Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 308
- 1,354
NYEMO CHILONGANI
0718069269
Sehemu ya 01
Ndiyo ni mzuri!
Tena hasaaa!
Kwanza ni mweupe.
Ana mwili ulionyambulika.
Macho ya goroli, ya kurembua ambapo akiamua kukuangalia, basi tuseme umepata bahati ya kuangaliwa na mwanamke mzuri, inawezekana kuliko wote waliokuwa wakikaa jijini Dar es Salaam.
Kwa jina aliitwa Nasria Abdul, msichana aliyekuwa na mchanganyiko wa rangi, baba yake alikuwa Mwarabu wa Oman aliyezaliwa na kukulia Zanzibar huku mama yake akiwa Mzigua kutoka Handeni, jijini Tanga.
Nasria alikuwa na uzuri wa asili, alivutia, alipendeza kila alipokuwa akitembea, alijua kuringa, kama watu walisema twiga walikuwa wakitembea kwa maringo, basi tuseme hao twiga walijifunza kwa binti huyu mrembo namna ya kutembea.
Naam!
Alijua kutembea.
Alirusha mikono yake kwa madaha.
Alikilegeza kiuno chake.
Kifua saa sita.
Huku lipsi zake nene na laini akipenda kuzipitishia ulimi.
Kila aliyekuwa akiziangalia, alitamani kuzinyonya, tena azinyonye hasa, azipake hata asali, halafu azinyonye tena mpaka asali iishe mdomoni, yaani huyu msichana hakuisha hamu hata kidogo, na kama ungepewa karatasi uandike sifa za uzuri wake, si ajabu ukajaza kitabu kikubwa na bado isitoshe kuzimaliza.
Nasria alikuwa akiishi Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam, mahali kulipokuwa na wanawake wengi wa Kipemba, waliojua kuvaa, kunukia na hata kuringa. Nasria alikuwa miongoni mwao, alikuwa binti mrembo kupita kawaida, halafu hakuwa yule mwepesi kwamba mwanaume huyu akienda, amvulie nguo, yule akienda basi aende nyumbani kwake.
Huyu Nasria alikuwa tofauti kabisa. Alijiheshimu, alikuwa na nidhamu na kitu kikubwa kabisa alikuwa msafi, tena msafi sana, yaani hakuwahi kunuka kwapa wala jasho, hakuwahi kunuka sehemu yoyote ile mwilini mwake, na endapo ungebahatika kuvuliwa nguo na msichana huyu, basi ungesema sasa uliingia kwenye duka la manukato, yaani alinukia kila harufu ya pafyumu.
Unadhani kuna mtu Magomeni ambaye hakuwa akimfahamu msichana huyu? Atoke wapi? Wanaume wote waroho walimtamani, kulikuwa na wanamuziki waliokuwa wakimuimbia yeye tu, kuna waandishi walikuwa wakiandika simulizi na kulitumia jina lake, wapo watu waliokuwa wakifanya kila kitu kwa ajili yake lakini huyu Nasria, hakuwa msichana wa kawaida hata kidogo.
Ulipomuita.
Alikuitikia.
Uliongea naye.
Unamuomba namba ya simu.
Bila hiyana anakupa huku akitabasamu.
Ila ukimpigia na kumwambia ushenzi, anakubloku.
Ndiyo!
Anakubloku.
Kulikuwa na wanaume wengi waliblokiwa na msichana huyo, si kwamba hakutaka kuwa na mwanaume yeyote yule, alitamani lakini alisema hakuwahi kumuona mwanaume muoaji, yaani kwake wote walikuwa wababaishaji tu.
Huyo alikuwa Nasria.
Msichana mzuri kupindukia.
Nasria hakuwa bikira, kwa miaka yake ishirini tayari kulikuwa na wanaume wawili ambao walifanikiwa kumvua nguo zake, wakambakiza mtupu kabisa, kama alivyotoka tumboni mwa mama yake, wakamwambia alale kitandani, alitii na hivyo kumfanya walivyotaka wao.
Aliyemtoa bikira aliitwa Rahim, alidumu naye kwa miezi kadhaa tu, wakaachana, kisa tu alimfumania akiwa na mwanamke mwingine, tena chumbani kwake alipokwenda kumtembelea kwa kushtukiza.
Akajiapiza kwa viapo vyote kwamba asingeweza kuwa na mwanaume yeyote yule, kama ingekuwa rahisi kwake kwenda mahakamani na kuapa, basi angekwenda ili akaape vizuri kuwa hakutaka kuwa na mwanaume yeyote yule kwani kwa jinsi Rahim alivyomfanya, mapenzi yakaingia shubiri na kumuumiza kupita kawaida.
Sasa moyo wake ukachomwa na mkuki.
Ndiyo, mkuki wa mapenzi moyoni mwake.
Moyo ukavuja damu.
Ikachuruzika mpaka kiganjani mwake.
Akalia weee, akajiapiza angekufa akiwa peke yake, kama alivyokuwa amezaliwa leba miaka kadhaa iliyopita. Alibaki na msimamo wake huo kwa miezi michache, lakini kuna siku isiyokuwa na jina, mbele ya macho yake akapita mwanaume mzuri wa sura, moyo wake ukapiga paa! Hakuamini kumuona mwanaume mzuri kama huyo akiishi Tanzania hii.
Alikuwa mrefu.
Maji ya kunde.
Kifua kipana.
Ndevu nyingi kidogo na kichwani alikuwa na upara.
Nasria alibaki akimwangalia mwanaume huyo kwa jinsi alivyokuwa akitembea, alimpenda, moyo wake ukamwambia sasa huyo ndiye alikuwa mwanaume sahihi wa kuwa naye, yaani atengeneze naye familia, wapendane kufa na kuzikana.
Akasahau kiapo chake alichojiwekea, akajiuliza kwani wakati anaapa kulikuwa na mtu aliyemsikia? Hakuna! Alikuwa mahakamani? Hapana! Alishika Msaafu? Hapana! Sasa kwa nini asiamue kujirudi tu?
Kama kulikuwa na watu waliokuwa na kesi walipelekwa mahakamani, wakapewa Biblia ama Msaafu waape na swali la kwanza kwamba walifanya hilo tukio ama la, bado walidanganya kwa kusema hawakufanya, yeye alikuwa nani sasa?
Pale alipokuwa amekaa kibarazani kwao, alitamani kusimama na kumfuata mwanaume huyo. Alikuwa mzuri sana machoni mwake, yaani alijisemea kama kweli wanawake hawakuwa huru kumfuata mwanaume na kumtongoza, basi yeye angekuwa wa kwanza.
Ndiyo!
Angeamua kumfuata tu.
Amwambie kaka nakupenda.
U mzuri sana na nimeshindwa kuvumilia.
Huku akiwa anamwangalia na moyo wake ukiwa na hamu ya kutaka kuzungumza naye, ghafla bin vuu naye akageuza macho na kugongana, tobaaaaa.
Moyo wa Nasria ukapiga paaa! Hakuamini kama angeangaliwa na mwanaume huyo ambaye pia akaamua kutoa tabasamu pana usoni mwake, tabasamu lililomwambia Nasria yeye na majeshi yake waweke silaha chini na kusalimu amri, na kweli wakafanya hivyo.
Alitamani kubaki pale kibarazani alipokaa lakini mwili wake ulitamani kusimama na kumfuata mwanaume huyo, hakuwahi kumuona, hakumjua, hakujua aliitwa nani lakini alitamani sana kumfuata na kuzungumza naye. Huku akiwa hajui nini la kufanya, Mungu akawa upande wake, mwanaume yule akaanza kumfuata yeye.
“Mambo!” alimsalimia baada ya kumfikia, Nasria akapagawa.
“Poa! Karibu!”
“Ahsante sana. Naomba kuuliza,” alimwambia.
“Uliza tu!”
“Namtafuta jamaa mmoja anaitwa Iqram Maduro, aliniambia anaishi huku Magomeni Mapipa, sijui utakuwa unamfahamu?” alimuuliza.
“Oh! I guess!” (Oh! Nadhani) akaingizia Kiingereza safi kidogo, alikwishawahi kusikia mwanamke mzuri akiongea Kiingereza, anakuwa mzuri zaidi, hivyo akafanya kama alivyosikia.
“Anaishi nyumba gani?”
“Wewe nani kwanza?”
“Naitwa Osman!”
“Unaishi wapi?”
“Hapo Kagera Oilcom!”
“Ooh! Sawa. Iqram anaishi nyumba ile pale ya bluu!” alimwambia huku akiinyooshea kidole nyumba hiyo.
“Nashukuru sana!” alisema kijana yule, akaanza kupiga hatua kuelekea mbele kuifuata nyumba ile.
Huku nyuma Nasria alibaki akimwangalia Osman, alitamani kumuita na kumwambia kuna kitu amesahau kumpatia, nacho ni namba ya simu, ampigie na kuzungumza naye.
Huyo Osman alikuwa mzuri.
Ilikuwa vigumu kumuacha tu akiondoka.
Kama kweli alimpenda, basi amwambie tu.
Ghafla akamuona mwanaume huyo akisimama, akageuka na kuanza kurudi nyuma alipokuwa amekaa, akamsogelea huku akiangalia kila upande kama mtu aliyekuwa akiogopa.
“Nimerudi lakini naogopa,” alisema kijana yule.
“Unaogopa nini?”
“Umeolewa?”
“Hapana!”
“Una mchumba?”
“Hapana! Kwani unataka nini?”
“Kitu kimoja tu! Namba yako ya simu, nadhani leo ni siku njema sana kwangu kukutana na msichana mrembo kama wewe. Nimejitahidi sana kuvumilia, niondoke zangu lakini moyo wangu umeniambia weeee, hebu rudi huko,” alisema Osman huku akitoa tabasamu kwa mbali, moyo wa Nasria ukalegea, ukaisha kabisa, yaani ukapagawa kupita kawaida.
“Sina simu!”
“Oh! Huna simu! Kila msichana mrembo hana simu, wale wasichana wabaya wote wana simu. Sawa. Haina shida. Mungu akipenda tutaonana tena,” alisema Osman, hakutaka kubaki, huyo akaanza kuondoka zake.
Nasria sasa akabaki anajuta.
Ndiyo!
Yalikuwa majuto makubwa mno.
Akajiona mjinga.
Tena mama wa wajinga duniani.
Inakuwaje mwanaume umetokea kumpenda, tena umemuona siku hiyo tu akakuomba namba ya simu halafu ukamletea pozi kwa kumwambia huna na wakati unayo? Alihisi labda Osman angembembeleza lakini haikuwa hivyo, akaamua kuondoka zake.
Kichwani mwa Nasria kulimwambia Osman aliamua kufanya hivyo kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura, yeye hakutakiwa kumbembeleza mwanamke bali mwanamke alitakiwa kumbembeleza yeye.
Ndiyo!
Hivi mwanaume kama huyo anapata wapi nafasi ya kukubembeleza mwanamke kama wewe? Kwanza kila siku anafuatiliwa na wanawake wazuri, tena zaidi yako.
Ghafla akamuona mwanaume huyo akirudi tena.
“Basi naomba nikupe yangu,” alimwambia.
“Sawa,” akaitikia haraka haraka.
“Naweza kupata kalamu nikuandikie?”
“Usijali! Ngoja nifuate hapo dukani.”
Ilikuwa ni kama bahati, kama wahenga walisema bahati haiji mara mbili basi kwa Nasria ilikuwa tofauti, mwanaume huyo akarudi na kutaka kumwandikia namba ya simu. Hilo likafanyika, namba ikaandikwa na wawili hao kuanza kuwasiliana.
Wakapendana.
Tena sana.
Sana kabisa ila kilichotokea sasa....
Kuna wahenga wa kizazi kipya wakasema mtaachana tu.
Na kweli wakaachana baada ya miezi sita.
Siku walipoachana Nasria alilia sana, hakuamini macho yake kama kweli aliachwa, alimpenda sana Osman, mwanaume huyo alimuacha na kumwambia sasa alitaka kumuoa mchumba wake, alichoka kumsaliti. Alishangaa mno.
Ilikuwaje amwambie hayo? Inamaana yeye hakuwa mchumba wake? Kumbe alipokuwa naye alikuwa na mwanamke mwingine! Halafu hakumwambia, yaani yalikuwa ni mauamivu yake kwa mara nyingine.
Sasa akajiambia ni muda wa kuwa siriazi na viapo vyake, kama kile cha kwanza alikikana na kujiingiza tena kwenye mahusiano, sasa alitakiwa kuwa siriazi kabisa, kama kuapa, sasa aape kikwelikweli, basi akajiapiza zake huku akiugulia maumivu makali moyoni mwake.
Siku zikaenda mbele, zikakatika tu kama kawaida, hazikumsubiri mtu. Akayapiga teke mapenzi, hakutaka kuwa na mwanaume mwingine yeyote yule.
Mwaka wa kwanza ukapita, wa pili ukaingia, ulipofika wa tatu, wazazi wake wakamuita na kumwambia sasa kuna mwanaume amejitokeza, anataka kumuoa, alikuwa akiishi huko Oman.
“Mwanaume gani?” aliuliza kwa mshtuko.
“Utamuona akija,” aliambiwa.
Alichaguliwa mume, kilikuwa kitu asichokipenda kabisa, hizo zama zilikuwa za zamani bwana, si za siku hizi, siku hizi unaingia vitani mwenyewe, unamtafuta mateka wako, unamteka na kuondoka naye, ila si kama zamani.
Hilo hakulipenda lakini akaona bora aolewe, aondoke zake kwani aliamini sasa angeishi maisha ya peke yake, akiwa na mume wake, ampikie, ampakulie, amtengee chakula, akile na akimaliza, aende chumbani na yeye kuliwa.
Moyo wake ukawa na presha ya kumfahamu mwanaume huyo, alitaka kumuona, aliambiwa alitoka huko Oman, bila shaka alikuwa mzuri, labda zaidi ya Rahim na Osman, hivyo akasubiri kwa hamu kubwa mno.
Siku zikakatika, binti wa watu akazidi kujilinda, hakumwambia mtu kuhusu kuolewa huko mpaka pale ambapo angapata nafasi ya kuonana na mwanaume huyo, aolewe na kuondoka zake huku akiacha heshima nyumbani kwao.
Baada ya mwezi mmoja hatimaye ule ugeni uliokuwa ukisubiriwa ukafika, walikuwa wanaume watatu, wote walikuwa na umri kuanzia miaka hamsini, wakakaribishwa nyumbani hapo na kuanza kuzungumza na wazazi wake, walipomaliza akaitwa na kwenda sebuleni kwa heshima zote.
Aliwaangalia watu hao, alihisi labda mwanaume aliyetakiwa kumuoa aliwapeleka watu wake hapo kumuona yeye kwani wote walikuwa wakubwa kiumri, sasa na wazazi wake.
“Ni mwanamke mzuri sana,” alisema mwanaume mmoja.
Huyo ndiye ambaye alitakiwa kumuoa Nasria, alipoambiwa hivyo, alijisikia huzuni moyoni mwake, hakuamini kama mrembo yeye leo alitakiwa kuolewa na mwanaume aliyekuwa na umri kama wa baba yake.
Alimwangalia, alikuwa mwanaume mzee, ndevu nyingi na alionekana kutisha sana, alikuwa mbaya, kitambi kikubwa na alionekana kupenda sana ngono kutokana na ndevu zake zilivyokaa tu. Nasria alitamani kukataa, awakatalie lakini angeanzia wapi?
Unawezaje kuwakatalia wazazi wako?
Hilo likamuogopesha, hakuwa na jinsi, akakubali kuolewa lakini kamwe asingeuruhusu moyo wake umpende hata kidogo, yaani msichana mzuri kama yeye aolewe na mwanaume mtu mzima kama huyo! Tena aje kumpenda! Kwake lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo.
“Sitoweza kumpenda, sitoweza kuwa naye miaka yote, nitaishi naye kidogo tu na kuomba talaka yangu!” alijisemea huku akimwangalia mwanaume huyo ambaye muda mwingi alikuwa akiifuta simu yake kwa kutumia kitambi chake. Kwa jina aliitwa Hussein Bin Kaifah, moja ya ukoo mkubwa sana huko Oman.
Je, nini kitaendelea?
Kitabu changu cha MZIGO USIO NA ANUANI kitakujia mwezi huu kwa shilingi 10,000 tu.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app