Media promo Vs. Real Hip Hop Emcees

Media promo Vs. Real Hip Hop Emcees

Kaveli

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
5,467
Reaction score
9,007
Huwa sielewi kuna nini kwenye music industry ya Bongo as regards to Hip-Hop. Kwanini media inawabania sana promo maemcee wanaofanya hip hop ya ukweli???!! mfano.. jamii kubwa inafahamu zaidi uwepo wa NEY WA MITEGO (ambae anajiita mwanahip-hop) kuliko uwepo wa BONTA (ambae kwa mtazamo wangu ni mwanahip hop wa ukweli). Mfano..

jamii inafahamu zaidi uwepo wa CHID BENZ (ambae anajiita mwanahip hop) kuliko uwepo wa SALU-T (ambae kwa mtazamo wangu ni mwanahip hop wa ukweli). Kuna wasanii wanafanya conscious hip hop lakini bado kabisa media haiwapi support au kuwaweka katika nafasi wanayostahili kuwepo. Mfano sikiliza kazi za Bonta, jamaa anafanya hip hop ya ukweli sana lakini bado legacy yake kwenye jamii ipo too low!!!!

JE kuna vitu fyongo vinafanyika kwenye music industry (hasa Media) kuhusu hip hop emcees' legacy? au jamii yenyewe ndo bado haitoi mwitikio chanya towards real emcees wa hip hop?

Kwa mtazamo wangu... nadhani Lack of media promo, pamoja na mambo mengine, imesababisha kwa kiasi kikubwa sana wakongwe real emcees wengi wa hip hip aidha kupunguza kasi au ku-quit game mazima. Mfano... ZAVARA, HASHIM DOGO 'Mwanaharamu', SALU-T, n.k. magwiji hawa leo hii hip-hop community inamiss sana kazi zao.

Karibuni wadau kwa michango yenu katika hili.
 
rushwa.

wasanii wengi wanaojiita wana hip hop ilhali they no northing about it wanatoa rushwa kwa mapresenter ili wapate air time

uelewa mdogo wa mapresenter kuhusu hiphop,

presenters wengi hawajui nini maana ya hiphop,hawajui kwamba hiphop ina nguzo,hawaijui misingi ya hiphop..hatimaye wanajikuta wakipiga baadhi ya nyimbo na kuziita hiphop songs wakati sio hiphop songs,,,
inauma sana kusikia presenter anatambulisha wimbo wa ney wa mitego afu anasema '''huyo ndo msanii aliyenyakua tuzo ya best hiphop artist kwenye KTMA,,,,,

poor management upande wa hawa wasanii wanaofanya real hiphop,,

ebu watazame tamaduni music, mfano nikk.songa..one..Nash..stereo n.k,,ebu mtazame salu T,,ebu mtazame j moe,solo thang,,,hawa jamaa wanakosa management sahihi.


N.B

wasanii hawa hawatakiwi kujiita wana hiphop,

ney wa mitego,
county boy,
god zila,
madee,
 
Mkuu Moon, nakubaliana na wewe kabisa aisee. RUSHWA kwa mapresenter na POOR MANAGEMENT kwa artists wenyewe ndizo sababu kubwa kwa hiphop artists wa kweli kushindwa kukubalika kwenye jamii. mapresenter wanaangalia pesa ili wakupe promo, na sio contents za nyimbo. ni shidaaaaa
 
Nadhani ukitoa media za Bongo kukosa watu wa muziki haswa kama zamani pia tukubali nyakati zimebadilika na watu wamebadilika sana pia.Watu wengi wa muziki wameacha kufanya kazi za muziki hasa upande wa media na kufanya hata vijana wanaofanya kazi kwenye media hivi sasa kuwa na wrong role models.

Watangazaji wenye upeo level za ML Chriss (Clouds) , Sebastian Maganga (Clouds) , Mike Mhagama ,DJ John Dilinga (amerudi radio one lakini anapiga old skool tu Jmosi) , DJ Bonny Love , DJ Boggie Master, SOS B n.k wote wameacha UDJ au utangazaji wa vipindi vya burudani au kuacha kabisa kutangaza kipindi wakiwa wanahitajika kutengeneza generation mpya yenye uwezo mkubwa na upeo wa muziki.

Watangazaji wa sasa wanawaiga sana B12 na Adam hasa uongeaji huku hakuna challenge ya maana kutoka kwao ya kuwapa home work ya kutosha muigaji.Hebu assume leo "mjukuu wa ambua" anataka kumuiga Masoud Masoud! angetakiwa sio kuiga sauti tu bali na namna ya kuchambua muziki tena wa mbele si bongo tu.

Ndio maana wasanii bora zama hizi hawasikiki wanasikika walamba midomo tu sababu hata watu wa media wamejaa walamba midomo tu!!
 
Mkuu Moon, nakubaliana na wewe kabisa aisee. RUSHWA kwa mapresenter na POOR MANAGEMENT kwa artists wenyewe ndizo sababu kubwa kwa hiphop artists wa kweli kushindwa kukubalika kwenye jamii. mapresenter wanaangalia pesa ili wakupe promo, na sio contents za nyimbo. ni shidaaaaa

Hivi unafikiri hata hawa wanaotamba sasa wana GOOD MANAGEMENT kuliko wasiotamba? labda tungeelewa maana ya GOOD MANAGEMENT ndio tungejua sanaa ya Bongo hakuna GOOD MANAGEMENT.

Muda huongea!
 
Hivi unafikiri hata hawa wanaotamba sasa wana GOOD MANAGEMENT kuliko wasiotamba? labda tungeelewa maana ya GOOD MANAGEMENT ndio tungejua sanaa ya Bongo hakuna GOOD MANAGEMENT.

Muda huongea!
mkuu hao wanaotamba ni kwasababu,,

1,wanatoa rushwa.
2,kujuana kwingi.

sio kwamba wana management nzuri
 
kitu unachokiongea sio kwa tz tu ni dunia nzima mf huwezi kuona video za watu conscious mtv au bet watu km.talib kweli mos.def . immortal technique nk utawaona wakina lil wayne drake future nk medias ni cooparate companiz ambazo nikm zina ajenda moja yakupromote gayizm stupidness na destruction of morals among mass. wakipiga nyimbo za watu conscious wanaogopa kwamba watu watakua empowered mentally.

spiritual nk. media nyingi zina ajenda ya shetani. kwa hiyo km neno linavyosema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. sisi tulioelimika na kujitambua tunapaswa kuwapa support ma emcee conscious km kununua kazi zao mixtape or album na franchise zao nyingine. support tamaduni weusi nk
 
Mziki umebadilika Hip hop ya miaka 90 sio kama sasa. Mziki wenye kuburudisha ndo unapendwa zaidi kuliko wa mziki wenye messages.(miziki inayofaa kupigwa clubs ndo inapendwa na watu wengi) kitu ambacho mamc's wengi hawafanyi wao ni concious tu.

Mamc's wa tz wajaribu kutengenza na miziki ya kuchezeka(club bangs) lazima nyimbo zao zitapata airtime .Siku hizi afro pop ndo ina kick. Ona kina Ommy dimpoz,diamond n.k wanavyokick kimataifa.Hits kama prof jay (kipi sijasikia) itavuma hapa bongo sio international japo itapata airtime bongo kwa ajili ya message yake.
 
Namlaumu profesa J a.k.a nigger J kwa kubadilsha iliyojuwa hip hop na kuja na kitu kinachojulikana leo hii kama bongo flavour.

Chemsha bongo ndio imetuharibia muelekeo...! Kwa wafwatiliaji mtakuwa mmenisoma!
 
Namlaumu profesa J a.k.a nigger J kwa kubadilsha iliyojuwa hip hop na kuja na kitu kinachojulikana leo hii kama bongo flavour.

Chemsha bongo ndio imetuharibia muelekeo...! Kwa wafwatiliaji mtakuwa mmenisoma!

Umenikumbusha jambo hapa, Chemsha Bongo ilimfanya kila mtu aone kuwa hata yeye anaweza kurap...
 
SAIGON wetu wa bongo (nasema wa bongo kwasababu kuna Saigon US pia ) alijitahidi sana kurudisha heshima ya Hip Hop kupitia Kipindi chake cha HIP HOP BASE kilichokua kikirushwa EATV niliweza kuwasikia maemcee kama BALOZI DOLA, DJ YUSUPH, MANSU LI, SALU T, KIKOSI CHA MIZINGA, WATENGWA, NAKO 2 NAKO (enzi zile kabla hawajaanza kuimba nyimbo za mchakamchaka na weusi )

Kipindi kilikua kizuri lakini nae sijui kaishia wapi? Kuna Ujamaa Hip Hop Darasa ya Fid na Cheusi Dawa TV na FidStyleFriday navyo naona vimesizi kwa sasa... matokeo yake kizazi cha sasa ndio wanakua wakijua ukizungumzia Hip Hop unawazungumzia weusi (waimba nyimbo za mchakamchaka ).ney wa mitego.. roma (muimba taarabu? na mafake emcee kama hao...
 
Mi nadhani kama mdau alivyosema hapo juu, mziki umebadilika sana. Si tu kwa Tz bali hata kwa waasisi wenyewe wa hip hop. Kwa kiasi kikubwa real hip hop ni kama inaelekea kufa na hata ukiangalia kwa Marekani ambapo mziki huu ulianzia, wasanii wengi waliovuma kama kina Mystical, Busta Rymes, DrDre, Eminem, Xzibit, Snoop Dogg, Lil Kim, Da Brat, DMX, Ja Rule na wengine wengi..

either wameacha kabisa muziki na kujishughulisha na ishu nyingine, AU wanafanya muziki kwa kushirikiana na wanamziki WANAOIMBA na kuweka vionjo vingine.

Tumeona Snoop akishirikiana na R.Kelly, Ja rule na kina Jenifer Lopez/Ashanti, Busta Rymes na Mariah Carey na vitu kama hivyo. Ikumbukwe pia kwamba muziki ni biashara kama biashara nyingine kwahiyo kuna swala la kulisoma soko na kuangalia walaji wanataka nini na sio tu kung'ang'ania kubaki stagnant. Watu wanataka vitu soft soft siku hizi.. na vionjo.. na mziki unaochezeka. n.k. Huwezi kulazimisha soko lipende kitu fulani hata kama kimepitwa na wakati!
 
Asante kwa mada nzuri sana wakuu shida kubwa hapa nchini ni hawa clouse.. kiukweli hawa jamaa wanamalengo yao katika mziki na wamefanikiwa kubadili mziki uwe watakavyo.. kwa mfano mtu pekee pala clouse anayependa kupiga miziki ya hiphop ya maana ni mchonvu basi akina b 12 na madj wote ni watu wa bongofleva.

lakini pia hata dunia nzima mziki umebadilika.. unaweza nambia mtu kama common amepotelea wapi.. wanaotamba akina jay z wanaimba hiphop ya ajabuajabu lakini wanakubalika sana,lakini akina common wanapotea.. sasa hivi ata 50 cent ana imbaimba tu..

ndio maana ata tanzania, akina Bonta,nash mc,nikk mbishi,one the incredible Wanapotea lakini akina madee,nay wa mitego,weusi n.k wanavuma wakati wanaimba utumbo..
 
Ukitaka kujua sababu sikiliza/angalia pini la nikki wa pili kuboom kuba ka- portrait vitu vinavyoua mziki wa hiphop wale watumwa waliovaa mabango.
 
ukweli ni kwamba kuna baadhi ya wadau(watu wa kati) wamehodhi hii music industry na kujionakama yakwao. hao hawata kuona mamcee wa kwel wakina kwenye gemu, hivyo bas huwa wanaanyakia linalowezekana kuwakwamisha. shaihi upo kaika hili.
 
Mziki umebadilika Hip hop ya miaka 90 sio kama sasa.
Mziki wenye kuburudisha ndo unapendwa zaidi kuliko wa mziki wenye messages.(miziki inayofaa kupigwa clubs ndo inapendwa na watu wengi) kitu ambacho mamc's wengi hawafanyi wao ni concious tu.
Mamc's wa tz wajaribu kutengenza na miziki ya kuchezeka(club bangs) lazima nyimbo zao zitapata airtime .Siku hizi afro pop ndo ina kick. Ona kina Ommy dimpoz,diamond n.k wanavyokick kimataifa.Hits kama prof jay (kipi sijasikia) itavuma hapa bongo sio international japo itapata airtime bongo kwa ajili ya message yake.

unajua hata binadam kuna warefu wafupi weusi weupe nk ndo ivo iov kwa muziki unapaswa kuwa diverse....swala sio kupiga conscious tu bali ni kubalance aina za muziki sababu hata mashabiki tuko tofauti tofauti...unaweza saa nzima radio unashangaa inapiga mziki wa aina moja(uo uusemao) wanasound the same midundo inafanana theme zinafanana ....hiyo inapunguza hata creativity na ndo mana wengi wanaingia kwenye mziki wakizani ni kitu rahisi tu ...si atasound tu km diamond ama davido atatoa hela ya promo ndo ivo....
 
kitu unachokiongea sio kwa tz tu ni dunia nzima mf huwezi kuona video za watu conscious mtv au bet watu km.talib kweli mos.def . immortal technique nk utawaona wakina lil wayne drake future nk medias ni cooparate companiz ambazo nikm zina ajenda moja yakupromote gayizm stupidness na destruction of morals among mass. wakipiga nyimbo za watu conscious wanaogopa kwamba watu watakua empowered mentally. spiritual nk. media nyingi zina ajenda ya shetani. kwa hiyo km neno linavyosema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. sisi tulioelimika na kujitambua tunapaswa kuwapa support ma emcee conscious km kununua kazi zao mixtape or album na franchise zao nyingine. support tamaduni weusi nk

kiongozi umeongea sense sana. naunga mkono hoja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom