Mdau: Mlitaka Rais afanye nini kuhusu tozo ya miamala ya simu?

Asha Ommary

Member
Sep 1, 2020
97
125
Katika awamu hii ya sita hakuna jambo ambalo linapaswa kupongezwa kama utulivu, hekima na maarifa aliyoyaonyesha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi hiki ambacho alipitia magumu kama Rais wa Nchi kwa kupambana na mtikisiko wa kiuchumi kutokana na janga la korona ambalo ni kwa Dunia nzima kila mahali ni kilio.

Hivi kweli Watanzania wenzangu tunakubalije kuchezewa akili na watu ambao kwao hakuna jema katika Nchi yetu wao wanaona mabaya tu basi kiasi cha kuwa wapingaji wa kila jambo na wapinzani wa muda wote hata kama Serikali inafanya mazurii kiasi gani.

Rais alishatuweka wazi kuwa uchumi wetu ulishuka na sababu iko wazi kabisa kutokana na janga hili la corona , licha ya kwamba serikali muda wote imejitahidi kupambana ili kuhakikisha uchumi mwetu unakuwa imara. Hili tu la Rais Samia kusema wazi ni dalili tosha ya kuonyesha ni kwa namna gani sisi kama Watanzania tunapaswa kuwa sehemu ya kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu licha ya changamoto zilizopo ambazo ni kwa Dunia nzima.

Serikali ina vyanzo mbalimbali vya mapato vya ndani na vya nje kama mikopo lakini unadhani ni salama zaidi kuliongezea Taifa deni katika kipindi hiki cha mdororo wa kiuchumi wa kidunia? Ndio maana tunapotakiwa kushiriki katika kulipa kodi ya mshikamano kupitia tozo hizi za miamala na katika mafuta lazima tujiulize maswali matatu muhimu .

Swali la kwanza “ Kwa nini tozo hii kwa wakati huu? “ leo hii uchumi umeshuka na dunia inalia kuna dhambi gani kuwa na tozo itakayochagiza maendeleo katika Taifa letu tena ni maendeleo kule vijijini ambako tuliopo mijini tumekuwa tukipokea simu za changamoto kila uchao, sasa kwanini simu hizi zisipungue angalau kwa kuwapa nafuu na wenzetu wa vijijini.

Swali la pili “ Tozo hizi zinatumika wapi na zinamnufaisha nani na zitatumikaje? “ Hapa ni muhimu sana kupaelewa kwani moja kati ya njia ya kujipatia maendeleo kwa nguvu zetu wenyewe ni kulipa kodi au kupitia tozo kama hizi za mshikamano ambapo serikali imeshatuweka wazi ni kwa ajili ya maendeleo au shughuli za kijamii maji, afya, elimu , barabara vijijini pamoja na nishati vijijini . Ni nani asiyetambua ni kwa kiasi gani wananchi walioko pembezoni huko wanavyopata shida ya barabara , suala la nishati na maji jambo ambalo kwa sasa serikali imeamua kutumia njia ya moja kwa moja kutatua changamoto hizi kwa kuanzisha kodi mahususi kwa ajili ya changamoto hizi ili ziwe historia.

Swali la tatu “ Mimi ninayekatwa ni kwa kiasi gani nitaathiriwa na tozo hizi kuliko athari ambazo ningezipata kwa kuwa mchoyo wa kuwachangia ndugu zangu kijijini kupitia serikali ili angalau niepushe madhara yatokanayo na kukosa barabara , kukosa maji na umeme bila kusahau vitendea kazi katika huduma za afya. Ni wakati sahihi kwa Watanzania kuamini katika uwezo wetu wa kujijenga kiuchumi na sio kulalamika kwani hakuna wa kutupa msaada bure usiokuwa na msharti ambayo yatakuwa mwiba na mzigo mzito kwa vizazi vijavyo.
Naomba kutoa rai kwa watanzania tusiisaliti Nchi yetu kwa dhambi ya ubinafsi ambapo madhara yake ni makubwa sana. Wewe uliyejaaliwa hicho kidogo hebu tamani kuwa sehemu ya mageuzi ya kiuchumi katika Taifa lako.

Hivi kweli tunamini kabisa kwamba wafanyakazi na wafanyabiashara wakubwa ndio watubebe kiuchumi kama Taifa ? kiasi ambacho hata tu kuchangia 300 mpaka 10,000 au 16,000 tunaona ni mzigo mkubwa ambapo tunatambua fika ndg zetu wafanyakazi wao kila mwezi wanakatwa kodi na bado wanakatwa tena kwenye matumizi katika ongezeko la thamani?

Natambua hoja ya rasilimali za nchi kuwepo na uwekezaji lakini je hatuzioni shule kila kata na elimu bila malipo ? je hatuzioni hospitali za rufaa kila mkoa, hatuzioni hospitali za wilaya, vituo vya afya kila kata na zahanati kila kijiji? Je hatuwaoni watu wa REA kila kijiji na kitongoji? Hatuzioni barabara kila wilaya kwa nchi nzima? Je kweli hatulioni bwawa la Mwl Nyerere na Mradi wa Reli ya kisasa? Hivi kweli hatuzioni ndege za ATCL?

Jamani Serikali inafanya mengi tena makubwa lakini kama kweli tuna nia njema na tunaiona dhamira ya Rais Samia na awamu hii ya sita tuchapeni kazi na tushiriki kulipa kodi ili tupige hatua na daima tutambue Watanzania Hakuna maendeleo yanayokuja bila maumivu na siku zote Mvumilivu hula mbivu.

TUMUUNGENI MKONO RAIS SAMIA ANA DHAMIRA NJEMA KATIKA TAIFA LETU.

Ni mimi mpita njia

Kamshamura Kuku Magu Dedede
 

Rangi 2

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
294
250
Dawa ni moja tu: Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima mfano, wabunge wa covid 19, wabunge wa kuteuliwa na rais, ukubwa wa baraza la mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya. Mamlaka mbalimbali zisizokuwa na tija.

Na wewe jiongeze mshenzi wewe!
 

jailos mrisho

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
466
1,000
Kwani leo ndo kodi zinaanza kulipwa? Hujui watu walianza kulipa kodi toka enzi za mkoloni? Miaka 60 wameshindwa kufikisha huduma vijjn ndo wataweza kufikisha kwa hizo kodi.

Shida mnashabikia vitu kufuata mikondo ya kiitikadi za kisiasa, kidini, kikabila na mengine bila kujali hatma ya taifa kwa ujumla hii n sumu kubwa sana inayomaliza watu weusi ingekuwa kodi zinasimamiwa vzuri hata hzo chache zinazopatikana nakuhakikishia huduma bora zingekuwepo, mfano mdogo tu.

JPM alikuwa anakusanya kodi kwa uhakika hakutaka ushenzi wa kuwabembeleza mabwenyenye..leo hii unaingia unaanza kuwaramba miguu hao walikuwa wanaikwapulia serikal mapato kwa kukwepa kulipa kodi kama mwenyekit mmoja wa chama huko mwanzaa..jpm alijenga hospital kila wilaya na huduma zilikuwa zinapatikana wanafunzi walikuwa wanakaa kwenyr viti shule zilikarabatiwaa.

Leo hii unakuja na plan ya kipuuzi kabisaaa kana kwamba huko nyuma hatukuaa tunalipa kodi.

Nakuhakikishiaa miaka kumi itapita na hakuna chochote kitakachofanyika zaidi ya hizo pesa kuingia kwenye mifuko ya wezi
 

MAPITO Mwanza

JF-Expert Member
Aug 21, 2018
1,811
2,000
Dawa ni moja tu: Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima mfano, wabunge wa covid 19, wabunge wa kuteuliwa na rais, ukubwa wa baraza la mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya. Mamlaka mbalimbali zisizokuwa na tija.
Na wewe jiongeze mshenzi wewe!
Makofi mengi sana kwa mjumbe huyu kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwa kwaaaaaaaaaa
 

DURACEF

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
1,253
2,000
Dawa ni moja tu: Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima mfano, wabunge wa covid 19, wabunge wa kuteuliwa na rais, ukubwa wa baraza la mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya. Mamlaka mbalimbali zisizokuwa na tija.
Na wewe jiongeze mshenzi wewe!
Asante sana....umemaliza
Huyu jamaa kima sana.
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,429
2,000
Dawa ni moja tu: Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima mfano, wabunge wa covid 19, wabunge wa kuteuliwa na rais, ukubwa wa baraza la mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya. Mamlaka mbalimbali zisizokuwa na tija.

Na wewe jiongeze mshenzi wewe!
 

Vivax

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
473
250
Hiyo tozo haieleweki ni ya nini kwenye miamala.
Mimi ndugu yangu amekufa tumetumiwa fedha za mazishi kwenda kuzitoa mpaka tugawane na serikali?
Wakifa wengi furaha kwa serikali. maana Miamala mingi na italeta pesa mingi.
 

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,836
2,000
Dawa ni moja tu: Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima mfano, wabunge wa covid 19, wabunge wa kuteuliwa na rais, ukubwa wa baraza la mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya. Mamlaka mbalimbali zisizokuwa na tija.

Na wewe jiongeze mshenzi wewe!
Kwa kufanya hivyo,tutazipata a trillion tshs?
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,317
2,000
Dawa ni moja tu: Serikali kupunguza matumizi yasiyo ya lazima mfano, wabunge wa covid 19, wabunge wa kuteuliwa na rais, ukubwa wa baraza la mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa na wilaya. Mamlaka mbalimbali zisizokuwa na tija.

Na wewe jiongeze mshenzi wewe!
Ifute posho za wabunge za nini zile hali wanalipwa mishahara.
 

kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,317
2,000
Sheria sio msahafu.wanaopelekewa Sheria wanayo haki ya kuikataa Sheria kama ni kandamizi.
Sheria kama haitekelezeki hata kama imepitishwa na bunge inakuwa ni batili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom