Mechi ya Mbao na Simba fainali bora FIFA U20 world final.

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Wakuu, nimegundua kumbe upeo wetu ni mdogo mno. Pana fainali za FIFA U20 huko Korea Kusini, sawa na fainali za timu kubwa za mataifa, lakini hakuna hapa nchini anaefuatilia hasa media zetu. Ukulinganisha ubora wa michuano hii ya FIFA walahi fainali ya Simba na Mbao huko Dodoma ilikuwa so chochote zaidi ya unazi tu. Tubadilike.
 
Yanga FC na mbao FC.
Mechi za mwisho zilikuwaje ?.
Zilizidi hizo fainali za
under 20 ?
Kwa uchezaji
Naskia mliishia kumpiga refa na wachezaji wamefungiwa mechi 5.
Mlicheza vizuri sana naskia
 
Upeo wako ndio mdogo TV 1 kila siku wanatoa overview ya mashindano hayo na wafuatiliaji tupo wengi tu sasa ww huo utafiti wako kuwa hakuna media inayofuatilia wala watu unautoa wapi?..na wala usitupangie eti tusitazame mnyama wa tanzania eti tukawatazame wakorea for what?
 
Ilikuwa "classical fainal" Hayo ni maneno ya Mpenja.Yaani ulichezwa mpira wa kitabuni. Sasa wewe mtoa hoja huko korea hatuna under20 wa Tanzania tukamtazame nani?
 
Vipi Tanzania under 20 ndo ilikuwa inacheza fainali huko Korea kusini?
Mkuu unachekesha. Hiyo timu yetu ya U20 IPO wapi? Timu hizi huandaliwa kimagumashi tu muda wa mashindano ukufika tofauti na timu ya soka ya wakubwa (Taifa Stars).
 
Yanga FC na mbao FC.
Mechi za mwisho zilikuwaje ?.
Zilizidi hizo fainali za
under 20 ?
Kwa uchezaji
Naskia mliishia kumpiga refa na wachezaji wamefungiwa mechi 5.
Mlicheza vizuri sana naskia
Hata hao hakuna chochote hata mechi za ligi baina ya timu za Simba na Yanga ndani ya dakika 90 so lolote ila sikiliza/soma kwenye vyombo vya habari, loh.
 
hivi yanga kwanini inawauma lakini? mwambieni hata Malinzi kuwa simba imeshinda mbili moja dhidi ya mbao iliyowapiga yanga mara mbili
 
Wakuu, nimegundua kumbe upeo wetu ni mdogo mno. Pana fainali za FIFA U20 huko Korea Kusini, sawa na fainali za timu kubwa za mataifa, lakini hakuna hapa nchini anaefuatilia hasa media zetu. Ukulinganisha ubora wa michuano hii ya FIFA walahi fainali ya Simba na Mbao huko Dodoma ilikuwa so chochote zaidi ya unazi tu. Tubadilike.
Vp ile penati ya Simba?
 
Upeo wako ndio mdogo TV 1 kila siku wanatoa overview ya mashindano hayo na wafuatiliaji tupo wengi tu sasa ww huo utafiti wako kuwa hakuna media inayofuatilia wala watu unautoa wapi?..na wala usitupangie eti tusitazame mnyama wa tanzania eti tukawatazame wakorea for what?
Sio wanatoa overview TV 1 walikua wanaonyesha kabisa,kwa bahati mbaya game nyingi kwa mda wa hapa kwetu ilikua ni asubuhi...!
 
Hata hivyo mleta mada ana point,haiwezekani wale waandishi wanaojiona nguli wa michezo,mpka mashindano yanaisha jawajaandika sana,kiukweli bila kuwapa taarifa za kuwahamasisha hawa wadogo zetu tutaishia kuwa wasindikizaji tu!!
 
Upeo wako ndio mdogo TV 1 kila siku wanatoa overview ya mashindano hayo na wafuatiliaji tupo wengi tu sasa ww huo utafiti wako kuwa hakuna media inayofuatilia wala watu unautoa wapi?..na wala usitupangie eti tusitazame mnyama wa tanzania eti tukawatazame wakorea for what?
Mkuu, hawa TV 1 mie ndo wananiwezesha kuyaona hayo mashindani. Nadhani hujanielewa lengo langu ni nini. Yaani kwenye vipindi vya michezo vya radio na TV nyingi tu hapa husikii habari za mashindano hayo tens kama Clouds FM ambao hujifanya wanaujuzi wa kuchambua mambo ya michezo hasa soka ni ZERO. Jana tu ndo nimewasikia kwa sekunde kama mbili hivo wakitihabarisha kilichotokea huko. Kwenye magazeti hakuna. Ikiwa TV 1 na Star times wanaonesha mechi hizi kubwa za soka inakuwaje media nyingi bado vinajikita na masuala ya EPL tuuu? Hapo ndo tatizo langu mkuu na so vinginevo.
 
Ilikuwa "classical fainal" Hayo ni maneno ya Mpenja.Yaani ulichezwa mpira wa kitabuni. Sasa wewe mtoa hoja huko korea hatuna under20 wa Tanzania tukamtazame nani?
Mkuu, kwani huko England tuna klabu yoyote inayoshiriki ligi yoyote pale? Kama tunashindwa kufuatilia mechi kubwa kama za FIFA 'ETI' hatushiriki kila tunajikita EPL wakati hakuna timu yetu huko basi sie ni binadamu wa ajabu sana hapa Ulimwenguni.
 
hivi yanga kwanini inawauma lakini? mwambieni hata Malinzi kuwa simba imeshinda mbili moja dhidi ya mbao iliyowapiga yanga mara mbili
Mkuu, mie kwa sasa nimepozi tu kwani Azam FC walinivutia walipoanza lakini nao sasa ni kama Yanga na Simba. Majanga tu.
 
Sio wanatoa overview TV 1 walikua wanaonyesha kabisa,kwa bahati mbaya game nyingi kwa mda wa hapa kwetu ilikua ni asubuhi...!
Sio asubuhi tu mkuu, pana mechi mpaka mchana saa nane. Takriban mechi tatu kwa siku hivi sasa TV 1 wanaonesha.
 
Back
Top Bottom