Mdhamini wa waasi wa ADF

75 wa ADF waliuawa
Ukisoma Post No. 60 utajiuliza, hivi hizo maiti zinazotangazwa mbona hazikuonekana? Ni nani alithibisha uwepo wa hizo maiti? Kama mtoa bandiko anavyosema kuna mengi yapo nyuma ya pazia kuliko tunavyosema. Hao ADF wanasingiziwa lakini ukweli ni kwamba FARDC wanahusika na hili shambulizi.
 
Wakati mwingine, ingawa sina uhakika, sio kila taarifa au picha za matukio yote ya mapigano ya kijeshi huwekwa bayana kimkakati wanaoujua wanajeshi wenyewe kama wataalamu
 
Wakati mwingine, ingawa sina uhakika, sio kila taarifa au picha za matukio yote ya mapigano ya kijeshi huwekwa bayana kimkakati wanaoujua wanajeshi wenyewe kama wataalamu
Hiyo taarifa ni kwa mujibu wa online magazine ya Beni. Hawa huwa hawana kuremba
 

Kweli. Utawarundikaje watu wa aina moja sehemu moja ?

Anyway, tusubiri wajuvi wa Haya mambo waseme ilikuwaje wazenj waliwekwa pamoja? - nahisi au najua ni wazenj kwa kuangalia majina yao, somehow sura pia
Ndo utaratibu? Au ilitokea kibahati tu ?

Lakini inawezekana ni utaratibu uko hivyo kuwa askari kadhaa kutoka kikosi Fulani wanaenda kwenye mission nje. Huenda sio effective kwa jeshi kuchanganya askari kutoka vikosi tofaut tofauti wanapoenda kwenye mission moja huko nje. Huenda askari wanaojuana siku nyingi wanaweza kufanya kazi pamoja kwa ubora zaidi
 


Labda hapa kwenye hiki kivungu ndipo penye jibu kamili. Huwezi kuchukua ovyo ovyo. Huenda wanachukua kwa mfano ,narudia kwa mfano Brigade ya Unguja wanachukua askari toka Kikosi cha jeshi 43KJ Chakechake,platuni mbili au tatu toka kombania mbili au tatu tofauti.
Tena wanachukua askari wengine toka 21 KJ Micheweni, platuni kadhaa.


Nakumbuka simulizi za wakati wa vita ya Kagera,kuna kipindi askari wetu walipigwa vibaya na wengi wao walikuwa wa kikosi cha nyuki ambacho ni kutoka Zanzibar.

NB: Ni mawazo yangu binafsi tu , si lazima yawe sahihi.
 
Alafu eti wame hasi Uganda lkn hujuma zao zimeelekezwa Congo na si Uganda!!!!.. it's actually inconceivable
 
Hii kitu ni uhujumu.
Vijana wetu watapotea sana kule.
Siasa za hii Dunia ni Magumashi tupu.
 
Upendeleo ni mkubwa sana! Mamilioni ya un lazima roho nyingi zitapotea! Askari wafanikiwao kurudi na takehomekubwa kichocheo cha wengine kuhonga ili waende! Tunalinda amani au tunaongeza kipato?
 
"I Will Wait For U At The Right Place And I'll Hit U"-Paul Kagame's Words To Kikwete.
 
Mpaka enzi hizi unazungumzia ubara na uzabzibar? U must have a problem upstairs!!! Sio bure.
 
Mseveni na kagame ni maadui wao kweli au wana mgogoro wa maslahi. Wajeshi wetu wameuawa na watu wa Rwanda.
 
Hakuna mwanajeshi hata mmoja anaetoka nchi maskini na kujiongeza kama unavyofikiria.
Na ni makosa kwa sheria za UN kuondoka na kitu kilichopo Congo (Madini, mafuta nk) labda vitenge.

Hakuna mda wanaoupata wa kwenda kujiongeza hata kidogo, wakifika wanakua kama wafungwa makambini. Kutoka kwao nje watatoka na convoy na si kwenda kuzurura au kutafuta unachokifikiria.

Congo ni kweli imejaa mali lakini sio rahisi kupata, kuchimba kwenyewe mchanga kuna mlolongo mzima mpaka watoe eneo kwa maana wanaona kama wanataka kuibiwa mali zao.

Watanzania wamekua target sana kwa sababu asilimia kubwa sana ya waasi hawampendi Kabila na wanataka aondoke madarakani.
Sasa basi, mawazo yao yanawapelekea kwamba JWTZ ndo wanaempa kiburi na kuendelea kutawala.

Kuna majeshi yanaenda mission na kuna majeshi yanaenda kibiashara. Wahindi toka enzi na enzi wapo Congo na wameshafanya kama ndo mji wao kwa ajili ya biashara. Hao hawapo kimisheni.

Tukija suala la nani anawapa msaada ADF jibu kubwa ni wazungu. Na kama kuna mtu humu alishawahi kufika kwenye ngome yao utakuta kuna uwanja wa kufulia chopper, jiulize inaenda kufanya nini.

Mgao wa juisi wanazopata jeshi la UN ndo hizo hizo wanazokua nazo wao. Pia kuna habari baadhi ya wafanyakazi wa Munosco wanazivujisha. Silaha kubwa zikiingia na kutoka wanajua.

Kuna mizinga ilisafirishwa kutoka Congo to Tanzania pia walijua.
Hata hivyo sio wazungu tu wanaofurahia vita kuendelea. Wa Congo wenyewe wanayafurahia hayo ambao wameajiriwa na UN.
Na wao pia wanawachukia JWTZ.
Maana wanajua wao wanaweza kimaliza vita, na vikiisha wao watakula wapi???
 
Mkuu mbona jibu lipo wazi wala sio gumu simple kabisa. Nakujibu la kufa Wazanzibari wengi ni hivi:

Kila mission watu wanayoenda kuna kundi (brigade) linapewa uhuru wakuandaa askari na baada ya hapo wanaongezea sehemu zingine kama ujirani mwema wa kikazi.

Brigade kama sikosei zipo Tano.
* Chui - Dar es laam.
* Faru - Tabora.
* Tembo - Songea.
* Mbuni - Arusha.
* Nyuki - Zanzibar.

Naomba tuelewane; kwa mtindo huo ndo wanakua wanapokelezana kuandaa mission.
Hii ya mara hii wameandaa "Nyuki" jiulize wengi watatoka wapi?
Nafikiri umenielewa na kama hujanielewa uliza sehemu ambayo inakutatiza.
 
''Mmeshaanza kuuona ukweli'' My literature teacher Mr Michael Simwaba
 
Ajabu ninayoiona katika kadhia hii yote, ni kuwa hakuna mshambulizi hata mmoja aliyejeruhiwa na kutekwa! Au ni mimi sina habari?!
Balozi Augustine Mahiga akihojiwa na BBC anatudanganya Eti Vijana wetu walipambana kwa saa 14, uongo mtupu, wale Vijana walipigwa Ambush ya kustukiza
 
Balozi Augustine Mahiga akihojiwa na BBC anatudanganya Eti Vijana wetu walipambana kwa saa 14, uongo mtupu, wale Vijana walipigwa Ambush ya kustukiza

Ile wengi tulishaishtukia ni porojo za kawaida. Vijana walivamiwa kwa kushtukizwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…