MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
- Thread starter
- #21
Umafahamu vipi kama kapauka?Polepole kapauka jaman
Umefikia hitimisho kwa kuangalia picha hii au? Kama ni picha, unafahamu ilipigwa lini?
Umafahamu vipi kama kapauka?Polepole kapauka jaman
Neno haki ni pana sana kiasi kwamba kile ambacho wewe unadhani ni haki kwa watu wengine siyo haki na kile unachodhani siyo haki kwa wengine ni haki.Amani haipatikani kwa mdahalo,pia haipatikani kwa mikesha ya kinafiki ya maombi. Amani Tanzania itadumu haki ikitendeka Oct 25. Bila haki ni vurugu tu Zanzibar na Tangayika.
Hawa wanaenda kujadili AMANI tu na sio UKAWA sasa agenda ya ukawa imetoka wapi labda wawe na kiherehere waende nje ya mdahalo..
Mdahalo wa watu wanaofanana
Halafu wamepanga kiujanja sana, Hao wote ni makada wa CCM, Getrude Mongela anawakilisha wanawake, Joseph Butiku(Wazee), Humphrey Polepole(Vijana). Star Tv kikiwa ndio kitengo chao rasmi cha Propaganda, wamegundua Mkikimkiki wa Uchaguzi hauna watazamaji tena, Twaweza ilishashtukiwa, sasa wamebadili gear, lakini imegoma mapema.
lakiwosha yaani wewe huoni huo mchezo hapo, ngoja nikupe darasa kidogo hapa, ili ugundue kitu.
1/Hao wote ni makada waandamizi wa CCM waliopo kwenye timu maalum ya kampeni ya CCM inayojulikana kama Jukwaa huru(Mongella(wanawake), Butiku(wazee), Polepole(Vijana)).
2/Toka lini Amani ikadumishwa kwa kufanya midahalo? Kuna sababu gani ya msingi ya kuwaweka watanzania kwenye wasiwasi wa kupoteza Amani katika kipindi hiki?
3/Kwanini waongeaji wakuu wawe ni watu wenyewe mlengo mmoja tu wa kisiasa tena katika kipindi hiki?
4/Toka lini Polepole akawa mtetezi wa Amani wakati kila mara amekuwa live kwenye Tv akiipigia kampeni CCM kwa kutumia Propaganda chafu dhidi ya UKAWA zenye kuchochea chuki na ubaguzi?
Umesababisha nicheke. Bora hata waseme wapiga kampeni wa magamba kwenye tv kuliko hilo neno mdahaloWanatumia gharama kubwa watu wanajua ni mechi baina ya simba na yanga, wanakuja wanakuta ni yanga wenyewe wamejigawa mara mbili yani team A na team B.
Mimi nashangaa sana juu ya watu katika maandalizi ya midahalo. Kwa nini hufanya Midahalo ikiwa wahusika wote wana msimamo mmoja? Kwa nini wagombea Urais na hata Ubunge ndio wasipewe nafasi za Mdahalobadala yake wachukue watu wanauzungumzia siasa tu za porojo kunyoosheana vidole wakati haibadilishi kitu pasipo wao kujua kitafuata nini katika Utawala ujao? Je kweli wanayajua ya Magufuli ama wanaweka matumaini kama walokuwa nayo wakati JK akiingia madarakani!..
Wataalam wa siasa walisema kuwa mwanzo wa kuwepo vyama vingi sii ushindani wa Kulia (Marekani) na Kushoto (Urusi) bali watu kutokubaliana na sheria mama za kikatiba ambazo zilihitaji mitazamo na mwelekeo mpya. Na katika kupambanua umuhimu wa mabadiliko hayo kikatiba ndio kukaundwa vyama vya Liberal ambavyo vilipingana na sheria mama inayolinda maadili na Utaifa wa wananchi wake (Conservatives).
Sasa kama tulianza na Ujamaa na Kujitegemea na ikiwa ndio chimbuko la Utaifa wetu, ikaundwa miiko na maadili yake, changamoto za kubadilisha mambo hayo kikatiba ndipo hutokea kuundwa kwa vyama vingine kupingana na mwelekeo uliopo. Kundi jingine likiendelea kulinda misingi ile ile iloyolizaa Utaifa wao sio habari za ugonvi wa Warusi na Wamarekani juu ya mambo yao ya kutawala.
Maadam sisi hatufungamani na yeyote juu ya misimamo yao na kwa maslahi yao ni muhimu sana kupambana katika majukwaa ya kisiasa na kudadavua marekebisho ya kikatiba juu ya mwelekeo wa Taifa letu bila kupoteza Mila, desturi na Tamaduni zetu muhimu katika kujitambua.
hiyo lazima niwepoMdahalo utarushwa moja kwa moja (Live) na kituo cha Star TV.