KIUNGOMCHEZESHAJI
Senior Member
- Oct 4, 2013
- 120
- 255
Jamani mimi kuna kitu sikielewi, wataalam wa mambo ma mahusiano na psychology mnisaidie.
Mimi niko mikoani, ila nimekaa Dar kwa muda takriban miaka 9. Miaka miwili iliyopita nilifahamiana na dada mmoja, mzuri sana. Tulifahamiana vizuri mpaka akanishawishi nifike kwao nipafahamu. Anauza stationery ambapo kuna internet cafe. Basi ikawa nikija tu kutoka mikoani akijua lazima anishawishi kwa gharama yoyote ile nifike pale, tupige story.
Wakati mwingine hataki niondoke pale. Kwenye simu ananitumia sms nzuri sana na ni mpole na mkarimu sana. Ilifika hatua nikashindwa kujizuia, mwanaume nikawa nimempenda na hisia zangu zote aliziteka. Nilipomweleza, akasema haiwezekani kwa sababu mimi nimeoa nina mke. Akaniambia haijalishi mimi nina tatizo kiasi gani kwenye ndoa yangu maadam nina mke, hata nisipopata huduma miezi sita, yeye hawezi kunisaidia.
Baada ya kusumbuana muda mrefu, nikaamua kumuacha, wakati mwingine tunagombana nakata mawasiliano ili angalau nimsahau. Niliamua kumblock kwenye simu na kila aina ya social media. Lengo langu ilikuwa tu ili nisahau nisiendelee kuumia kwa ajili yake.
Akaanza kunitafuta kwa namba zingine, tukiongea mpaka ananibembeleza, wakati mwingine analia. Ananiambia ananipenda lakini isiwe mahusiano. Kuna wakati alinikubalia kwa masharti magumu sana ambayo hayatekelezeki katika uhalisia.
Kiufupi nimeshindwa kuelewa kwa nini ananisumbua kiasi hiki? Mimi sitaki anitafute nikimwambia asinitafute anasema hawezi kuacha kunitafuta, na hawezi kuacha kunitumia sms. Ni zaidi ya mwaka sasa tunasumbuana. Natamani sana nijue kilicho akilini mwake kinachomfanya awe ananihitaji sana wakati suala la mapenzi halipo.