachana na mumewe na kurudi jijini Dar es Salaam.
Alitumiwa kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya maisha yake, alimuona Nasria kuwa rafiki wa kweli kwani pesa aliyopewa iliyafanya maisha yake kuwa mepesi kwa sehemu fulani.
Alipokuwa ndani ya chumba chake alikuwa na furaha tele, alimshukuru sana Nasria na mara kwa mara alikuwa akimpigia simu kwa namba mpya aliyokuwa ameisajili kwa matumizi yake mapya kwani hakutaka hata kuwasiliana na wazazi wake.
Zuhura akawa mwanamke wa starehe, kila kitu alichokuwa akikifanya kwa pesa hizo zilikuwa ni starehe tu, alinunua mavazi ya bei kubwa, simu ya gharama na vitu vingine vya anasa, yote ni kwa sababu alikuwa na pesa nyingi ambayo hakuwa ameihangaikia hata kidogo.
Kila siku alikuwa akinunua pombe na kuwaita marafiki zake na kuanza kunywa pamoja kwake, ilikuwa ni sherehe kila siku, hakutaka kujali hata kidogo, kwake aliona ni bora kuula ujana kabla ya ujana kuanza kumla yeye.
Baada ya siku mbili, akampigia simu rafiki yake mwingine aliyeitwa kwa jina la Ashura na kumwambia alitaka amfuate nyumbani kwake kwani kulikuwa na mambo mengi alitaka kuzungumza naye.
Ashura akaenda mpaka nyumbani kwa rafiki yake na kuanza kuongea mambo mengi kuhusu mabuzi na hata maisha yao ya udangaji. Alimsimulia Ashura kila kitu kilichotokea kwa Nasria, Ashura alimuona Nasria kuwa mjinga kwani kwenye kitu alichokitamani maisha yake yote ni kuolewa na mwanaume aliyekuwa na pesa.
Alifuatwa na wanaume wengi lakini hapakuwa na muoaji, wengi waliomfuata walimuahidi kumuoa lakini mwisho wa siku baada ya kumvua nguo zake na kumuacha utupu kitandani, wakaachana naye na kuendelea na maisha yao.
Alikuwa na hamu ya ndoa, alitamani mno kuolewa, hakuipata bahati hiyo iliyokwenda kwa Nasria ambaye mbali na kuolewa, aliolewa na mwanaume mwenye pesa zake, aliyetaka kujenga maisha pamoja naye.
“Sasa kwa nini akamuacha?” aliuliza Ashura.
“Basi tu! Hakupenda kuishi na kibabu!” alijibu Zuhura.
“Lakini si alikuwa ana pesa?”
“Ndiyo! Nasria alisema yule mwanaume ana pesa mpaka anaumwa.”
“Na akamuacha?”
“Ndiyo! Akamuibia pesa na kutimka zake jijini,” alisema Zuhura.
Kila alichokuwa akikiongea na rafiki yake huyo, moyo wa Ashura ulikuwa na maumivu makali, hakuamini kama rafiki yake huyo angekuwa na maisha ya kijinga ya kukataa kuishi na mwanaume aliyekuwa na pesa kama ilivyotokea.
Waliongea mengi na ilipofika majira ya saa mbili usiku, akamwambia Zuhura alitaka kuondoka. Hilo halikuwa tatizo, akakubaliwa kuondoka lakini kitu alichotaka ni kutembea kwa miguu kwani haikuwa mbali na mahali alipokuwa akiishi.
“Jamani shoga’angu, si uchukue hata Uber,” alisema Zuhura, pesa zilikuwa zikimuwasha na muda wote alitaka kuombwa.
“Acha nitembee tu, wala usijali!”
“Basi acha nikusindikize,” alisema Zuhura, akasimama na kuanza kumsindikiza rafiki yake huyo.
Walitembea pembezoni mwa barabara huku wakipiga stori mbalimbali, Ashura alikuwa akilaumu uamuzi wa Nasria wa kumuacha mumewe na kutoroka na wakati alijua alikuwa na pesa lakini kwa Zuhura alimsifia kwa kuwa aliufuata moyo wake.
Huku wakiwa hapo, mara ghafla sauti za honi ya gari ikaanza kusikika kutoka nyuma, haraka sana wakageuka na kuangalia hilo gari lililokuwa likipiga honi. Waliziona taa tu tena likiwa linakuja kwa kasi. Hata kabla ya kufanya jambo lolote lile, gari likawagonga, mzinga ukasikika mahali hapo, Ashura akaangukia kama hatua tano kutoka pale walipokuwa lakini Zuhura aliangukia kama hatua ishirini kutoka hapo.
“Mamaaaaaaaaaaa.....” ilisikika sauti hiyo tu.
Ashura akashangaa pale alipoanguka hapakuwa mbali na walipokuwa wakitembea. Kwake ilishangaza kidogo kwani kwa jinsi gari lile lilivyokuwa limekuja kwa kasi na kuwagonga, hakika alitakiwa kutupwa mbali kabisa na hapo.
Lililomshangza halikuwa hilo tu bali hata mwilini mwake, hakuwa na maumivu yoyote yale zaidi ya yale aliyoyapata zaidi ya kuanguka chini. Hilo nalo lilimshangaza. Haikuwa kawaida kwa yeyote yule kugongwa na gari lililokuwa likija kwa kasi na mwili kutokuwa na maumivu yoyote yale.
Ukiachana na hayo yote, kitu cha tatu kilichomshangaza mno ni gari hilo. Walilisikia likiwa nyuma yao likipiga honi, kila mmoja alichanganyikiwa, wakajitahidi kulikwepa lakini walishindwa, yaani ilionyesha gari lilimshinda dereva hivyo kwenda pembeni na kuwagonga.
Sasa utata ulikuwa hapa.
Ni kweli waligongwa lakini kitu cha ajabu ni kwamba gari halikuwa likionekana. Baada ya kuhisi gari lilipotea njia na kuwagonga inamaana lingekuwa hata mbele limesimama, ama watu kuteremka na kuanza kuwajulia hali, la ajabu kabisa, kila kona halikuwepo gari hilo.
“Ama halikuwa gari?” alijiuliza.
Akaanza kusikika kelele za Zuhura aliyekuwa mbali na mahali hapo alipokuwa na kuanza kumsogelea, watu waliokuwa pembeni ambao nao walionekana kushangazwa na tukio hilo wakaanza kumfuata msichana huyo.
Walipomfikia, kila mmoja alishtuka, huyo Zuhura akawa kama mfu aliyekuwa akipiga kelele tu za mwisho. Alivunjika miguu yote, kichwa chake kilibonyea, mabega yalivunjika na alikuwa akitokwa na damu nyingi, yaani kwa kila walivyokuwa wakimwangalia mahali pale walijua tu hata dakika tatu hatochukua atakuwa amekufa.
Haraka sana wakambeba, ikaitwa bajaji, akapandishwa na kuanza kukimbizwa hospitalini huku wengine wakiwa kwenye pikipiki. Njiani, Ashura alikuwa akijiuliza zaidi kuhusu ajali ile, kilikuwa ni kitu kisichowezekana kwa kitu hicho kutokea.
Swali lake kubwa lilikuwa ni lile gari lililokuwa limewagonga, kwa nini dereva alikimbia bila kuwapa msaada? Na kama kweli alikimbia basi alikuwa kwa mwendo wa kasi sana kwani baada ya yeye kuanguka tu, gari hakuliona tena.
Hawakuchukua muda mrefu wakafika hospitalini, Zuhura akateremshwa, akapakizwa juu ya machela na kuanza kusukumwa kuelekea ndani. Kila mtu aliyekuwa akimuona, alijiuliza kama alikuwa mzima kwani muonekano wake haukuonyesha uzima hata mara moja.
Akaingizwa kwenye chumba cha upasuaji huku Ashura akibaki na watu wengine aliokuja nao kutoka kule barabarani. Kichwa chake kilikuwa kimechanganyikiwa, yaani hakufikiria kuhusu rafiki yake kitu kilichomuumiza kichwa ni namna ile ajali ilivyotokea.
“Kwani ilikuwaje?” aliuliza mwanaume mmoja huku akimwangalia, naye alikuwa kule barabarani, alikuwa mmoja wa vijana walimpeleka Zuhura pale hospitalini.
“Ni ajali! Tuligongwa na gari,” alijibu.
“Mligongwa na gari? Yaani ilikuwajekuwaje?” aliuliza.
“Gari ilikuja na kupiga honi, hata kabla ya kufanya kitu, tukagongwa,” alijibu.
“Gari gani?” aliuliza mwanaume huyo, alionyesha mshangao.
“Sijajua! Dereva alikimbia.”
“Kwani pale mliokuwa mmeanguka, gari liliwagonga dakika ngapi nyuma?”
“Kama nusu dakika, yaani ghafla!”
“Gari?”
“Ndiyo!”
“Unasema lilikuja na kupiga honi?”
“Ndiyo!”
“Mbona sisi hatukuona gari?” aliuliza.
“Hamkuona gari?”
“Ndiyo! Si muda ule uliokuwa mmeanguka! Kwani pale mligongwa na gari?”
“Ndiyo!”
“Hapana! Hapakuwa na gari!”
Ashura akanyamaza, alichokisema mwanaume huyo na mwezake kushadadia kwamba hapakuwa na gari kiliingia moyoni mwake na kumkumbusha kile alichokifikiria. Maneno yao yaliendana na kile kilichosumbua kichwa chake.
Walipoanguka na kuangalia huku na kule, hapakuwa na gari lolote lile lakini jambo jingine ni jinsi mwili wake ulivyokuwa. Kama kweli waligongwa na gari basi angekuwa na maumivu makali sana, cha ajabu kabisa, hakuwa na maumivu yoyote yale.
“Kama si gari lilikuwa nini?”
“Sisi ndiyo tukuulize wewe.”
“Ila lilikuwa linapiga honi sana!”
“Hatukusikia honi yoyote ile.”
Ashura akakaa kimya kwa sekunde chache, kwa kile alichoambiwa hakika kilimshangaza sana, hapo akaamini kweli uchawi ulikuwepo. Huku akiwa anafikiria hivyo ndipo akapata wazo kwamba inawezekana hayo yote yalisababishwa na mume wa Nasria kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa haikuwa ya kawaida hata kidogo.
Huku akiwa amekaa hapo, mara mlango wa wagonjwa mahututi ukafunguliwa na daktari mmoja aliyekuwa na koti kubwa jeupe na mashine ya kupimia mapigo ya moyo, stethoscope ikiwa shingoni mwake.
“Ndugu yake nani huyu?” aliuliza daktari huku akiwaangalia.
Haraka sana Ashura akasimama.
“Nifuate ofisini!” alisema.
Hakutaka kubisha, akaanza kumfuata ofisini kwake huku akiwa na hofu tele. Wale wanaume wengine nao hawakutaka kusubiri, wakaungana na Ashura na kuanza kuelekea huko. Walitaka kujua kilichotokea kwani nao walimsaidia mpaka kumfikisha hospitalini hapo.
Walipofika nje ya ofisi hiyo, wakaingia ndani na kukaa kwenye viti huku dokta akiwa kwenye kiti kingine. Kwa kumwangalia tu tayari walihisi kulikuwa na kitu kilichotokea, sura yake haikuwa kwenye muonekano mzuri, alikuwa na majonzi.
“Poleni sana,” alisema huku akiwaangalia.
“Tunashukuru! Anaendeleaje?”
“Kwanza ni nani kwako?”
“Rafiki yangu kipenzi, kama ndugu yangu!”
“Pole sana. Tumejitahidi sana kuokoa maisha yake lakini imeshindikana kabisa,” alisema daktari huku akiwaangalia.
Hilo walilitegemea, kwa jinsi Zuhura alivyokuwa, ilionyesha kabisa hapakuwa na mategemeo yoyote ya kupona na tena walihisi kabisa alifariki akiwa njiani kuelekea hospitalini hapo.
Ashura akaanza kulia, hakuamini alichokisikia, kwake, alimpenda sana msichana huyo, alikuwa rafiki yake wa karibu, walidanga pamoja na kufanya mambo mengi tu. Leo, Zuhura hakuwepo duniani, alifariki baada ya kuhisi alipata ajali mbaya ya gari.
Yeye ndiye akaanza kuwapigia simu marafiki zake wengine, ndugu na majamaa wa karibu na kuwapa taarifa ya msiba. Kwao, ilikuwa ni maumivu makali, hawakuamini kama Zuhura angefariki kipindi cha hivi karibuni.
Siku iliyofuata haraka sana ndugu zake wakafika Zanzibar ambapo huko waliamua kuuzika mwili wake kwani hawakuwa na pesa za kutosha kuusafirisha na kwenda kuuzika jijini Dar es Salaam.
Ashura akabaki peke yake, hakuwa na rafiki yake huyo na kitu pekee kilichokuwa kikimuumiza ni namna rafiki yake huyo alivyokufa. Hakutaka kukaa tu, ilikuwa ni lazima kuujua ukweli wa kile kilichotokea, baada ya siku mbili tu, akaamua kwenda kwa mganga.
Huko ndipo alipoambiwa kilichotokea, kwa mara ya kwanza akamjua mtu aliyeitwa kwa jina la Hussein Kaifah, mwanaume aliyetoka kwenye ukoo uliokuwa na ushirikina mkubwa nchini Oman.
Alipoambiwa kuhusu mwanaume huyo, jinsi alivyokuwa na nguvu za kumuua mtu yeyote yule ndipo akapata wazo la kuwasiliana na Nasria na kumwambia kilichokuwa kikiendelea. Kama mwanaume huyo aliamua kumuua Zuhura kwa kuwa alishirikiana na Nasria, basi aliamini kama msichana huyo hakuwa amefariki, basi zamu yake ilikuwa ikifuata.
Akajaribu kumpigia simu, haikuwa ikipatikana, hakutaka kubaki Zanzibar, alichokifikiria ni kesho kuondoka huko na kuelekea jijini Dar es Salaam, aende nyumbani kwao, azungumze naye na kumwambia sasa alitakiwa kujilinda kwani yule mwanaume aliyemkimbia alikuwa mtu hatari sana kwenye masuala ya uchawi.
“Ngoja nikamuokoe, akajilinde anavyoweza,” alisema Ashura huku hata naye akionekana kuogopa, kwa kilichotokea, aliamini kweli uchawi ulikuwepo.

Je, nini kitaendelea?
Je, Ashura atamuwahi Nasria?
Je, Nasria atakufa?
Nini kitatokea endapo atakufa?

Mkuu asante sana sana japo umeirudia mara mbili
 
NYEMO CHILONGANI
MEDUSA: MALKIA WA DAMU
SEHEMU YA 05

Japokuwa Ashura alikuwa akienda jijini Dar es Salaam kuonana na wazazi wa Nasria lakini hakuacha kujaribu kumpigia simu kujua kama alikuwa akipatikana ama la. Majibu ya jana ndiyo yalikuwa ya siku hiyo, msichana huyo hakuwa akipatikana.
Moyo wake ukaanza kuwa na hofu kwamba inawezekana alikufa na mume wake kwani kwa kipindi hicho, tayari msichana aliyekuwa ameshirikiana naye, Zuhura alikufa kwenye kifo kilichoacha maswali mengi mno.
Boti ilikuwa ikiendelea kukata mawimbi, alisimama pembeni kabisa, hakutaka kuongea na mtu yeyote yule, kichwa chake kilikuwa kikifikiria mambo mengi yaliyotokea siku ile ambayo yeye na rafiki yake waligongwa na kitu alichohisi kilikuwa gari na kutupwa chini.
Kulikuwa na mauzauza yaliyomfanya kugundua huyo Hussein hakuwa mtu wa masihara na alitakiwa kuzungumza na rafiki yake haraka sana ili waone ni kwa namna gani angeweza kuepuka kifo ambacho alihisi kingemfuata mahali popote pale atakapokwenda.
Boti ilichukua saa moja na nusu hatimaye ikafika katika Bandari ya Azam na kuteremka. Hakutaka kuchelewa, haraka sana akachukua bodaboda ambayo ilimpeleka mpaka katika Mtaa wa Magomeni kwa lengo la kuonana na msichana huyo kwanza kabla ya kufanya lolote.
Alipofika, akateremka na kumlipa dereva pesa yake na kuanza kuelekea ndani huku moyo wake ukiwa na shauku ya kutaka kumpa taarifa Nasria kuwa hakutakiwa kuwa na masihara kwenye jambo hilo hata kidogo.
Alikuwa akijulikana mahali hapo, akakaribishwa na mama yake Nasria, akaingia na kukaa kwenye kochi huku akipulizwa na feni lililokuwa sebuleni.
Mwanamke huyo alimshangaa tu, alichokijua ni kwamba Nasria aliolewa, kama msichana huyo alifika mahali hapo kumsalimia Nasria inamaana hakuwa amempa taarifa ya harusi yake ama vipi?
“Karibu sana binti yangu,” alimkaribisha msichana huyo.
“Nashukuru sana! Nimemkuta Nasria?” alimuuliza huku akimwangalia.
Alilitegemea swali hilo, inawezekana kabisa Nasria hakuwa amempa taarifa kama alikuwa akiolewa na ndiyo maana siku hiyo alifika nyumbani hapo kwa lengo la kumuulizia.
“Nasria aliolewa, aliondoka nyumbani na kwenda kwa mumewe, kwani hakukwambia?” alimuuliza huku akimwangalia, kwa mbali Ashura akashtuka.
“Najua kwamba aliolewa.”
“Sasa hapa atafikaje na wakati yupo kwa mumewe?” aliuliza.
Swali hilo likamfanya Ashura kugundua kuwa Nasria hakuwa amefika nyumbani hapo, inawezekana kabisa baada ya kuondoka Zanzibar, alikimbilia mahali na kuanzisha maisha yake binafsi.
Huku akifikiria hilo pia akajiwa na kitu kingine akilini mwake, hakutakiwa kujipa uhakika kwamba Nasria alianzisha maisha yake mengine, inawezekana wakati alipoondoka Zanzibar na kwenda Dar es Salaam, ule mtumbwi alioupanda ulipinduka na kuzama baharini.
Hilo likapata nafasi zaidi moyoni mwake na kuhisi inawezekana ilikuwa hivyo kwani kama kweli msichana huyo alitoroka huko Zanzibar basi ilikuwa ni lazima muda huo awe hapo nyumbani, cha ajabu hakuwepo, na mbaya zaidi hata mama yake hakuwa akijua kama alitoroka kwa mumewe.
“Mama! Naomba uniambie ukweli,” alisema Ashura huku akimwangalia mwanamke huyo.
“Ukweli gani binti yangu?”
“Nasria hajafika hapa nyumbani?” alimuuliza.
“Kufika kutoka wapi? Si nimekwishakwambia kwamba aliolewa!”
“Mama!”
“Kuna nini?”
“Nasria alitoroka kwa mumewe majuzi,” alimwambia.
Mwanamke huyo aliposikia hivyo akashtuka, hakuamini kusikia alichoambiwa, alimwangalia Ashura mara mbilimbili, alitamani kusikia kwa mara nyingine kile alichoambiwa.
Kutoroka kwa Nasria akilini mwake hakukumuingia kabisa, alihisi ni uongo tu ambao msichana huyo alifika nao nyumbani hapo na kumwambia. Alichokijua ni kwamba Nasria aliolewa na kuondoka na mumewe kuelekea Zanzibar kisha Oman, kama kweli alitoroka kwa mumwe, basi ilikuwa ni lazima kufika mahali hapo.
“Haiwezekani!”
“Mama! Niamini ninachokwambia,” alimwambia.
“Nasria aliolewa na kwenda kwa mumewe, hilo ndilo pekee ninalolijua mimi,” alimwambia.
Tayari Ashura aliona ni kwa namna gani mwanamke huyo alikuwa amechanganyikiwa, hakutaka kuzungumza kitu kwanza, alimuachia muda wa kuongea yeye tu. Aliongea kwa dakika kumi nzima, akanyamaza na kumwangalia Ashura.
Sasa hapo ndipo alipoanza kumwambia kila kitu kilichotokea kama alivyohadithiwa na Zuhura. Mama yake Nasria alikaa kimya akimsikiliza Ashura alivyokuwa akisimulia.
Hakuacha kitu, alimsimulia kila kitu mpaka rafiki yao, Zuhura alipogongwa na kitu walichohisi ni gari lakini kumbe halikuwa gari. Alipofika hapo, tayari mama yake Nasria akaanza kuonekana kuwa na majonzi, kilichosimuliwa na Ashura kilimtisha kupita kawaida.
“Inawezekana vipi?” aliuliza.
“Mama! Nasria yupo hapa hapa Dar. Alimuibia pesa yule mumewe, na sasa hivi inawezekana anakula maisha,” alimwambia.
Hilo likashindwa kuvumilika moyoni mwake, haraka sana akampigia simu mume wake na kumuhitaji nyumbani hapo kwani kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea. Ndani ya dakika chache mwanaume huyo alikuwa mahali hapo na kuanza kuhadithiwa kile kilichotokea.
Kama ambavyo asivyoamini mke wake hata naye ilikuwa hivyohivyo, hakumwamini mkewe wala Ashura aliyekuwa amepeleka taarifa nyumbani hapo, alichokifanya ni kuchukua simu yake na kumpigia binti yake, simu haikuwa ikipatikna.
“Nasria alibadilisha namba,” alimwambia.
“Wewe umejuaje haya yote?”
“Nilihadithiwa na Zuhura.”
“Ndiye nani?”
“Huyo rafiki yangu!”
Sasa wote wakabaki kimya na kuangaliana.
Taarifa waliyoipokea ilikuwa ni ya hatari sana na kitu kilichokuja mioyoni mwao ni kwamba mpaka muda huo tayari Nasria alifariki dunia hivyo ilikuwa ni lazima kuanza kutafuta mwili wake, haraka sana harakati zikaanza.
Sehemu ya kwanza kabisa kwenda ilikuwa ni Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Walikwenda huko na kuanza kuulizia, walitoa sifa ya Nasria kwa muonekano wake, jinsi alivyokuwa na vingine vingi, huko wakajibiwa hapakuwa na maiti iliyokuwa na muonekano huo.
Walipotoka hapo wakaenda kwenye hospitali nyingine lakini majibu yalikuwa hayohayo, maiti ya Nasria haikuwa imepatikana. Kila mmoja alionekana kukata tamaa, hapo wakakumbuka kulikuwa na hospitali kubwa ambayo hawakuwa wameiangalia, hiyo ilikuwa ni Kairuki, ilikuwa ni lazima kwenda huko na kuulizia kwanza.
Walipofika, wakaambiwa ni kweli kulikuwa na maiti ya msichana wa Kiarabu iliyokuwa imepelekwa hospitalini hapo na mpaka muda huo hapakuwa na ndugu yeyote aliyekuja kuripoti zaidi yao, kuna uhakika wa asilimia mia moja akawa huyo Nasria.
Waliposikia hivyo mama yake akaanza kulia kwa uchungu kuondokowe na binti yake, moyo wake ulichoma na kuhisi maumivu ambayo hakuwahi kuyasikia kabla. Alimpenda binti yake, alikuwa msichana wa pekee, aliyeringia naye, hakubahatika kuwa na msichana mwingine zaidi ya huyo, watoto wake wengine wawili wote walikuwa wa kiume.
Wakataka kuiona maiti hiyo, hapakuwa na shida, daktari akawachukua na kuwapeleka mpaka mochwari, walipofika huko, masanduku yakaanza kutolewa, maiti mbalimbali zikaanza kuonyeshwa, waliogopa lakini hawakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima wajue kuhusu binti yao.
“Mkuu! Unatafuta maiti ipi?” aliuliza kijana mmoja aliyekuwa akilinda humo.
“Yule binti Mmanga!” alijibu daktari.
“Oh! Yule nilimuhamisha, niliupeleka mwili wake kule,” alijibu kijana huyo huku akianza kuelekea mahali ambapo mwili wa msichana huyo ulipokuwa.
Muda wote huyo mama yake Nasria alikuwa akitokwa na machozi tu, hakuamini kama mwisho wa maisha ya binti yake yangekuwa ndani ya chumba hicho kikubwa kilichokuwa na baridi kali.
***
Nasria aliamua kuwa na maisha yake, hakutaka kurudi nyumbani kwao, ilikuwa ni lazima kuishi kisiri pasipo mtu yeyote kugundua kama alikuwa jijini Dar es Salaam.
Hakutaka kuwasiliana na ndugu yeyote yule zaidi ya Zuhura ambaye ndiye aliyekuwa akijua kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Alitaka kuishi maisha yake mpaka siku ambayo angeamua kwenda nyumbani kwao kutembea basi kila mtu ayashangae mafanikio yake na kusiwe na mtu yeyote wa kumpigia kelele kwa lolote lile.
Kitu cha kwanza alichofikiria ni kuwa na nyumba yake, alimuibia mume wake pesa nyingi ambazo zingeyaendesha maisha yake na hata kama angefungua biashara bado angekuwa na uwezo wa kusimamia na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alifikia loji iliyokuwa Mwenge na kesho yake akaamua kuanza safari ya kuelekea Mtaa wa Tandale kwa lengo la kuonana na dalali yeyote na kumuuliza kama kulikuwa na nyumba yoyote iliyokuwa ikiuzwa.
Alitaka kuhamia Tandale, Manzese ama Mwananyamala, kwa pesa aliyokuwanao aliamini angepata nyumba nzuri huko, angeishi maisha yake na kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angejua kama alikuwa akiishi huko.
Alipofika huko, akaonana na dalali na kumwambia alichokuwa akikihitaji. Dalali huyo aliyeitwa Kidiru akamwambia kulikuwa na nyumba mbili zilizokuwa zikiuzwa, kama kweli alikuwa na pesa, basi hapakuwa na tatizo.
“Gharama?”
“Moja milioni hamsini na nyingine sabini. Zote zina wapangaji wake,” alimwambia.
“Haina shida. Twende tukazione,” alimwambia.
Hilo halikuwa tatizo, akachukua simu yake na kumpigia dalali mwenzake aliyeitwa Mzee Tesha na kuomba kuonana naye, haraka sana mzee huyo akafika na watatu wote kuongozana mpaka huko kulipokuwa na nyumba ya kwanza.
Nyumba hiyo ilikuwa Kwa Mkunduge karibu kabisa na barabara ya lami, ilikuwa nyumba nzuri lakini kwa jinsi alivyoiangalia, na kwa jinsi eneo hilo lilivyokuwa alihisi kabisa mahali hapo kulipokuwa kukinyesha mvua kubwa basi kulikuwa na mafuriko.
Aliwaambia madalali kuhusu hilo, wakaangaliana na kumwambia basi waongozane kwenda kuangalia nyumba nyingine iliyokuwa Kwa Tumbo karibu na msikikiti.
Wakaenda huko na kuiona nyumba hiyo. Ilikuwa nzuri na ilikuwa sehemu nzuri, akatokea kuipenda, ilikuwa na vyumba vinne vya wapangaji na chumba kimoja kilikuwa na choo kwa ndani.
“Hii ndiyo kiasi gani?” aliuliza.
“Milioni sabini.”
“Nyingi sana!”
“Yaani dada‘angu sijui nikwambieje!”
“Niambie lolote lile ila hiyo sabini nyingi. Kama sitini nitatoa. Ila kama mwenye nyumba hataki kwa sitini, basi acha nikaangalie hata kule Tabata,” aliwaambia.
Madalali hao wakaangaliana. Kwa jinsi msichana huyo alivyoonekana, alikuwa na pesa nyingi, kama alikubali kutoa kiasi cha shilingi milioni sitini, basi wao walitakiwa kufanya juu chini wampeleke kwa mwenye nyumba kwa lengo la kuingia makubaliano.
Mwenye nyumba alikuwa akihitaji shilingi milioni hamsini tu ili ahamie zake huko Mbagala, aishi karibu na barabara iliyokuwa ikielekea kwao huko Tandahimba.
Kabla ya kuitiwa mwenye nyumba, wakamuita na kuanza kuzungumza naye, walimpanga kabisa ili asije kuharibu kabisa na mteja kukimbia. Walimwambia kila kitu na kuonana na Nasria, wakazungumza, walipokubaliana msichana huyo akaahidi kurudi baada ya siku mbili akiwa na mwanasheria wake na pesa hizo.
Alikuwa na pesa, hakuwa Mswahili, baada ya siku mbili akarudi akiwa na pesa, mwanasheria wake na kumalizana kila kitu. Mwenye nyumba alihitaji pesa taslimu mkononi, hakutaka kuingiziwa benki, hivyo akapewa pesa zake, Nasria akakabidhiwa hati ya nyumba, kila kitu kikakamilika siku hiyo na hatimaye kuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo.
Sasa kilichokuwa kimebaki ni kuangalia biashara gani alitakiwa kufanya kuanza maisha yake mapya hapo Tandale Kwa Tumbo. Kulikuwa na biashara nyingi lakini kwa haraka biashara ambayo ilikuja kichwani mwake ni kufungua mabanda ya chipsi na chakula cha kawaida, akanunua bodaboda nne na bajaji mbili kisha kuanza kuingiza pesa huku akiwa anafikiria ni kwa namna gani angeanza biashara ya nafaka, yaani achukue mchele na mahindi mikoani na kuipeleka jijini Dar es Salaam.

Je, nini kitaendelea?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA 06

Kila mwanaume Tandale aliyemuona Nasria alishtuka, hapakuwa na mtu aliyetegemea msichana mrembo kama huyo angekwenda kuishi huko uswahilini. Ndiyo! Huko kulikuwa na wanawake wengi warembo lakini hiyo haikumfanya Nasria kwenda kuishi huko.
Wale vijana waliokuwa na tamaa kama kawaida yao wakaanza kufanya mishemishe kuhakikisha wanampata msichana huyo. Kwa namna alivyokuwa mrembo na kuvutia, kila mmoja alitaka kuhakikisha anampata na kuwa naye.
Madereva bodaboda nao walikuwa mstari wa mbele, walikuwa wapo tayari kumpa lifti msichana huyo popote pale alipokuwa akienda lakini mwisho wa siku kuwa naye kimapenzi lakini bahati mbaya kwao, huyo Nasria hakuwa mtu wa kupenda mapenzi, tena kipindi hicho aliyachukia haswa.
Aliyaangalia maisha yake, alikuwa na pesa za kufanya lolote lile, alitakiwa kuyaendesha maisha yake yawe juu, kwa pesa alizomuibia mume wake basi zimnufaishe na kuwa tajiri mkubwa mno na kuacha alama nyuma yake kipindi atakachofariki dunia.
Maisha yake yalikuwa ni Tandale tu, alisimamia biashara zake alizoanzisha na kufanya mambo mengine. Ilichukua siku kama tano hivi ndipo vijana wakagundua kwamba huyo Nasria alikuwa tajiri, mwanamke mwenye pesa zake hivyo hakuwa na haja sana ya kuwa na mwanaume aliyekuwa na pesa.
Hapo, wakapiga hatua na kurudi nyuma. Huyo Nasria alikuwa mrembo na pia tayari dalili zilionekana kuwa mgumu sana kuingia mikononi mwako kwa sababu kusingekuwa na kitu chochote kile ambacho kingemfanya akupende, kwani kama ni pesa alikuwanazo nyingi sana.
Wakati vijana wakianza kumuogopa kwa sababu ya pesa alizokuwanazo, hilo lilikuwa tofauti kwa kijana aliyeitwa kwa jina la Kamulika. Huyu alikuwa mmoja wa vijana watanashati waliokuwa wakiishi maisha ya kawaida kabisa.
Hakuwa amesoma sana lakini alikuwa na uelewa mkubwa kuhusu maisha. Kwa siku ya kwanza tu kumuona Nasria alishtuka, hakukumbuka kama aliwahi kumuona mwanamke mzuri kama alivyokuwa huyo aliyesimama mbele ya genge akinunua mahitaji yake.
Alisimama na kumwangalia tu na aligundua kila mwanaume aliyekuwa maeneo hayo alikuwa akimwangalia Nasria lakini hakuthubutu kumfuata, kila mtu alikuwa akimuogopa.
Hakutaka kuacha kumwangalia, kitu cha kwanza kilikuwa ni kufahamu mahali alipokuwa akiishi ili iwe rahisi kwake kumfuata na kufanya mambo yake, alipomuona anaondoka gengeni, akaanza kumfuatilia kwa nyuma mpaka alipokuwa akiishi na kuingia ndani.
Hapo akaridhika, huo ukawa mtihani wa kwanza aliotaka kuufahamu, kujua mahali alipokuwa akiishi na mtihani wa pili ulikuwa ni kutaka kufahamu kuhusu Nasria, aliitwa nani na alikuwa akifanya kazi gani, kubwa zaidi pale alikuwa akiishi na nani.
Kupata taarifa hizo zote ilikuwa ni kwa vijana wa bodaboda, hao ndiyo waliokuwa wakimfahamu kila mtu mtaani hivyo kuwafuata na kuanza kuzungumza nao na kuwauliza kuhusu mwanamke huyo.
“Yule demu mkali sana aiseee! Kumbe hata wewe umeona!” alisema bodaboda mmoja.
“Si mchezo aisee! Kanipagawisha sana. Hivi anaishi na nani pale?” aliuliza.
“Anaishi peke yake!”
“Peke yake?”
“Ndiyo! Amenunua ile nyumba. Demu ana mtonyo kishenzi!” alisema bodaboda yule huku akimwangalia Kamulika ambaye sasa tayari alionekana kupagawa.
“Amenunua nyumba? Ana mtonyo kumbe?” aliuliza Kamulika kwa mshangao.
“Noma sana!”
Baada ya kusikia hivyo akaondoka zake. Hakutaka kuendelea kusikia kuhusu huyo Nasria, yaani alitakiwa kujipanga na kujua ni kwa namna gani angeweza kumpata kwani ingeshindikana endapo tu angekwenda kwa staili ya kujifanya ana pesa nyingi.
Kwa kuwa alikuwa na akili, uelewa mkubwa, siku ambayo alimuona tena gengeni hakutaka kuchelewa, kulikuwa na baadhi ya wanawake wengine lakini naye akaenda kujumuika, lengo lake kubwa likiwa ni kuongea na msichana huyo na si kununua mahitaji yoyote yale.
Kwa wanaume ambao walimuona, tayari walijua lengo lake lilikuwa nini. Hawakuamini kama kamulika angempata mwanamke huyo, alikuwa mzuri, alipendaza na kuvutia machoni, kubwa zaidi alikuwa na pesa, sasa huyo Kamulika angempata kwa staili gani.
Alipofika pale, kila mwanamke akawa anamwangalia, alinukia pafyumu nzuri sana, Nasria mwenyewe akahamisha macho na kumwangalia Kamulika, naye akajifanya kutokujali, akawa amesimama huku akijifanya kusubiria huduma.
“Mbona huna kamba mguuni?” alimuuliza Nasria kwa sauti ya chini, swali hilo likamshtua Nasria na kujiangalia miguuni.
“Kamba gani?” aliuliza baada ya kuona hakuna kamba yoyote ile.
“Kuku mgeni hakosi kamba mguuni!” alimwambia Nasria na kutoa tabasamu.
“Eh! Makubwa!”
“Umekuja lini mtaani kwetu bila kuniambia mwenyekiti wa mtaa?” alimuuliza huku akimwangalia.
“Unanijua?”
“Hapana! Ni mgeni kiasi machoni mwangu, nimeshangaa kukuona kama mara tatu halafu sina taarifa kuhusu ujio wako,” alimwambia.
“Upate taarifa kuhusu ujio wangu?”
“Yeah! Kwa sababu mimi ndiye kiongozi hapa mtaani!” alisema Kamulika.
Nasria hakujibu kitu, alibaki akimwangalia Kamulika na baadaye kuhamisha macho yake na kumwangalia muuzaji na kuhitaji huduma yake.
“Naitwa Kamulika! Nimefurahi sana kukuona! Kama utakuwa na tatizo lolote lile, ama kuna mtu anakusumbua, nitaarifu, nitahakikisha unaishi bila hofu yoyote!” alimwambia.
“Sawa.”
“Uwe na asubuhi njema!” alimwambia na kuondoka.
Nasria alibaki akimwangalia, hakuwahi kuzungumza na mwanaume yeyote kwa muda mwingi kama huyo, wengi walimuogopa, alilijua hilo, alijua aliogopwa kwa sababu ya maisha yake.
Hakutaka kuona hilo likitokea, alikuwa kama wanawake wengine, alitamani kufuatwa na kutongozwa ili kuona kweli alikuwa mzuri, sasa kwa kitendo cha kutokufuatwa, kama msichana alijisikia vibaya moyoni mwake.
Huku hilo likiwa linamtesa, ghafla akaja Kamulika. Mwanaume huyo alimshangaza kwa kuwa hakumuogopa hata kidogo, alizungumza naye na kuondoka zake. Alibaki akimwangalia lakini akaamua kuachana naye.
Hicho kilikuwa kizingiti cha kwanza alichokiruka Kamulika, ilikuwa mbinu ya kwanza ya kijeshi ambayo ilitakiwa kufanywa na mwanaume yeyote yule kwa mwanamke mgeni mtaani.
Kwa mwanaume yeyote ambaye alikuwa akimtaka mwanamke yeyote mgeni mtaani kwao, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumfuata na kuzungumza naye, kwanza ilikuwa ni lazima aizoee sura yako, sio kumfuata siku moja na kuanza kumtongoza huku ukionekana kuwa mgeni kwake, hakika atakukataa tu.
La kwanza ni kumfuata, kuongea naye hata kwa dakika moja, mchangamkie, umwambie kwamba mara kwa mara umekuwa ukimuona hata kama haukuwa ukimuona, hilo litamfanya kuhisi kumbe ulikuwa unamfuatilia, unafanya yote hayo ili akufahamu kwa sura, siku ya pili ukimfuata, hutokuwa mgeni kwake, atakuwa anakujua kwa sababu aliwahi kukuona siku ya kwanza.
Baada ya kuzungumza naye kwa mara ya pili, sasa hapo unaweza kujitambulisha rasmi na hata kumuomba namba yake ya simu, kwenye hilo hutakiwi kubembeleza sana, omba namba kama huna kazi nayo, akikunyima, usipaniki, mwambia haina shida, baada ya hapo mtakie siku njema na ondoka zako.
Kesho hakikisha huonekani machoni mwake, jifiche, siku ya pili jifiche tena na siku ya tatu jitokeze halafu uanze kulalamika kwa nini hukumuona kwa siku mbili na wakati ulimmisi, hapo, tayari mwanamke ataanza kujiona wa muhimu kwako, mwambie jinsi ulivyokuwa ukipata shida kumtafuta, yaani endapo ungekuwa na namba yake, basi ungempigia japo usikie sauti yake nzuri, halafu baada ya kumwambia hayo, muombe namba yake. Hawezi kukunyima.
Hilo ndilo allolifanya Kamulika. Baada ya kuongea na Nasria kwa siku ya kwanza akaondoka zake, siku iliyofuata akajificha, na siku nyingine pia akajificha na siku ya tatu alipomuona anakwenda gengeni akamfuata. Nasria alipomuona tu, akamkumbuka kijana huyo.
“Kwa hiyo ukaamua kujificha ili nisikuone tena?” alianza kusema Kamulika hata kabla ya salamu.
“Kujificha?”
“Ndiyo! Nilikukumbuka tu! Nikakusubiri sana nione japo ukipita lakini kwa siku mbili mfululizo hukupita. Kwa nini sasa uliamua kufanya hivyo?” alimuuliza huku akimwangalia.
“Wala sikujificha!”
“Kumbe nisemeje? Mpaka nikahisi umetekwa ama kuhama nyumba baada ya kugundua huku ni wachawi sana,” alisema Kamulika kwa utani.
Aliyazungumza maneno hayo kwa sababu hakutaka kumjulisha Nasria kwamba nyumba ilikuwa yake. Alitaka kumfuata huku akijifanya hajui kama nyumba ile aliinunua, yaani hakutaka kumfanya kugundua kama alijua alikuwa na pesa.
Alijua kabisa endapo angejifanya kumjua sana Nasria kwamba alikuwa na pesa basi ingekuwa na ugumu mno kwake kwa kuwa tayari msichana huyo angejua alifuatwa kwa ajili ya pesa alizokuwanazo, hivyo akaamua kumshusha.
“Kwani kuna wachawi huku?”
“Yeah! Wapo ila si wengi. Nilikuulizia sana lakini kila mtu akawa ananishangaa tu!”
“Uliniulizia? Kwa nani?”
“Kwa watu kama wamekuona. Unajua nilikumisi sana mpaka nikajiona nimebeba mzigo mkubwa. Kuja pale kwenu nikawa naogopa, nikajisemea nisije kutolewa ngeu bure!” alisema na kutoa kicheko cha chini.
“Mh! Aya!”
“Kwa hiyo unanisaidiaje sasa?”
“Kuhusu nini?”
“Ikitokea siku nimekumisi tena halafu ukajificha au nitaruhusiwa kuja kukuulizia kwenu?,” alimuuliza.
“Hapana huruhusiwi!”
“Mh! Sawa! Na nitaruhusiwa kuwa na namba yako?”
“Ya nini?”
“Kukubipu kila nikikumisi!” alimjibu, kidogo Nasria akatoa tabasamu.
“Namba yangu huwa sitoagi!”
“Hata kwa mtu kama mimi ninayekumisi sana na kukutafuta kama pesa?”
“Huwa sitoi!”
“Hapana bwana Nasria! Naomba uniandikie,” alimwambia, tayari alitoa simu na kuishika.
“Umelijuaje jina langu?”
“Mbona wewe staa sana hapa mtaani! Kila mtu anakujua,” alimwambia, Nasria akashtuka.
“Kila mtu ananijua?”
“Ndiyo!”
“Mimi sio staa!”
“Inawezekana wewe sio staa, ila sura yako ni staa. Uzuri wako umekuwa gumzo kila kona, kila sehemu watu wanabishana, wengine wanasema umezaliwa, wengine wanasema umeshushwa, wengine wanasema wewe ni binadamu, wengine wanasema wewe ni malaika! Ila mimi naungana na kundi la hao wanaosema wewe ni malaika. U mzuri sana Nasria,” alimwambia, msichana huyo akaanza kusikia aibu. Kamulika akaona hiyohiyo ndiyo njia ya kupata alichokuwa akikihitaji.
“Hebu acha maneno yako!”
“Nasria! Uzuri wako ni wa ajabu sana, hebu tazama watu wanavyokuangalia,” alimwambia, Nasria akasikia aibu zaidi.
“Naomba uniandikie namba yako! Nakuahidi sitokusumbua,” alisema Kamulika, hapohapo Nasria akachukua simu ile ya Kamulika na kumuandikia namba yake. Baada ya kumaliza, huyooooo, Kamulika akaondoka zake.
“Amekwisha!” alijisemea huku akipiga hatua kutokomea zake.

Unatuweka sana mkuu na hii simuliz yako isije ikawa unampango wa kutuacha njia panda. Mkuu nashukuru story ni tamu na inamafundisho flan tunayapata
 
Mzigo umetulia sana
 
SEHEMU YA 07.

Ilikuwa ni lazima Nasria atoke ndani ya chumba hicho na kurudi nyumbani kwake lakini hakujua ni kwa namna gani angeweza kuondoka bila kugundulika. Yule mwanamke jini lilipotea na kutimka zake, lilimwacha ndani ya chumba kile huku akiwa na mwili wa Kamulika tu.
Hakujua afanye nini na kutoka, kumfuata dada wa mapokezi na kumwambia yule mwanaume alikufa chumbani kwake angeaminika kwa kuwa kweli amekufa na mwili wake kuonekana kitandani ila suala la kumwambia ni jini ndilo lililomuua, hakia kingekuwa kichekesho na kila mtu angemuona alikuwa akijitetea.
Kurudi mapokezi na kumwambia mhudumu kwamba kulikuwa na maiti lingekuwa jambo gumu sana na kitu alichokifikiria ni kuondoka chumbani humo. Kitu cha kwanza kabisa alichokifanya ni kufuta alama zote za vidole kwa kutumia kitambaa kilichokuwa na unyevunyevu.
Alifanya hivyo kwa kuwa alipenda sana kusoma simulizi za kipelelezi, pale wauaji walipokuwa wakimmaliza mtu, kitu cha kwanza kilikuwa ni kufuta alama za vidole vyao ili kuwapa kazi polisi kuwatafuta, naye alifanya hivyo.
Alipomaliza, akahakikisha hajasahau kitu, akakishika kitasa na kuufungua mlango, halafu akafuta tena alama za vidole vyake na kuanza kutembea kuelekea mlango wa nyuma. Alitaka kutoroka kupitia huko. Kwenye loji nyingi huwa na mlango wa nyuma ambao huwa mahususi kwa wazinzi wote ambao hawakutaka kuonekana mlango wa mbele, hasa wale waliokuwa wakiingia na wake za watu ama walikuwa wakifahamika sana.
Alikwenda huko, akakutana na geti, huku akionekana kutokujiamini, akalifungua na kuondoka zake, sasa akawa anatembea kwa mwendo wa haraka kutafura bodaboda. Akiwa njiani ndipo akaanza kukumbuka kilichokuwa kimetokea chumbani mule, akaanza kulia, hakika aliumizwa na hakujua lile jini lilifanya nini mpaka kumuingia.
Aliliota usiku huo, likampa mhemko mkubwa wa kufanya mapenzi, akamtafuta Kamulika lakini kilichotokea, likajitoa mwilini mwake na kumuua. Machozi yalikuwa yakilowanisha macho yake, aliumizwa moyoni, hakuamini kama alisababisha kifo cha mwanaume huyo.
Huku akiwa anaendelea kuomboleza, sasa akaanza kuwa na hofu wa watu wengine kufahamu kilichotokea, ilikuwa ni lazima watu wagundue kama yeye ndiye aliyesababisha hilo kama tu Kamulika aliwapigia simu marafiki zake usiku ule na kuwaambia alikuwa akimfuata.
“Ningechukua na simu yake!” alijisemea.
Alifanya kosa kuiacha kwani namba yake ingeonekana humo, uchunguzi wa polisi ungefanyika hata kupitia kwa simu ya Kamulika, na endapo namba yake ingeonekana, tena akiwa amempigia simu basi lingekuwa tatizo.
Alichokijua polisi wangeanza na yule mhudumu, angeelezea kilichotokea na baada ya hapo, wangetaka kumfahamu mwanamke aliyekuwa humo. Ili kumfahamu ilikuwa ni lazima kuchukua simu yake na kuangalia namba iliyoingia muda huo, ilikuwa ni lazima kuiona namba yake, angepigiwa simu na kutakiwa kituo cha polisi, endapo angefika huko na kukutana na yule mhudumu, ilikuwa ni lazima kumkumbuka.
“Nifanye nini?” akajiuliza huku akiwa na hofu.
Kurudi kule loji lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo, kurudi huko ilimaanisha alikuwa akiyarudia matatizo yake, alihisi inawezekana mhudumu ama watu waliochukua vyumba vya jirani tayari walijua kilichotokea, endapo angejifanya kurudi, angedakwa na kupelekwa polisi.
“Kurudi ni upumbavu!” alijisemea.
Moyo wake ukaingia kwenye mateso makubwa na hofu nzito, hakujua ni kipi hasa alitakiwa kufanya, alijiona kuanza kupitia kwenye matatizo makubwa mno, hakutaka kufungwa jela wala kupata tatizo lolote lile, alikuwa na pesa, biashara zake, alitaka kuona zikiendelea na kuwa tajiri mkubwa.
Mwanamke jini.
Huyo ndiye aliyempa maswali makubwa, hakuwahi kuwa na jini, alisoma madrasa tangu akiwa binti mdogo tu, alishiriki kwenye shughuli zote za Kiislamu zikiwemo Maulidi lakini kote huko hakuwahi kuona ama kuambiwa alikuwa na jini, hilo jini lilitoka wapi na nini kilitokea?
Hakumfikiria mume wake wala kumuwaza kwa lolote baya, alichokijua ni kwamba walimalizana na wakati ndiyo kwanza mwanaume huyo alikuwa ameanza. Alitembea mpaka alipofika katika Barabara ya Shekilango sehemu iitwayo Sinza Makaburuni na kuita bodaboda.
Akataka apelekwe Manzese Tip Top, hilo halikuwa tatizo, akachukuliwa na kupelekwa huko kulipokuwa na klabu ya usiku. Alifanya hivyo makusudi kwa kuwa hakutaka kugundulika kabisa, bodaboda ilichukua dakika kadhaa, ikafika, akamlipa dereva na kuondoka zake.
Akasimama kwa dakika kadhaa, kulikuwa na watu wengi kiasi waliokuwa wakiendelea na mambo yao, hakutaka kujishughulisha nao sana, kwa jinsi alivyokuwa, muonekano wake kila mmoja alihisi alikuwa mmoja wa wanawake waliokuwa wakijiuza.
Akaenda mbele mpaka alipoona bodaboda nyingine na kuichukua ambayo ilimpeleka Tandale. Kila kitu alichokuwa amekifanya kilitokana na simulizi mbalimbali za kipelelezi alizowahi kuzisoma.
Kama mtu amefanya kosa sehemu na aliona baada ya hapo angetafutwa, mara baada ya kuchukua usafiri ilikuwa ni lazima kubadilishabadilisha, hilo lingewafanya hata watu kumpa kuwa vigumu.
Kwa alichokifanya, hata kama asubuhi ingegundulika maiti halafu kuifuatilia, hata kama wangempata dereva ambaye alimpeleka Manzese, angesema yeye alimpeleka huko na kuondoka kumbe mwenzake alichukua bodaboda nyingine na kumpeleka Tandale, tena si bodaboda ya eneo aliloachwa.
Alipofikishwa Tandale, akateremka na kufungua geti na kuingia chumbani kwake, sehemu ya kwanza kwenda ilikuwa ni bafuni, akaoga na kwenda chumbani. Usingizi haukuja, alikuwa na hofu tele na alikuwa akifikiria kile kilichokuwa kimetokea.
Hakika kilimtisha, hakuamini kama kwenye maisha yake siku moja angemuona mtu akifa

Je, nini kitaendelea?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom