Media Council vs Radio 104.4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Media Council vs Radio 104.4

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by luck, Jun 3, 2012.

 1. luck

  luck JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 771
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  Leo asubuhi nilikuwa nasikiliza habari kwa njia ya redio nikajikuta nimenasa kwenye radio ya fm 104.4 (sifaham jina la kituo cha redio).Wahusika walikuwa wakizungumzia masuala ya vurugu zilizotokea unguja ambazo kwa taarifa mbalimbali zinadai vurugu hizo zilianzishwa na kundi la uamsho.

  Mtangazaji alikuwa akiongea na mgeni ambaye alikuwa anaongea kutetea msimamo wa kundi la uamsho na kutoa lawama kwa wale wanaolinyooshea kidole kundi hili la uamsho.


  Kwangu mimi niliona kinachofanywa na wahusika hawa ni kinyume na matamko yaliyotolewa na marais wetu JK na Sheni na hakina tofauti na kuchochea vurugu nchini kwa sababu naamini redio hii itakuwa inasikilizwa na watu wengi.

  Swali langu ni je hivi ni kazi ya nani kuviadabisha vyombo vya habari vinavyokiuka misingi ya uanahabari au mambo yanaenda hivyohivyo bora liende? Hii ni hatari kubwa kwa sababu vyombo vya habari usikilizwa na kuaminiwa na umma mkubwa wa wananchi. Vyombo hivi vinapaswa kuwa na udhibiti wa aina fulani vinginenyo kwa maoni yangu itakuwa ni suala la muda tu kabla nchi haijaingia kwenye matatizo yanatokana na upotoshaji na uchochezi unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari.

  Nafahamu kuna baraza la habari. Hivi ni nini kazi ya chombo hiki? Kimtazamo nafikiri moja ya kazi yao ni kudhibiti watu kama hawa
   
 2. Masulupwete

  Masulupwete JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hao ni radio Imaan wako morogoro

  Mkuu unawashangaa hao? mbona kuna mahubiri mengi tu ya mwelekeo huohuo yanafanywa maeneo ya wazi kabisa na mengine huko vichochoroni lakini hakuna anayekemea, japo serikali ya mitaa?!
   
Loading...