Mdomo umekosa magego na sio meno

julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
2,606
3,399
Eeh waswahili wanasem mdomo ulikosa magego sio meno. Msiba huu umegusa kila mwenye mapenzi na nch yake. Dr Magufuli alikua na sauti inayoenda nyika,sauti moja tu inaheshimika akisema kasema.

Sifa ya kiongozi akisema sauti yake iwe kuu. Mambo aliyoyafanya Itakuchukua miaka mingine 50 kuyaongea. Kaweza kujenga vituo vya afya idadi kubwa kushinda awamu zooote zilizopita tena kwa muda mfupi eeeh mdomo umekosa magego sio meno.... msiba mzitooo hasa.

Yeye ndio alituambia Jamen tupo kwenye vita ya uchumi, na ndio alisema mwelekeo ndio huuu ndugu zangu lazima tuseme ukweli..vita ya uchumi ipo hivi na inapopiganwa inapiganwa hivi.

Naomba sana Dr Mpango ukaze uzi kweli kweli kwemye mapato kama ilivokuwa kipindi cha marehem mzee kiwe zaidi na zaidi, mkazo uwe kwenye mapato pesa zifuatwe huko hukoo walipozila wazitapike kupitia matundu yao yote yalio wazi "eeh mdomo umekosa magego na sio meno"

Rais alitupa ujasiri wa kujiamini na tusiwe mbuzi wa kafara mfano wa chanjo hizi ambazo mpaka sasa ni kizungumkuti tafrani kubwa. Mh hakukataza kujikinga bali alisema njia zote zitumiwe eeh mdomo ulikosa magegoo na sio meno.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom