ThnkingAloud
JF-Expert Member
- Sep 13, 2017
- 598
- 609
Kwa bahati nzuri leo nimesikiliza kipindi cha Redio Tumaini cha Dukuduku. Nimependa dukuduku kuhusu watangazaji wa Redio Tumaini. Watangazaji wameifanya Redio igeuke kituko kama siyo Redio ya Kanisa Katoliki. Hata mkurugenzi wa Redio Tumaini hana habari kinachoendelea. Pamoja na kuchangisha michango ya kila mara kupitia makanisani kwa ajili ya kueneza na kuendeleza injili kupitia vyombo vya habari, watangazaji wameigeuza kijiwe chao rasmi. Ninakubaliana na mchango wa mama mmoja aliyechangia kuhusu hilo ni kweli Redio Tumaini mnatuboa mmegeuka kituko kama redio za mipasho na umbea. Badilikeni.