Mdaiwa HESLB, Unaikumbuka hii toka kwa Lowassa?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
51,974
114,281
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa,amesema iwapo atachaguliwa katika nafasi hiyo, atahakikisha kwamba serikali yake inawafutia mikopo wanafunzi wote wa elimu ya juu waliowahi kukopeshwa kwa ajili ya masomo ya vyuo
vikuu.

Lowassa anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro jana.
 
Lowassa is finished!

Lowassa alikuwa anatoa ahadi za ajabu ajabu mpaka wananchi wakamuona ni tapeli tu.

Huwezi kuwatapeli Watanzania wengi kwa njia ya ahadi ambazo hata wewe unafahamu ni utapeli ili wakupe tiketi ya kwenda kufisadi zaidi maliasili zao.

Wahenga walisema, ukiumwa na nyoka hata jani likikugusa unakimbia.

Lowassa alishawafisadi sana Watanzania wengi kwa sasa hata maneno yake wanayakimbia.
 
Lowassa is finished!

Lowassa alikuwa anatoa ahadi za ajabu ajabu mpaka wananchi wakamuona ni tapeli tu.

Watanzania wengi huwezi kuwatapeli kwa njia ya ahadi ambazo hata wewe unafahamu ni utapeli ili wakupe tiketi ya kwenda kufisadi zaidi maliasili zao.
Ahadi za kilimo cha umwagiliaji wa mibuyu dodoma ilikua ni ahadi ya ajabu au sio ajabu?

Ahadi ya tanzania ya viwanda ni ya ajabu au sio ajabu?.

Ahadi ya kuwafanya malaika wawe mashetani ni ya ajabu au sio ya ajabu?

Hayo yote na mengina ya ajabu ajabu aliyasema Lowassa?
 
MsemajiUkweli post: 16328531 said:
Lowassa is finished!

Lowassa alikuwa anatoa ahadi za ajabu ajabu mpaka wananchi wakamuona ni tapeli tu.

Watanzania wengi huwezi kuwatapeli kwa njia ya ahadi ambazo hata wewe unafahamu ni utapeli ili wakupe tiketi ya kwenda kufisadi zaidi maliasili zao.
Hebu tuache ukasuku, kuna kashfa kubwa za ufisadi zilizofanywa na serikali ya CCM, unapomrefer lowassa kama fisadi basi ni bora uweke record sawasawa, hadi anajiuzulu uwaziri mkuu ni kiasi gani kilikuwa kimeishalipwa kwa Richmond na serikali? Maana baada ya kutoka mkataba ukahamishwa kinyemela ukapelekwa DOWANS.
Pili hebu tuwekee uhusika wake na ufisadi mwingine otherwise wewe ni muimba mipasho huna la zaidi
 
Ahadi za kilimo cha umwagiliaji wa mibuyu dodoma ilikua ni ahadi ya ajabu au sio ajabu?

Ahadi ya tanzania ya viwanda ni ya ajabu au sio ajabu?.

Ahadi ya kuwafanya malaika wawe mashetani ni ya ajabu au sio ya ajabu?

Hayo yote na mengina ya ajabu ajabu aliyasema Lowassa?
Kama ahadi ya kwenda kuchunga ng'ombe Monduli imemshinda unadhani angeweza kufuta madeni ya Watanzania?

Mwambieni kwanza atimize ahadi yake ya kwenda kuchunga ng'ombe kabla ya kuanza kufanya kazi za Katibu Mkuu wa CHADEMA.
 
Siku zite mabadiliko huletwa na wasomi ni sheria na katiba ambayo inawafunga wanafumzi kupata haki yao. Katiba ambayo inaipa nguvu CCM hivyo wasomi wamekosa haki yao ya msingi ya kupata elimu bure kwa kuwa CCM inashinda kwa nguvu ya katiba ya nchi hii. Sasa kama wanata haya mabadiliko waliganie katiba ya wananchi irudishwe mezani sio ile katiba iliyopitishwa kinyemela.
 
Hebu tuache ukasuku, kuna kashfa kubwa za ufisadi zilizofanywa na serikali ya CCM, unapomrefer lowassa kama fisadi basi ni bora uweke record sawasawa, hadi anajiuzulu uwaziri mkuu ni kiasi gani kilikuwa kimeishalipwa kwa Richmond na serikali? Maana baada ya kutoka mkataba ukahamishwa kinyemela ukapelekwa DOWANS.
Pili hebu tuwekee uhusika wake na ufisadi mwingine otherwise wewe ni muimba mipasho huna la zaidi
Wewe acha unafiki na unyumbu!

Unakumbuka ulivyoandika hivi;
Kama mabadiliko hayatapatikana CCM tutayatafuta nje ya CCM,kwanza nakuomba uondoe hizo Roho za hofu,za kitumwa tena za kishetani zinazokufanya uone kuwa bila CCM Tanzania hatuendi,siyo Masiya kwamba lazima atoke ukoo wa Daudi,tunahitaji mabadiliko ambayo hatutaweza kuyapata ndani ya CCM.
PILI kwa nini Lowassa? mwaka 1995 mwalimu Nyerere alimkataa kwa sababu ya ukwasi mkubwa aliokuwa na,kumbuka hakuwa mfanyabiashara Bali Mtumishi wa serikali. Leo wapambe wake mnasema tuhuma tu kama walivyosema wapambe wake mwaka 1995, Nyerere aliwajibu wale mwaka 1995,na sisi tunawajibu nyinyi 2015,mke wa kaisari alituhumiwa ugoni,baada ya uchunguzi ikabainika si kweli,lakini Kaisari akamuacha akisema mke wa Kaisari hatakiwi kutuhumiwa, Tunarudisha heshima ya taasisi ya Raisi Tanzania,Raisi wetu hatutaki atuhumiwe. Tuna watu millioni 45 hatuwezi kupata clean(si clean ya Mr Clean wa mwaka 1995)Mwenye uwezo,dhamira safi,nia thabiti,ya kutuongoza hadi tumpe mtuhumiwa wa ufisadi?
narudia kusema mnatunyanyasa,mnatudhalilisha, hamtutendei Haki maana mnatudharau kutuletea corrupted person watanzania zaidi ya millioni 45.
Unakumbuka msemo huu"show me your friend and I all tell you what kind of a person u are" na Lowassa we nu kazungukwa na Rosti tamu(epa,RICHMOND),Mzee wa vijisenti,mama wa mboga ya sh millioni 10,Karamagi ,God forbid mmelogwa na nani jamani???
Kwenye thread hii;
 
Alikuja Kahama akaahidi ukiwa na mbuzi 2 watakuwa 20,ukiwa na baisikeli itabidilika kuwa pikipiki,mwenye pikipiki atapata gari...mwenye hiace atapata basi...mwenye kirikuu atapata lori...zungusha mikono......Pumbavu kabisa.
 
Wewe acha unafiki na unyumbu!

Unakumbuka ulivyoandika hivi;

Kwenye thread hii;
Of course naukumbuka sana, ni kweli na alituhumiwa na wakati wote hakuwahi kukanusha wala kutoa maelezo ya uhusika wake katika hizi tuhuma, ukizingatia yeye kama Waziri mkuu ni symbol ya utendaji wa serikali iliyoko madarakani ambayo iligubikwa na ufisadi.
Amefungua chapter ingine ameeleza uhusika wake na mhusika mkuu na ameichallenge serikali ambayo imewapeleka mahakamani akina Yona na Mramba na yeye apelekwe mahakamani serikali imegwaya, hata kujiuzulu kwake amesema alijiuzulu ili kuinusuru serikali iliyoko madarakani isianguke kwa kashfa ya Richmond .
Tuliomsikia tukamuelewa na JK kimya hakumpeleka mahakamani, sasa na wewe uliomshikia bango tupe maelezo maana kauli yangu si msahafu, na wala huendeshwi kufikia maamuzi kwa kauli yangu , hebu mwaga ushahidi wako kuonyesha hasafishiki
 
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa,amesema iwapo
atachaguliwa katika nafasi hiyo, atahakikisha kwamba serikali yake inawafutia mikopo
wanafunzi wote wa elimu ya juu waliowahi kukopeshwa kwa ajili ya masomo ya vyuo
vikuu. Lowassa anayeungwa mkono
na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro jana.
Halafu wewe ni moja ya nyumbu mlimpinga Lowassa kwa hoja ila upumbavu mliouvaa...?
 
Lowassa is finished!

Lowassa alikuwa anatoa ahadi za ajabu ajabu mpaka wananchi wakamuona ni tapeli tu.

Huwezi kuwatapeli Watanzania wengi kwa njia ya ahadi ambazo hata wewe unafahamu ni utapeli ili wakupe tiketi ya kwenda kufisadi zaidi maliasili zao.

Wahenga walisema, ukiumwa na nyoka hata jani likikugusa unakimbia.

Lowassa alishawafisadi sana Watanzania wengi kwa sasa hata maneno yake wanayakimbia.
Fake kama zipi
 
Ahadi za kilimo cha umwagiliaji wa mibuyu dodoma ilikua ni ahadi ya ajabu au sio ajabu?

Ahadi ya tanzania ya viwanda ni ya ajabu au sio ajabu?.

Ahadi ya kuwafanya malaika wawe mashetani ni ya ajabu au sio ya ajabu?

Hayo yote na mengina ya ajabu ajabu aliyasema Lowassa?
Watu wengine niwakuhurumia tu...vinginevyo utapata shida mkuu
 
Nitayafunga Majizi Na Mafisadi Yaani Nitalala Nayo Mbele Tu Hivi Kama Nilikuwa Natumwa Halafu Sasa Niwe Nakutuma!!! Waziri Wa Ujenzi Akalale Kwenye Madaraja

Lugumi Kwasasa Tu Anaitoa Jasho Serikali Na Sukari Ndiyo Bhalaa Ila Ukweli Ccm Imeoza Na Inanuka.
Rais Tunataka Kuona Akitekeleza Ahadi Moja Baada Ya Nyingine
Bila Kujali Sura Rangi Kabila Dini Chama
Na Yote Mengine Ila 2020 Najua Siyo Mbali Ni Kumuomba Mungu Atupe Pumzi Ila
Wafanyakazi Wako Hoi
Povu Linawatoka Sukari Haionekani

Lugumi Kinyemela Anafunga Vifaa Kwenye Vituo Vya Police Halafu Ukimya Umetanda Tu
Hakuna Kauli Ya Serikali
 
Back
Top Bottom