Mdude aeleza kilichomfanya asihamie Kenya

Kifaurongo

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2010
Posts
4,287
Reaction score
2,437
Nimestushwa na taarifa hii ya Mdude aliyotoa kwa muandishi wa Gazeti la Mwananchi. Kuwa kabla ya tukio hili kulikuwa na mipango ilioratibiwa na Bonface Jacob na John Heche ya kumkimbizia Kenya. Kama si Mdude kughaili baada ya kufika Arusha, nahakika mpango huu ungefanikiwa tungetangaziwa kupotea kwa Kamanda mwingine wa chama hicho.

=====

Mdude aeleza kilichomfanya asihamie Kenya

Mbeya/Dar. Mdude Nyagali, maarufu ‘Mdude Chadema’, amesema kutokana na misukosuko ambayo amekuwa akiipata alifikia hatua ya kutaka kuhama nchi ili akaishi uhamishoni, lakini alighaili akiwa njiani.
Mdude kwa sasa amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kuokotwa na madereva bodaboda kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Inyala wilayani Mbeya.

Jumamosi ya Mei 4, Mdude, mkazi wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe alidaiwa kutekwa na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake mjini Vwawa, kisha akapelekwa kusikojulikana hadi alipokutwa usiku wa Jumatano iliyopita eneo la Inyala akiwa hoi kutokana na kipigo alichokipata.

Akizungumza na Mwananchi hospitalini hapo, Mdude alisema kutokana na misukosuko iliyokuwa inamkabili kabla ya tukio hilo aliomba msaada kwa viongozi wa Chadema na baadaye akazungumza na meya wa Ubungo, Boniface Jacob na mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche ambao walimfanyia mpango kwenda kuishi nchini Kenya kabla ya kubadilisha uamuzi wake.

“Ni sahihi kabisa, kwani kuna kipindi misukosuko ilizidi, mara kesi mahakamani. Baadaye nikasema nitafute hifadhi nchi nyingine. Ndio wakawa wamenitafutia hifadhi Kenya, wakanifanyia michakato mingine yote. Na nikasafiri hadi Arusha kwa ajili ya kuelekea nchini Kenya,” alisema Mdude.

Alisema alipofika Arusha, nafsi yake ilimsuta, akafikiria kwamba akiondoka nchini watu wengi watakata tamaa, hivyo ni bora arudi kwa sababu Tanzania ni nchi yake.

Alisema uamuzi wake huo uliambatana na kumwachia Mungu kila jambo maishani mwake, na kama ana makosa basi atahukumiwa kwa makosa yake na iwapo yuko sahihi Muumba wake atamsimamia.

Akizungumzia uamuzi wa Mdude kutaka kutimkia uhamishoni, Meya Jacob alisema, “binafsi amenifundisha ujasiri, kuna wakati alikuwa anatumiwa meseji za vitisho na watu wasiojulikana, ilifikia hatua kama chama tukaona atafutiwe makazi nje ya nchi lakini yeye alikataa akasema ataendelea kuwepo hapa na kupambana hadi mwisho wake.”

Jacob, ambaye diwani wa Ubungo (Chadema), alisema kwa muda aliofahamiana na Mdude amemfundisha ujasiri na kutokata tamaa wala kukubali kuyumbishwa kifikra.

“Ni mpiganaji asiyekata tamaa, anasimama na kuonyesha wazi kupigania anachokiamini, haya matatizo si mara ya kwanza kumkuta na amekuwa akikutana na vitisho mara kadhaa, lakini hajawahi kuwa na hofu.”
Alisema umaarufu wa mwanachama huyo wa Chadema ambaye pia ni kiongozi wa mafunzo Kanda ya Nyasa umekuwa mkubwa kutokana na mwenendo wake wa kuikosoa Serikali kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Naye mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alimwelezea Mdude kuwa ni kijana mzalendo mwenye kusimamia kile anachokiamini na kutekwa kwake kunahusishwa na mwenendo wake wa ukosaji.

Alieleza kuwa mwanachama wao huyo amekuwa akiikosa Serikali kwa sababu anaamini ni nafasi yake ya kikatiba kama Mtanzania na vilevile ni kiongozi wa chama cha upinzani ambacho kina jukumu la kutoa mawazo mbadala ikiwemo kukosoa.

Akizungumzia uchunguzi wa polisi, kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando alisema wanaendelea na uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa Mdude, lakini wanapata ugumu kwa kuwa mhusika mwenyewe hasemi ukweli.

“Daah! Unauliza maswali magumu... Mdude mwenyewe hasemi waliomteka akina nani na kama yeye mwenyewe anasema hawajui, unafikiri sisi tutajua kweli? Anapaswa kusema gari lilikuwa na namba fulani, walioniteka walikuwa wanasema hiki, hiki na hiki, ili na sisi tuanzie hapo,” alisema kamanda Kyando.
“Tukimuuliza walipokuwa wanakupiga walikuwa wanakuambia nini? Hasemi. Sasa hapo tunafanyaje? Kimsingi majibu rahisi ni kwamba bado uchunguzi unaendelea, ukikamilika tutawaambia.”

Alisema, “Mdude hayupo wazi kwani lazima wanapokupiga wanasema kwa nini uliniibia au kwa nini ulifanya hivi au kwa nini umefanya hivi.”
 
Naona sababu kwanini mungu hajamuua shetani tuishi kwa amani... Maana akisema amuue shetani tutakufa wengi sana ambao tunajivika unafiki
 
Naamini wengi tumeisoma, ila ni kwamba walitaka kumsafirisha kwa sababu ya kutumiwa jumbe za kuhatarisha maisha yake..
Na kama wangekuwa wanamficha wasingemtumia askari ili amsaidie kumvisha boda..
Soma na uelewe sio kupotosha hapa
 
Mdude kusema hata anakosoa yaani mtu huoni pointi ni ujinga mtupu mfano anasema mnanunua ndege wakati hospitali hazina dawa Wala haziwezi tibu hate mende!!! Yeye Sasa hivi anatibiwa hospital hizo hizo alizosema hazina uwezo wa kutibu hata mende!!! Kiukweli upinzani wa Tanzania Bado Sana tu kihoja kwa Tanzania mtukanaji serikali na viongozi ndio huitwa mkosoa serikali very sad!!! Watu Kama Mtikila ndio walikuwa wakosoa serikali siji sahau Mtikila alivyosababisha passport kufutwa kutotumika kwenda Zanzibar kwa watanzania..Enzi hizo kwenda Zanzibar ilikuwa unaenda kwa passport Kama unaenda Ulaya.Vyama vingi vilipoanza ilitakiwa chama kiwe na wanachama Tanzania bara na Zanzibar ili kisajiliwe.Mtikila akagoma kusajili wanachama wa chama chake kutoka Zanzibar na akajenga hoja kuwa Zanzibar Ni nchi Tena unayoenda kwa passport akagoma kuwa chama chake hakiko tayari kusajiri raia wa nchi nyingine kuwa wanachama wake akajenga hoja passport kwenda Zanzibar zikafutwa Hadi Leo .Hawa wa Chadema SI wajenga hoja Ni waporomosha matusi tu ukiangalia hoja yenye mantiki huoni zaidi ya mitusi na kejeli tu.Hata mtu akiomba ukimbizi mamlaka za nchi husika kwa kweli wana kazi kubwa ya kupitia sababu za huyo mtu kukimbia kuangalia hasa anachopigania Nini chenye mantiki ? Unakuta yaani Ni Kama hakipo zaidi ya mitusi na kebehi kwa serikali na viongozi.Mkosoaji wa serikali na mtukanaji Ni watu wawili tofauti.Upinzani uliopo una watukanaji Sio wakosoaji..Mkosoaji huwa na hoja nzito zilizosheheni ushahidi hakikika wa kweli bila kebehi wala matusi kwenye hoja anayowakilisha na Mara nyingi Ni mtu asiye na jazba.Mfano Ni Marehemu Mtikila
 
Mkuu,

Kwakweli Makada wa siku hizi wanatia aibu.
Mdude kusema hata anakosoa yaani mtu huoni pointi ni ujinga mtupu mfano anasema mnanunua ndege wakati hospitali hazina dawa Wala haziwezi tibu hate mende!!! Yeye Sasa hivi anatibiwa hospital hizo hizo alizosema hazina uwezo wa kutibu hata mende!!! Kiukweli upinzani wa Tanzania Bado Sana tu kihoja kwa Tanzania mtukanaji serikali na viongozi ndio huitwa mkosoa serikali very sad!!! Watu Kama Mtikila ndio walikuwa wakosoa serikali siji sahau Mtikila alivyosababisha passport kufutwa kutotumika kwenda Zanzibar kwa watanzania..Enzi hizo kwenda Zanzibar ilikuwa unaenda kwa passport Kama unaenda Ulaya.Vyama vingi vilipoanza ilitakiwa chama kiwe na wanachama Tanzania bara na Zanzibar ili kisajiliwe.Mtikila akagoma kusajili wanachama wa chama chake kutoka Zanzibar na akajenga hoja kuwa Zanzibar Ni nchi Tena unayoenda kwa passport akagoma kuwa chama chake hakiko tayari kusajiri raia was nchi nyingine kuwa wanachama wake akajenga hoja passport kwenda Zanzibar zikafutwa Hadi Leo .Hawa wa Chadema SI wajenga hoja Ni waporomosha matusi tu ukiangalia hoja yenye mantiki huoni zaidi ya mitusi na kejeli tu.Hata mtu akiomba ukimbizi mamlaka za nchi husika kwa kweli wana kazi kubwa ya kupitia sababu za huyo mtu kukimbia kuangalia hasa anachopigania Nini chenye mantiki ? Unakuta yaani Ni Kama hakipo zaidi ya mitusi na kebehi kwa serikali na viongozi.Mkosoaji wa serikali na mtukanaji Ni watu wawili tofauti.Upinzani uliopo una watukanaji Sio wakosoaji..Mkosoaji huwa na hoja nzito zilizosheheni ushahidi hakikika wa kweli bila kebehi wala matusi kwenye hoja anayowakilisha na Mara nyingi Ni mtu asiye na jazba.Mfano Ni Marehemu Mtikila
 
Haishangazi.. bora huyu kaamua kusema ukweli. Wale wengine hakuna linalojificha chini ya jua.. chama hicho kitakuja kuumbuka na wanapopapenda gerezani wataingia kuishi huko kabisa..
 
Nakumbuka Mandela aliwahi kukimbilia Tanzania nadhani akielekea Ghana Kwa kutumia passport ya nchi ingine akiwakimbia kaburu.mdude naye alikua anakimbia mkono wa jiwe na bashite
 
Mdude kusema hata anakosoa yaani mtu huoni pointi ni ujinga mtupu mfano anasema mnanunua ndege wakati hospitali hazina dawa Wala haziwezi tibu hate mende!!! Yeye Sasa hivi anatibiwa hospital hizo hizo alizosema hazina uwezo wa kutibu hata mende!!! Kiukweli upinzani wa Tanzania Bado Sana tu kihoja kwa Tanzania mtukanaji serikali na viongozi ndio huitwa mkosoa serikali very sad!!! Watu Kama Mtikila ndio walikuwa wakosoa serikali siji sahau Mtikila alivyosababisha passport kufutwa kutotumika kwenda Zanzibar kwa watanzania..Enzi hizo kwenda Zanzibar ilikuwa unaenda kwa passport Kama unaenda Ulaya.Vyama vingi vilipoanza ilitakiwa chama kiwe na wanachama Tanzania bara na Zanzibar ili kisajiliwe.Mtikila akagoma kusajili wanachama wa chama chake kutoka Zanzibar na akajenga hoja kuwa Zanzibar Ni nchi Tena unayoenda kwa passport akagoma kuwa chama chake hakiko tayari kusajiri raia wa nchi nyingine kuwa wanachama wake akajenga hoja passport kwenda Zanzibar zikafutwa Hadi Leo .Hawa wa Chadema SI wajenga hoja Ni waporomosha matusi tu ukiangalia hoja yenye mantiki huoni zaidi ya mitusi na kejeli tu.Hata mtu akiomba ukimbizi mamlaka za nchi husika kwa kweli wana kazi kubwa ya kupitia sababu za huyo mtu kukimbia kuangalia hasa anachopigania Nini chenye mantiki ? Unakuta yaani Ni Kama hakipo zaidi ya mitusi na kebehi kwa serikali na viongozi.Mkosoaji wa serikali na mtukanaji Ni watu wawili tofauti.Upinzani uliopo una watukanaji Sio wakosoaji..Mkosoaji huwa na hoja nzito zilizosheheni ushahidi hakikika wa kweli bila kebehi wala matusi kwenye hoja anayowakilisha na Mara nyingi Ni mtu asiye na jazba.Mfano Ni Marehemu Mtikila
Mkuu 100% true said,hawa wapinzani wa tanzania ni kweli ni maamjma tupu!
 
Hivi

Waweza jitoa ufahamu makusudi unataka na wengine wawe kama wewe?
 
Hapo anasema mupango iliratibiwa na boniface jacob na heche, leo kasema ni lema na heche
 
Nimestushwa na taarifa hii ya Mdude aliyotoa kwa muandishi wa Gazeti la Mwananchi. Kuwa kabla ya tukio hili kulikuwa na mipango ilioratibiwa na Bonface Jacob na John Heche ya kumkimbizia Kenya. Kama si Mdude kughaili baada ya kufika Arusha, nahakika mpango huu ungefanikiwa tungetangaziwa kupotea kwa Kamanda mwingine wa chama hicho.

=====

Mdude aeleza kilichomfanya asihamie Kenya

Mbeya/Dar. Mdude Nyagali, maarufu ‘Mdude Chadema’, amesema kutokana na misukosuko ambayo amekuwa akiipata alifikia hatua ya kutaka kuhama nchi ili akaishi uhamishoni, lakini alighaili akiwa njiani.
Mdude kwa sasa amelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kuokotwa na madereva bodaboda kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Inyala wilayani Mbeya.

Jumamosi ya Mei 4, Mdude, mkazi wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe alidaiwa kutekwa na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake mjini Vwawa, kisha akapelekwa kusikojulikana hadi alipokutwa usiku wa Jumatano iliyopita eneo la Inyala akiwa hoi kutokana na kipigo alichokipata.

Akizungumza na Mwananchi hospitalini hapo, Mdude alisema kutokana na misukosuko iliyokuwa inamkabili kabla ya tukio hilo aliomba msaada kwa viongozi wa Chadema na baadaye akazungumza na meya wa Ubungo, Boniface Jacob na mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche ambao walimfanyia mpango kwenda kuishi nchini Kenya kabla ya kubadilisha uamuzi wake.

“Ni sahihi kabisa, kwani kuna kipindi misukosuko ilizidi, mara kesi mahakamani. Baadaye nikasema nitafute hifadhi nchi nyingine. Ndio wakawa wamenitafutia hifadhi Kenya, wakanifanyia michakato mingine yote. Na nikasafiri hadi Arusha kwa ajili ya kuelekea nchini Kenya,” alisema Mdude.

Alisema alipofika Arusha, nafsi yake ilimsuta, akafikiria kwamba akiondoka nchini watu wengi watakata tamaa, hivyo ni bora arudi kwa sababu Tanzania ni nchi yake.

Alisema uamuzi wake huo uliambatana na kumwachia Mungu kila jambo maishani mwake, na kama ana makosa basi atahukumiwa kwa makosa yake na iwapo yuko sahihi Muumba wake atamsimamia.

Akizungumzia uamuzi wa Mdude kutaka kutimkia uhamishoni, Meya Jacob alisema, “binafsi amenifundisha ujasiri, kuna wakati alikuwa anatumiwa meseji za vitisho na watu wasiojulikana, ilifikia hatua kama chama tukaona atafutiwe makazi nje ya nchi lakini yeye alikataa akasema ataendelea kuwepo hapa na kupambana hadi mwisho wake.”

Jacob, ambaye diwani wa Ubungo (Chadema), alisema kwa muda aliofahamiana na Mdude amemfundisha ujasiri na kutokata tamaa wala kukubali kuyumbishwa kifikra.

“Ni mpiganaji asiyekata tamaa, anasimama na kuonyesha wazi kupigania anachokiamini, haya matatizo si mara ya kwanza kumkuta na amekuwa akikutana na vitisho mara kadhaa, lakini hajawahi kuwa na hofu.”
Alisema umaarufu wa mwanachama huyo wa Chadema ambaye pia ni kiongozi wa mafunzo Kanda ya Nyasa umekuwa mkubwa kutokana na mwenendo wake wa kuikosoa Serikali kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Naye mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alimwelezea Mdude kuwa ni kijana mzalendo mwenye kusimamia kile anachokiamini na kutekwa kwake kunahusishwa na mwenendo wake wa ukosaji.

Alieleza kuwa mwanachama wao huyo amekuwa akiikosa Serikali kwa sababu anaamini ni nafasi yake ya kikatiba kama Mtanzania na vilevile ni kiongozi wa chama cha upinzani ambacho kina jukumu la kutoa mawazo mbadala ikiwemo kukosoa.

Akizungumzia uchunguzi wa polisi, kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando alisema wanaendelea na uchunguzi wa tukio la kutekwa kwa Mdude, lakini wanapata ugumu kwa kuwa mhusika mwenyewe hasemi ukweli.

“Daah! Unauliza maswali magumu... Mdude mwenyewe hasemi waliomteka akina nani na kama yeye mwenyewe anasema hawajui, unafikiri sisi tutajua kweli? Anapaswa kusema gari lilikuwa na namba fulani, walioniteka walikuwa wanasema hiki, hiki na hiki, ili na sisi tuanzie hapo,” alisema kamanda Kyando.
“Tukimuuliza walipokuwa wanakupiga walikuwa wanakuambia nini? Hasemi. Sasa hapo tunafanyaje? Kimsingi majibu rahisi ni kwamba bado uchunguzi unaendelea, ukikamilika tutawaambia.”

Alisema, “Mdude hayupo wazi kwani lazima wanapokupiga wanasema kwa nini uliniibia au kwa nini ulifanya hivi au kwa nini umefanya hivi.”
Ni mwandishi na MUANDISHI..!
 
Kwa kweli Mtikila type ndio uinzani wa kweli uinzani wenye hoja. Walitaka kumtoroshea Kenya Kinyemela na kuanza kuandika kwenye vyombo bya habari kapotea. Big up Mdude. Mtekaji atajulikana soon!
 
wangemfikisha Nairobi Heche Na Lema wangempoteza kama walivyompoteza Ben Saanane
 
Mdude kusema hata anakosoa yaani mtu huoni pointi ni ujinga mtupu mfano anasema mnanunua ndege wakati hospitali hazina dawa Wala haziwezi tibu hate mende!!! Yeye Sasa hivi anatibiwa hospital hizo hizo alizosema hazina uwezo wa kutibu hata mende!!! Kiukweli upinzani wa Tanzania Bado Sana tu kihoja kwa Tanzania mtukanaji serikali na viongozi ndio huitwa mkosoa serikali very sad!!! Watu Kama Mtikila ndio walikuwa wakosoa serikali siji sahau Mtikila alivyosababisha passport kufutwa kutotumika kwenda Zanzibar kwa watanzania..Enzi hizo kwenda Zanzibar ilikuwa unaenda kwa passport Kama unaenda Ulaya.Vyama vingi vilipoanza ilitakiwa chama kiwe na wanachama Tanzania bara na Zanzibar ili kisajiliwe.Mtikila akagoma kusajili wanachama wa chama chake kutoka Zanzibar na akajenga hoja kuwa Zanzibar Ni nchi Tena unayoenda kwa passport akagoma kuwa chama chake hakiko tayari kusajiri raia wa nchi nyingine kuwa wanachama wake akajenga hoja passport kwenda Zanzibar zikafutwa Hadi Leo .Hawa wa Chadema SI wajenga hoja Ni waporomosha matusi tu ukiangalia hoja yenye mantiki huoni zaidi ya mitusi na kejeli tu.Hata mtu akiomba ukimbizi mamlaka za nchi husika kwa kweli wana kazi kubwa ya kupitia sababu za huyo mtu kukimbia kuangalia hasa anachopigania Nini chenye mantiki ? Unakuta yaani Ni Kama hakipo zaidi ya mitusi na kebehi kwa serikali na viongozi.Mkosoaji wa serikali na mtukanaji Ni watu wawili tofauti.Upinzani uliopo una watukanaji Sio wakosoaji..Mkosoaji huwa na hoja nzito zilizosheheni ushahidi hakikika wa kweli bila kebehi wala matusi kwenye hoja anayowakilisha na Mara nyingi Ni mtu asiye na jazba.Mfano Ni Marehemu Mtikila
Bwana mdogo keshaumwa na nyoka, sasa hivi akiona jani tu mwili mzima unasisimka.
 
Mtoa uzi picha hiyo inasadifu akili yako kuwa ulichoweka humo huende ndo kipo kichwani mwako kwa uandishi huu.
 
Back
Top Bottom