Mdau: Mlitaka Rais afanye nini kuhusu tozo ya miamala ya simu?

Waanze wao kwanza kwa mwaka huu wabane matumizi hakuna kutembelea magari ya gharama waishi maisha kama ya kwetu sisi then mwaka wa pili walete sasa hizo tozo tutatoa kwa moyo mkunjufu. Sio tunabanwa kwenye tozo wao kutwa viguu na njia wapo safarini wanakula posho hapo hatutaelewana
 
Hatukatai hizi tozo,waangalie ukubwa wa tozo.mfano anaetuma 10000 wangechukua (500)tu hadi anayetuma200000. 2000 kwa 210000 hadi 600000 (2500) kwa610000 hadi 1,000000 (3000)kwa 1,001000 na kuendelea
 
Katika awamu hii ya sita hakuna jambo ambalo linapaswa kupongezwa kama utulivu, hekima na maarifa aliyoyaonyesha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi hiki ambacho alipitia magumu kama Rais wa Nchi kwa kupambana na mtikisiko wa kiuchumi kutokana na janga la korona ambalo ni kwa Dunia nzima kila mahali ni kilio.

Hivi kweli Watanzania wenzangu tunakubalije kuchezewa akili na watu ambao kwao hakuna jema katika Nchi yetu wao wanaona mabaya tu basi kiasi cha kuwa wapingaji wa kila jambo na wapinzani wa muda wote hata kama Serikali inafanya mazurii kiasi gani.

Rais alishatuweka wazi kuwa uchumi wetu ulishuka na sababu iko wazi kabisa kutokana na janga hili la corona , licha ya kwamba serikali muda wote imejitahidi kupambana ili kuhakikisha uchumi mwetu unakuwa imara. Hili tu la Rais Samia kusema wazi ni dalili tosha ya kuonyesha ni kwa namna gani sisi kama Watanzania tunapaswa kuwa sehemu ya kuhakikisha tunashiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu licha ya changamoto zilizopo ambazo ni kwa Dunia nzima.

Serikali ina vyanzo mbalimbali vya mapato vya ndani na vya nje kama mikopo lakini unadhani ni salama zaidi kuliongezea Taifa deni katika kipindi hiki cha mdororo wa kiuchumi wa kidunia? Ndio maana tunapotakiwa kushiriki katika kulipa kodi ya mshikamano kupitia tozo hizi za miamala na katika mafuta lazima tujiulize maswali matatu muhimu .

Swali la kwanza “ Kwa nini tozo hii kwa wakati huu? “ leo hii uchumi umeshuka na dunia inalia kuna dhambi gani kuwa na tozo itakayochagiza maendeleo katika Taifa letu tena ni maendeleo kule vijijini ambako tuliopo mijini tumekuwa tukipokea simu za changamoto kila uchao, sasa kwanini simu hizi zisipungue angalau kwa kuwapa nafuu na wenzetu wa vijijini.

Swali la pili “ Tozo hizi zinatumika wapi na zinamnufaisha nani na zitatumikaje? “ Hapa ni muhimu sana kupaelewa kwani moja kati ya njia ya kujipatia maendeleo kwa nguvu zetu wenyewe ni kulipa kodi au kupitia tozo kama hizi za mshikamano ambapo serikali imeshatuweka wazi ni kwa ajili ya maendeleo au shughuli za kijamii maji, afya, elimu , barabara vijijini pamoja na nishati vijijini . Ni nani asiyetambua ni kwa kiasi gani wananchi walioko pembezoni huko wanavyopata shida ya barabara , suala la nishati na maji jambo ambalo kwa sasa serikali imeamua kutumia njia ya moja kwa moja kutatua changamoto hizi kwa kuanzisha kodi mahususi kwa ajili ya changamoto hizi ili ziwe historia.

Swali la tatu “ Mimi ninayekatwa ni kwa kiasi gani nitaathiriwa na tozo hizi kuliko athari ambazo ningezipata kwa kuwa mchoyo wa kuwachangia ndugu zangu kijijini kupitia serikali ili angalau niepushe madhara yatokanayo na kukosa barabara , kukosa maji na umeme bila kusahau vitendea kazi katika huduma za afya. Ni wakati sahihi kwa Watanzania kuamini katika uwezo wetu wa kujijenga kiuchumi na sio kulalamika kwani hakuna wa kutupa msaada bure usiokuwa na msharti ambayo yatakuwa mwiba na mzigo mzito kwa vizazi vijavyo.
Naomba kutoa rai kwa watanzania tusiisaliti Nchi yetu kwa dhambi ya ubinafsi ambapo madhara yake ni makubwa sana. Wewe uliyejaaliwa hicho kidogo hebu tamani kuwa sehemu ya mageuzi ya kiuchumi katika Taifa lako.

Hivi kweli tunamini kabisa kwamba wafanyakazi na wafanyabiashara wakubwa ndio watubebe kiuchumi kama Taifa ? kiasi ambacho hata tu kuchangia 300 mpaka 10,000 au 16,000 tunaona ni mzigo mkubwa ambapo tunatambua fika ndg zetu wafanyakazi wao kila mwezi wanakatwa kodi na bado wanakatwa tena kwenye matumizi katika ongezeko la thamani?

Natambua hoja ya rasilimali za nchi kuwepo na uwekezaji lakini je hatuzioni shule kila kata na elimu bila malipo ? je hatuzioni hospitali za rufaa kila mkoa, hatuzioni hospitali za wilaya, vituo vya afya kila kata na zahanati kila kijiji? Je hatuwaoni watu wa REA kila kijiji na kitongoji? Hatuzioni barabara kila wilaya kwa nchi nzima? Je kweli hatulioni bwawa la Mwl Nyerere na Mradi wa Reli ya kisasa? Hivi kweli hatuzioni ndege za ATCL?

Jamani Serikali inafanya mengi tena makubwa lakini kama kweli tuna nia njema na tunaiona dhamira ya Rais Samia na awamu hii ya sita tuchapeni kazi na tushiriki kulipa kodi ili tupige hatua na daima tutambue Watanzania Hakuna maendeleo yanayokuja bila maumivu na siku zote Mvumilivu hula mbivu.

TUMUUNGENI MKONO RAIS SAMIA ANA DHAMIRA NJEMA KATIKA TAIFA LETU.

Ni mimi mpita njia

Kamshamura Kuku Magu Dedede
Rais kasema na yeye ameona ni kubwa sana andaa andiko lingine.
 
Hatukatai hizi tozo,waangalie ukubwa wa tozo.mfano anaetuma 10000 wangechukua (500)tu hadi anayetuma200000. 2000 kwa 210000 hadi 600000 (2500) kwa610000 hadi 1,000000 (3000)kwa 1,001000 na kuendelea

Na Hilo ndilo linakwenda kutizamwa, Mwalimu Nyerere alisema ni lazima tuchukue kodi lakini kwa wakati ule alisema kwa sasa sichukui toka kwao kwakua hawana kitu, maana yake ni kwamba serikali itazingatia hali za wananchi
 
Mama umeongea vizuri sana kwenye kukusanya, vipi kwenye matumizi na vyanzo vipya visivyo na mawaha.

Mmepanga bajeti ya 2020/2021 zaidi ya 33t, Sasa kwenye matumizi ya kawaida ni zaidi ya 20t na matumizi ya maendeleo ni zaidi 13t inakuja kuona matumizi ya kawaida ni 3× ya matumizi ya maendeleo maana yake nini serikali ina matumizi mengi yasiyoenda moja kwa moja kwenye maendeleo zaidi ya kulipa mishahara,posho na Mambo mengini Sasa je kwa namna hiyo ndio mmekuja kutaka nyongeza ya pesa kwenye matumizi yenu ya kawaida? Kwa gharama ya jasho la walala hoi?

Vyanzo vipya vya mapato ina maana ubunifu na mawazo yenu yameishia kwenye tozo na Kodi kandamizi? Mfano kwanini tusitumie PPP kwenye kuwekeza vyanzo vipya itakavyoleta mapato zaidi pasipokutumia jasho la mlala hoi i.e summer beach parks kwenye pwani yetu, migodi kwenye madini yetu, wazo Kama la badamoyo likaboreshwa tutapata pesa nyingi sana na ajira pia kusisimua uchumi

Kutengeneza sera na sheria rafiki kwa uchumi na uwekezaji ili kuvuta zaidi uwekezaji utakakaochochea uchumi na mzunguko wa pesa ili kupunguza kubana Kodi mpaka kwenye maeneo yanayoumiza hali za wananchi
Kwa kumalizia mlituambia tuko uchumi wa kati ina maana umedondoka kwa miezi 3, je ile style ya kununua madege cash vipi au ndio ile report magumashi ya BOT imekuja kuwastua kuwa hazina hakuna hela mkaamua mje na mkakati wa kutunyonya
Jamani muwe na huruma watanzania wengi ni masikini, vijana hawana ajira hakuna wakuwasemea maana wabunge wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi, CCM ipo busy kupiga propaganda sio kutoa majibu ya matatizo
 
Hatukatai, ila tozo zilizowekwa hazilipiki. Mitandao wenyewe wameona ada iwe 8000 kwa muamala wa milioni moja. jamaa na tozo zao juu yake wanaongeza zaidi ya 8000. Narudia zaidi ya 8000, unaenda makato zaidi ya mara mbili kwa muamala,hata ilipoongezwa ile ya benk haikuenda hivo. Its too much. Raia tunalipa kodi nyingi sana kama Value added Tax. Zitumike vzur na kila jambo litakuwa sawa.
 
Ningekuona wa maana Sana ungesema mishahara ya wabunge,wakuu wa mikoa na wilaya ma RAs,DAS,DED ipunguzwe kwanza na posho zao,ili tuwe wamoja kuliko hicho unachotetea.
 
Afanye nini ?
Kwamba hii Kodi ni muhimu kwa maendeleo ?
Je unajua kwamba huenda hizi Tozo zikapunguza watuamiaji hence kukosa hata walichopata mwanzo ?

 
Wasikilize maoni ya wadau kwanza ,wananchi wanaochangia hiyo tozo ndio watoe maoni yao wanataka iwe vipi ,hatukatai tozo ila iwe reasonable , maendeleo ni muhimu sana ila yasiwaumize wananchi na pia yasiathiri uchumi.

Yaani kutoa Tsh elfu 10 unakatwa Tsh 2000? Really? Makato ni makubwa sana!! Serikali ibanane na makampuni ya simu kuchukua kodi zaidi kwenye yale makato yao maana wanapata faida kubwa sana!!
 
Tukipunguza milioni mbili kwa wabunge 376 tunapata sh ngapi? Mara miaka mitano?
Tukiondoa milioni moja kwa Kila DC na DED katika wilaya 126 za TANZANIA nzima Mara 12 Mara miaka 5 tunapata sh ngapi?
2000000 Mara 126 Mara 2 Mara miezi sitini,tunapata sh ngapi? Wewe mleta bandiko? Piga hesabu hapo.
 
Back
Top Bottom