- Tunachokijua
- Halima Mdee aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Kawe mwaka 2010 hadi 2020 alipoachia nafasi hiyo baada ya kushindwa na Jesephat Gwajima katika uchaguzi mkuu wa 2020. Baadaye aliteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Madai
Kumekuwapo na grafiki inayosambaa mitandaoni ikiwa na nembo ya wasafi media huku ikiw ana ujumbe unaosomeka “MDEE AMVAA GWAJIMA KUANIKA MAOVU YAKE”, grafiki hiyo imeambatana na inayoonekana kuwa ni ‘sreenshot’ ya mbunge wa viti maalum Halima Mdee.
Uhalisisa wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli. Inayoonekana kuwa ni screenshot ya ukurasa wake wa X wa halima mdee ni ya kughushi.
Ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa katika ukurasa rasmi wa Halima James Mdee kama inavyoonekana. Hadi wakati ripoti hii inaandikwa taarifa ya mwisho inayoonekana katika ukurasa rasmi wa Mdee ni ya Mei 17, 2025 akimjibu mdau mmoja aliyekuwa akimshutumu kwa usaliti.
Aidha inayoonekana kuwa ni grafiki inayofanana na ya Wasafi media haikuchapishwa na wala kutolewa na chanzo hicho cha taarifa na badala yake ni ya kughushi. Licha ya kuwa grafiki hiyo haijachapishwa na chanzo hicho lakini pia ina baadhi ya makosa ikiwemo matumizi ya nukta kwenye ‘caption’ jambo ambalo kwenye grafiki za Wasafi halipo na utofauti mwingine ni aina ya mwandiko “font”