Elections 2010 Mdahalo kupitia TBC1 jimbo la Kigoma Kusini

Very shallow!

Kwa taarifa yako wengi wetu hapa tunapigania ukombozi wa kweli... Ukinichukua leo nikapige kura kuna wagombea wawili ambao ni Dr. John P Magufuli (CCM) na mwingine yeyote isipokuwa Dr Slaa wa Chadema nitampigia Dr Magufuli kwa sababu ninaheshimu mchango wake na wala si chama anachotoka

Hee huyu katokea wapi soma tena na tena utajua nilikuwa na maana gani.Usipende kukimbilia key board soma kwanza halafu jibu wacha ujinga.
 
Kwenye mdahalo wa wagombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini uliorushwa na kituo cha TBC1 jana usiku,mgombea ubunge wa NCCR-Mageuzi kwa kiasi kikubwa alimfunika yule gabachori wa Chadema.
Wadau mliupimaje ule mdahalo?

Kwa Chama kama cha NCCR Mageuzi, hata Slaa siku akihamia hapati kura tena!
 
iwapo 20% tu ya wat wakiwa na mawazo km haya basi nchi inaweza kutengamaa..........
Very shallow!

Kwa taarifa yako wengi wetu hapa tunapigania ukombozi wa kweli... Ukinichukua leo nikapige kura kuna wagombea wawili ambao ni Dr. John P Magufuli (CCM) na mwingine yeyote isipokuwa Dr Slaa wa Chadema nitampigia Dr Magufuli kwa sababu ninaheshimu mchango wake na wala si chama anachotoka
 
Nani asiyejua kuwa huyu mgombea wa NCCR amelelewa na kukuzwa na CHADEMA,mpaka hivi majuzi alipojiondoa? Umaarufu na umahiri wake CHADEMA ina mchango mkubwa!
 
hata akishinda wa Nccr Mageuzi poa, akiwa wa DP ni poa, kwangu ili nchi ikombolewe ni lazima kuwe na mageuzi/mabadiliko. kisha mambo mengine yatakuja.
nchi hii hatuheshimiani kwakuwa kuna genge la watu linalojiona limeumbwa kutawala, hili genge liko ccm.
tunahitaji mabadiliko kwanza , kisha mengine Tutazidishiwa.
 
Ndo maana Zitto alisema kuwa atamuunga mkono kijana huyu hata kama hayuko Chadema.
 
hata akishinda wa Nccr Mageuzi poa, akiwa wa DP ni poa, kwangu ili nchi ikombolewe ni lazima kuwe na mageuzi/mabadiliko. kisha mambo mengine yatakuja.
nchi hii hatuheshimiani kwakuwa kuna genge la watu linalojiona limeumbwa kutawala, hili genge liko ccm.
tunahitaji mabadiliko kwanza , kisha mengine Tutazidishiwa.

Heshima kwako nguvumali,

Haya ndiyo maneno ninayotaka kusikia habari za kusifia chama badala ya kutazama uwezo wa mtu yamechangia kuirudisha nchi yetu nyuma.CCM imekuwa ikitumia njia hii kuwadanganya wananchi kiasi kwamba ikafika mahali wakiweka mgombea mbovu bado alikuwa akichaguliwa bahati mbaya CHADEMA wameiga ujinga wa CCM.
 
yule bwana wa chadema hana takwimu kabisa kwa kitu ukilinganisha na wa nccr ambaye alikuwa akijibu kwa takwimu.

najua hoja hii si nzuri kwenu,na wengi mliangalia,mnafahamu nini kinaongelewa.
ni kweli,hapa ni kumsifia mtu yeyote wa chadema hata kama amevurunda.
Mgombea wa Chadema jimbo la Kigoma Kusini oyee!

Uko sahihi, yule bwana analijua jimbo analotaka kugombea kwa kila hali, jiografia, uchumi, miundombinu etc. Anajua matatizo yao anajua anataka kwenda bungeni kufanya nini.

Ningekuwa Kigoma kusini Ningempa kura yangu, tunahitaji wabunge wengi wa namna ile baada ya mika mitatu atakuwa Zitto Kabwe mwingine.

Ni hazina kubwa.
 
Bana eeh!! Kama wewe uliona si ulete critics zako tuchambue!!

By the way hata akishinda wa NCCR sawa tu , alimradi si dudumizi CCM.
 
Kuna thread ilipostiwa jana during mdahalo na ilisema hivyo na hakuna aliyelaumu wala kukandya... That is the fact!!! Kafulila was like another zitto....

Tangu midahalo ianze, nimeona ule wa kigoma kusini kama one of the best kwasababu hata yule jamaa wa chadema alikua mzuri lakini kafulila was next to none
 
Bwana nilicheki ule mchakato mmh ama kweli vijana waongea. Walikua jamaa wawili mmoja wa CHADEMA na Mwingine wa NCCR, all these guys were very competent. Walikuwa vizuri sana and they were very young.

Kingine kilicho nishangaza huko Kigoma kusini ni jinsi wananchi wa kule walivyokuwa na constructive questions. Wale jamaa sijui wamesoma wapi maanake walikuwa wanahit points kwenye maswali yao. Kila aliyeuliza swali awe mzee ama kijana aliuliza swali la msing. Mfano kuna mzee mmoja aliuliza swali kuhusu uhaba wa elimu ya uraia jimboni mwao.

Generally i was so impressed with those guys.

mimi pia nilinote hii kitu.wananchi wa kigoma wako very informed na wanaonyesha wanauchungu na nchi yao
big up sana kwao
 
[SIZE=+0]kigoma[/SIZE]
[SIZE=+0]kigoma mjinji[/SIZE]
1. Peter joseph serukamba-------ccm
2 .khamis r. Kwezi--------------------demokrasia makini
3. Fatma saadat kinguti-----------cuf
4. Shukuru venance kondo---------dp
5. Mandela daniel ntaondenga----tadea
6 .ally khafani mleh-----------------------chadema
7. Juma khafani mirembe---------------umd
8. Miseke shabani maranda--------- chausta
9. Mvano ramadhani juma------------sau
10 .hamis r mdida--------------------------udp
11. Hafsa musa ramadhani ---------nld
12 .johari rashid---------------------------tlp
13. Zena hemedi-----------------------------afp
14. Said chomba baruani-------------nra
15. Digio ahmad hamis----------------updp
16. Asia juma khairala---------------appt maendeleo

[SIZE=+0]kigoma kusini[/SIZE]
1. Muslin haiderali rajabali-----chadema
2. Philip john fumbo---------------------dp
3. Mvano rashid ramadhani--------nra
4. Zabibu mrisho kaliza--------------umd
5. Mwito juma kharallah-----------sau
6 .haziz hassan---------------------------chausta
7. Suleiman said msanu----------jahazi asilia
8. David kafulila---------------------nccr mageuzi
9. Kiffu gullamhussein shaban---ccm
10. Mwajuma maliki--------------------updp
11. Optatus likwelelile------------cuf

[SIZE=+0]kigoma kaskazini[/SIZE]
1. Omari musa mkwaruro---------cuf
2. Mfaume h. Mfaume---------------appt-maendeleo
3 .maua shauri kamana-----------jahazi asilia
4. Lembo fulgence robinson---ccm
5. Zitto zuberi kabwe-------------chadema
6. Agostino peter mbolegwa---sau
7. Said hussein-------------------------umd
8. Hamis fadhil kiswaga---------nra
9. German m mlete-------------------dp

[SIZE=+0]kasulu mjini[/SIZE]
1. Machali moses john----------nccr mageuzi
2. Jumanne issa ntkana--------nra
3. Fatuma khamis ntagurat---dp
4. Rashid seif kaduguda----------cuf
5. Ishmael luyagaza-------------chadema
6 .hamis rashid mgani------------sau
7. Neka raphael neka-------------ccm
8. Phares gowe hubanje-------appt maendeleo
9. Nestory seswa ntahondwa ------tlp

[SIZE=+0]kasulu vijijini[/SIZE]
1 .buyogera a. Zaituni ------------nccr mageuzi
2. Nsanzugwanko, daniel n ----ccm
3 .gidion jeremia soti ----------------dp
4 .thadeo gaudence lukinisha-chadema
5 .ally juma kikali-----------------------appt maendeleo
6 .ruheta daud hussein --------------cuf


hivi vyama vingi vilizaliwa kigoma? Au ni mpango mkakati wa kuchakachua kura!
 
Wakati nasikia sauti tu nilidhani ni zito anaongea kumbe kafulila. Ananikumbusha mrema wa arusha. Tatizo dogo anaonekana kazidi kiherehere ndio maana slaa alimtosa. Ila ni mzuri wa hoja. Yeyote kati yao akipata haitaleta tofauti maana ni wajuzi na wanajiamini
 
Uko sahihi, yule bwana analijua jimbo analotaka kugombea kwa kila hali, jiografia, uchumi, miundombinu etc. Anajua matatizo yao anajua anataka kwenda bungeni kufanya nini.

Ningekuwa Kigoma kusini Ningempa kura yangu, tunahitaji wabunge wengi wa namna ile baada ya mika mitatu atakuwa Zitto Kabwe mwingine.

Ni hazina kubwa.

ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom