Mdogo wangu katangaza ndoa na x wangu.

Mdogo wangu katangaza ndoa na x wangu.

SERIKALI 3

Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
82
Reaction score
18
Weekend iliyopita nilikuja kuombwa ruhusa na ushauri toka kwa mdogo wangu (mtoto wa baba mdogo) ambaye kwa namna moja au nyingine niko naye kwangu tokea 2009 kwamba anataka kuoa, la ajabu kumbe barua ya uchumba keshapeleka tayari na mahari inapelekwa wiki mbili zijazo. Kwa sasa nipo mkoani kimasomo na anayekwenda kumuoa ni ex wangu wa kitambo ambaye ni mtoto wa Baba mwenye nyumba hapo ninapokaa DAR.

Kwa sasa mie nimeoa na bado nipo nyumba hiyohiyo. Je, kipi nifanye hapo. Nikauke kimya au nimwambie dogo amuache huyo binti?.



 
mwambie tu kuwa uliwahi kutoka nae, kumpa tu taarifa kuliko akisikia kutoka kwa huyo mwanamke atakuhisi vibaya. si huna tena mahusiano nae?
 
Ww umepita umepita tu, dunia duara ww muache mwenzio aoe kwa raha zake, umeshasemax nikwamba kapita
 
mwambie tu kuwa uliwahi kutoka nae, kumpa tu taarifa kuliko akisikia kutoka kwa huyo mwanamke atakuhisi vibaya. si huna tena mahusiano nae?
sawa sina mahusiano naye tokea 2011 lakini nimepata taarifa wakati wameshapangiwa tarehe ya kutoa mahari( next two week) huoni kama litaleta zogo tena kwa wife akijua? ikizingatiwa pia ni mtoto wa mwenye nyumba.
 
Ina maana anaoa huju anaishi nyumbani kwako?

Akishaoa anarudi kwako na mkewe...watazalia kwako na kutukuu kwako?

Mtu hana pa kuishi bado anaoa halafu akaishi na mkewe kwa kaka?

Bado haijaniingia akilini
 
Sasa kama ushaoa na mlishaachana/ hampendani tena shida iko wapi?

Au unaogopa aibu wife akijua?!

Fanya mpango uhame kama vipi

"ukiona wa nini,mwenzio anasema atampata lini"
 
Muache aoe tu hakuna shida,yaliyopita si ndwele.....
 
Ina maana anaoa huju anaishi nyumbani kwako?

Akishaoa anarudi kwako na mkewe...watazalia kwako na kutukuu kwako?

Mtu hana pa kuishi bado anaoa halafu akaishi na mkewe kwa kaka?

Bado haijaniingia akilini
ni ghafla sana kwani jamaa kaanza kazi february tu, yaani hadi nashindwa kuelewa kilichotokea. Labda tulikuwa tunachanganywa kimya kimya?
 
Sasa kama ushaoa na mlishaachana/ hampendani tena shida iko wapi?

Au unaogopa aibu wife akijua?!

Fanya mpango uhame kama vipi

"ukiona wa nini,mwenzio anasema atampata lini"

sikuwa na hofu ya kuhama kwa kuwa naye (huyo bint) ailipata ajira mkoani mwaka wa pili sasa kwa hiyo akija home ni likizo ambayo hkai zaidi ya wiki 2.
 
Situation ya namna hiyo ilishawahi kunitokea.

By the way mimi nimeoa dada wa ex wangu.

Kiukweli kabisa ni kuwa mimi na huyo binti tulikuwa wapenzi(yeye alinipenda mimi) zamani sana(utoto) ila mimi sikuwa nampenda. Alivyonipeleka kwao nikamuona dada yake, tulivyoangaliana tu tulipendana sana(20yrs ago).

Anyways nikaendelea na mdogo mtu taratibu ila nikaanza kumpotezea. Mwishowe tukaachana naye alikuwa machepele na mambo yake akaendelea na hamsini zake.

Baada ya miaka kama 10 hivi nikakutana na dada mtu na kiukweli alishakuwa na maisha yake ila dah penzi halijifichi.

Tukafungua ukurasa. Aisee ilikuwa kama vita hivi maana mama mtu mchongaji sana ila ndio hivyo. Msure wake alisupport kuwa yaliyopita yalishapita.

Sasa hivi ex wangu ni shemeji, na ana watoto wake so wanakuja home fresh tu hakuna lolote.

Ushauri wangu;

Kwa case yako PIGA KIMYA! Its too late kusema lolote. Hata mimi nina siri zangu baadhi pia na ninaamini wife anazo ila tumezifukia.

Usiweke mahusiano yoyote ambayo si ya msingi na shemeji yako. Awe shemeji tu tena awe NDUGU!
 
ni ghafla sana kwani jamaa kaanza kazi february tu, yaani hadi nashindwa kuelewa kilichotokea. Labda tulikuwa tunachanganywa kimya kimya?

Nakushauri umwambie dogo mapema tena kwa hekima sana! uspofanya hivyo kinachofuata tegemea ni ugomvi na mdogo wako maana akili ya mwanamke ni kukomoa! jaribu kuangalia kwa kina kwanini atembee na wewe kisha muachane na aoane na mdogo wako!!!?? kuna elements za kukomoa hapo tena huyo mdada naona hana hekima mtu huwezi kuwa mpenzi wa ndugu wawili hata siku moja hata rafiki tu kwa wadada na wakaka wenye hekima huuliza kwanza ili kuepusha fedheha na malumbano! wahi mstopishe dogo, akikuelewa vyema asipokuelewa muache wembe mkate!
 
Yani mdogo wako mnakaa nyumba moja halafu hujui hata mpenzi wake ni nani? au ulikuwa unapita wakati tayari una wife? mwache mwenzio aoe. acha mkewe ndio amsimulie hizo hadithi
 
Nakushauri umwambie dogo mapema tena kwa hekima sana! uspofanya hivyo kinachofuata tegemea ni ugomvi na mdogo wako maana akili ya mwanamke ni kukomoa! jaribu kuangalia kwa kina kwanini atembee na wewe kisha muachane na aoane na mdogo wako!!!?? kuna elements za kukomoa hapo tena huyo mdada naona hana hekima mtu huwezi kuwa mpenzi wa ndugu wawili hata siku moja hata rafiki tu kwa wadada na wakaka wenye hekima huuliza kwanza ili kuepusha fedheha na malumbano! wahi mstopishe dogo, akikuelewa vyema asipokuelewa muache wembe mkate!
kumbuka nimeoa tayari na mtoto mmoja yakivuja je? wakati sikumpa taarifa wife za huyo mdada?
 
Weekend iliyopita nilikuja kuombwa ruhusa na ushauri toka kwa mdogo wangu (mtoto wa baba mdogo) ambaye kwa namna moja au nyingine niko naye kwangu tokea 2009 kwamba anataka kuoa, la ajabu kumbe barua ya uchumba keshapeleka tayari na mahari inapelekwa wiki mbili zijazo. Kwa sasa nipo mkoani kimasomo na anayekwenda kumuoa ni ex wangu wa kitambo ambaye ni mtoto wa Baba mwenye nyumba hapo ninapokaa DAR.

Kwa sasa mie nimeoa na bado nipo nyumba hiyohiyo. Je, kipi nifanye hapo. Nikauke kimya au nimwambie dogo amuache huyo binti?.




Mm sioni shida hpo uliacha yeye kabeba,haina shombo hyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom