Mechi hakuna lakini ameniganda kama ruba

unatembea na nyota yake ndio maana anakungangania,tafuta kanisa la kiroho uombewe
 
Jamani mimi kuna kitu sikielewi, wataalam wa mambo ma mahusiano na psychology mnisaidie.
Mimi niko mikoani, ila nimekaa Dar kwa muda takriban miaka 9.
Miaka miwili iliyopita nilifahamiana na dada mmoja, mzuri sana. Tulifahamiana vizuri mpaka akanishawishi nifike kwao nipafahamu. Anauza stationary ambapo kuna internet cafe. Basi ikawa nikija tu kutoka mikoani akijua lazima anishawishi kwa gharama yoyote ile nifike pale, tupige story. Wakati mwingine hataki niondoke pale. Kwenye simu ananitumia sms nzuri sana na ni mpole na mkarimu sana. Ilifika hatua nikashindwa kujizuia, mwanaume nikawa nimempenda na hisia zangu zote aliziteka. Nilipomweleza, akasema haiwezekani kwa sababu mimi nimeoa nina mke. Akaniambia haijalishi mimi nina tatizo kiasi gani kwenye ndoa yangu maadam nina mke, hata nisipopata huduma miezi sita, yeye hawezi kunisaidia.

Baada ya kusumbuana muda mrefu, nikaamua kumuacha, wakati mwingine tunagombana nakata mawasiliano ili angalau nimsahau. Niliamua kumblock kwenye simu na kila aina ya social media. Lengo langu ilikuwa tuu ili nisahau nisiendelee kuumia kwa ajili yake. Akaanza kunitafuta kwa namba zingine, tukiongea mpaka ananibembeleza, wakati mwingine analia. Ananiambia ananipenda lakini isiwe mahusiano. Kuna wakati alinikubalia kwa masharti magumu sana ambayo hayatekelezeki katika uhalisia.

Kiufupi nimeshindwa kuelewa kwa nini ananisumbua kiasi hiki? Mimi sitaki anitafute nikimwambia asinitafute anasema hawezi kuacha kunitafuta, na hawezi kuacha kunitumia sms. Ni zaidi ya mwaka sasa tunasumbuana. Natamani sana nijue kilicho akilini mwake kinachomfanya awe ananihitaji sana wakati suala la mapenzi halipo.

Sikiliza mjomba emu siku 1 mtanie mwambie mimi nimegombana na mke wangu nishamuacha na simtaki tena nataka wewe ndio uchukue nafasi yake au kama pia hutaki basi mimi naoa mke mwengine.

Yawezekana shida ni mkeo ila yeye anaona shida kukwambia muachane na mke wako antaka utaamuli wewe mwenyeo.
 
Exactly

Huu ndiyo ushauri.Hizo za wengine zote pumba tu
 
Khaa!! Chief, Kwanza mke wako anakushauri nini? 😎
Hii comment imeendana na jina lako 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Jamani mimi kuna kitu sikielewi, wataalam wa mambo ma mahusiano na psychology mnisaidie.
Mimi niko mikoani, ila nimekaa Dar kwa muda takriban miaka 9.
Miaka miwili iliyopita nilifahamiana na dada mmoja, mzuri sana. Tulifahamiana vizuri mpaka akanishawishi nifike kwao nipafahamu. Anauza stationary ambapo kuna internet cafe. Basi ikawa nikija tu kutoka mikoani akijua lazima anishawishi kwa gharama yoyote ile nifike pale, tupige story. Wakati mwingine hataki niondoke pale. Kwenye simu ananitumia sms nzuri sana na ni mpole na mkarimu sana. Ilifika hatua nikashindwa kujizuia, mwanaume nikawa nimempenda na hisia zangu zote aliziteka. Nilipomweleza, akasema haiwezekani kwa sababu mimi nimeoa nina mke. Akaniambia haijalishi mimi nina tatizo kiasi gani kwenye ndoa yangu maadam nina mke, hata nisipopata huduma miezi sita, yeye hawezi kunisaidia.

Baada ya kusumbuana muda mrefu, nikaamua kumuacha, wakati mwingine tunagombana nakata mawasiliano ili angalau nimsahau. Niliamua kumblock kwenye simu na kila aina ya social media. Lengo langu ilikuwa tuu ili nisahau nisiendelee kuumia kwa ajili yake. Akaanza kunitafuta kwa namba zingine, tukiongea mpaka ananibembeleza, wakati mwingine analia. Ananiambia ananipenda lakini isiwe mahusiano. Kuna wakati alinikubalia kwa masharti magumu sana ambayo hayatekelezeki katika uhalisia.

Kiufupi nimeshindwa kuelewa kwa nini ananisumbua kiasi hiki? Mimi sitaki anitafute nikimwambia asinitafute anasema hawezi kuacha kunitafuta, na hawezi kuacha kunitumia sms. Ni zaidi ya mwaka sasa tunasumbuana. Natamani sana nijue kilicho akilini mwake kinachomfanya awe ananihitaji sana wakati suala la mapenzi halipo.

Aisee kuna wanawake ni kimeo.
 
Naomba namba yake mkuu. Unatakiwa uwempole na uwe mnafik kwa mbaali
 
Mweleze mkeo halafu akiafiki wawe marafiki na ndipo huo urafiki utakuwa na maana.
Je ungemruhusu mkeo awe na rafiki swahiba wa kiume? Utaamini kuwa hakamati mzigo?
Urafiki wa chui na mbuzi hata wakati chui kashiba ni wa mashaka sana bado
 
Mshahara wa dhambi ni mauti hivyo jiangamize na upoteee duniani na mbinguni pia wakutoe baru
 
Hiyo ni kawaida kwa manzi wengi wewe fanya kila njia umchape nao!
 
Acha ujinga wewe...kama unataka kumgegeda na yeye hataki mtupilie mbali. Am sure u already have too many frends bana....mpotezee tuu.
 
Tangu lini kuna urafiki wa mwanamke na mwanaume asiye ndugu bila kugegedana?mwana kondoo aliyenona hawezi ishi na fisi mwenye njaa.
 
Back
Top Bottom