LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,496
- 3,389
Pole Bwana LiverpoolFC .
Mkubwa,
KUMEKUCHA TENA.
NIPe ripoti mipango inaendaje...
Natambua kuwableo ndio siku maalum ya kumpumzisha baba yetu mahala pa salama, nazidi kumsihi Mungu alisimamie suala hili mkamalize salama.
Naamini utatujuza maendeleo.
Kila la heri mkubwa.
Wacha tu Mkuu wangu!
Pole kipenzi.
Nilikuwa mbali.
Pole sana
Mkuu pole sana kwa matatizo. Mungu awape nguvu na faraja
Pole sana mkuu Liverpoolfc; ynwa.
Pole sana mkuu, sisi na wpenzi wote wa LiverpoolFC tupo pamoja nawe katika hiki kipindi kigumu cha maombolezo
Naaaam! Nashukuru sana Mkuu!
pole sana mkuu Mungu azidi kuwatia nguvu
Pole sana swahiba. Nasikitika ndo naiona hii habari. Mungu aendelee kuwapa moyo wa subira. Tafadhali nifikishie salamu za rambirambi kwa shemeji yetu.
Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa amani. Amina.
Mkubwa nakwambia haya yalitokea halafu sikuwa na nambari yako ya simu kwani zile vimeo vyote nilivyokuwa nazo wamepita nayo watoto wa mjini nimesahau kuweka lock gari hapo town nikakuta wameinyatia na kwenda nazo.
Na kunipa wakati mwingine mgumu wa kuwapata marafiki wangu wakubwa kama wewe! Kwa kifupi kama thread toka kwa PakaJimmy inavyojieleza ni ndivyo ilivyo Asprin Mzee wangu huyu ametutangulia mbele ya haki majira husika na hivi ndiyo naelekea huko nyumbani kuanua tanga ndugu tulioafikia ya kwamba ni leo. NiPM nipate nambari yako Mkuu!
Asante sana!