Lowassa kipao mbele chake namba moja Elimu, namba mbili Elimu na namba tatu elimu.
Magufuli yeye kipao mbele chake Viwanda, Viwanda Tanzania nzima.
Wote hao juu wanaomba kazi kwetu, sisi ndio mabosi wao. Wametuambia watatufanyia hayo tukiwapa ridhaa ya kutuongoza.
Sasa tujadili yupi kati ya hao atakaye weza kutuvusha. Je Elimu itawezekana? Viwanda vitawezekana?
Nondo zenu zitasaidia sana kutushawishi sisi ambao bado atujaamua tumpigie kura nani.
Karibuni kwa mjadala wa maslai mapana ya Tanzania yetu. Mungu ibariki Tanzania, Ibariki Africa