Hakuna wa kumuabudu, hizo zilikuwa enzi hizo. Muhimu ni kuchambua kipi kizuri na kinakidhi hitaji lako maana, "dunia sinia pakua unachoweza" labda kama uniambie una aleji na kila mlo toka kwa wapishi wa maudhui ya habari.
Kama ambavyo, wadhamini ama makampuni yanayotangaza biashara, yenyewe yanachagua ama kwa kushauriwa pia na wataalamu wa masoko wanaweza dhamini segment tu ya kipindi nawe nakushauri waweza sikiliza segment tu kama wapenda au kipindi kizima.
Dunia ya sasa, kwenye biashara hatutafuti upekee maana ni soko huria haupo peke yako bali utofauti maana unaweza fanya zaidi ya mwenzako na si lazma kuwe na utofauti mkubwa, kama ambavyo kinachofanya wenye iPhone waringe ni logo ya apple kabla ya mengine.
Tukitafuta original idea hakuna, hata Fiesta ambayo ilibadilishwa jina tu kutoka Summer Jam ya kibongo ni idea iliyotoka Marekani enzi hizo music festival iliyokuwa inabamba ni Summer Jam.