sizungumzii mapenzi ya Zanzibar kuungana na bara; ninachosema ni kuwa Wazanzibar wanaweza kwenda nje ya Muungano (na inapaswa kuwa hivyo mapema zaidi) lakini ni wao wanaojidanganya kudhania kuwa wanaweza kuishi na kufanikiwa bila bara. Sisi bara tunaweza kuishi na kufanikiwa bila Zanzibar wao hawawezi.
Mkandara,
Nakubaliana nawe kuwa wanachofanya ZNZ ni kutishia ili matakwa yao yaongezeke.
Imefika mahali hakuna sababu ya kuwabembeleza. Tumejitahidi Pan Africanism unfortunate we have wrong partner.
Msimamo wangu ni kuwa tuidai Tanganyika, si kwa kutaka serikali 3 au mkataba bali kuuvunja kabisa.
Hadi leo hatujaona kampeni ya kutaka kuvunja Muungano ikianza... hakuna aliyejitokeza kusema Wazanzibar walioko kwenye serikali au utumishi wa MUungano waachie ngazi
Mkandara,
..Ikiwa watagundua mafuta au gesi basi hawatatutegemea. vinginevyo nakuhakikishia watatafuta kila namna waendelee kuwa pamoja na Tanganyika.
..kuhusu utalii, mapato ya Tanganyika ktk sekta ya utalii ni around shilingi trilion 1.4, wakati Zanzibar wanaingiza around bilion 163.
..kukumbusha tu, katika bajeti hii ya juzi ofisi ya makamu wa raisi imetengewa kitita cha shilingi bilion 32 mahsusi kwa ajili ya Zanzibar. kabla ya hapo ZNZ waligoma kulipa sh bilion 40+ ambalo lilikuwa deni la tanesco.
nijuavyo mimi katika karne ya 13 Zanzibar iliwa ni Empire na ikiitwa Zenji Empire, hapajatokea empire nyingine yoyote ndani ya africa yote,,sasa wakati huo hata neno tangnyika hakuna, halikuwepo na wala hathubutu mtu kujinasibu kuwa ilikuwepo tanganyika,, tanganyika katika historia ilizaliwa baada ya Berlin conference ambapo kama mataifa mengine ya afrika yaligaiwa mipaka na wazungu ili yatawaliwe na tanganyika ikaangukia ndani ya mikono ya wajerumaji chini ya Germany East Africa Company pamoja na kenya mnamo mwana 1890,,,,na kwa wakati huo Zanzibar ni dola kubwa kushinda madola yoyote africa na wala africa nzima kwa maana ya bara hakukuwa na nchi isipokuwa Egypt nyengine zote zilikuwa ni kingship or kingdoms ndogo ndogo zilizoongozwa na makabila hata neno tangnyika lilitolewa na wajerumani baada ya kuripoti serikali yao tanga manake hadi dar salama wakati huo ilikuwa sehemu ya Zanzibar na pwani yote hadi kilwa sasa ukisema hakuna muda Zanzibar haikuwahi kutegemea bara itakuwa unachekesha na wala hujui usemalo. tanganyika haiwezi kuifikia Zanzibar hata kwa asilimia 10 kama hufahamu waulize wazee wa zamani wakitangnyika wanajua hivyo,,manake historia ya tanganyika baada ya uhuru nyerere aliipiga marufuku ili watangyika wasijue asili yao wapi na badala yake wakawa wanasomeshwa ya kupigania uhuru nyerere, kinyengetile basi.
JokaKuu
Mambo ya Muungano yana mapato na matumizi.
Hili haliwekwi wazi. Ngapi zinaingia kama mapato na ngapi zinakwenda kwa matumizi.
Hizo ni nyeti za serikali. Ulalamishi unaanzia hapo.
Deni la Tanesco ni deni la kibiashara na lina mkataba. Anaekiuka mkataba, sheria inachukua mkondo wake lakini Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar kila kitu kinafanywa ni siasa.
Wananchi tunaachwa kwenye mataa, wajanja wanakula nchi. Wananchi wanalishana kasumba na udaku.
nijuavyo mimi katika karne ya 13 Zanzibar iliwa ni Empire na ikiitwa Zenji Empire, hapajatokea empire nyingine yoyote ndani ya africa yote,,sasa wakati huo hata neno tangnyika hakuna, halikuwepo na wala hathubutu mtu kujinasibu kuwa ilikuwepo tanganyika,, tanganyika katika historia ilizaliwa baada ya Berlin conference ambapo kama mataifa mengine ya afrika yaligaiwa mipaka na wazungu ili yatawaliwe na tanganyika ikaangukia ndani ya mikono ya wajerumaji chini ya Germany East Africa Company pamoja na kenya mnamo mwana 1890,,,,na kwa wakati huo Zanzibar ni dola kubwa kushinda madola yoyote africa na wala africa nzima kwa maana ya bara hakukuwa na nchi isipokuwa Egypt nyengine zote zilikuwa ni kingship or kingdoms ndogo ndogo zilizoongozwa na makabila hata neno tangnyika lilitolewa na wajerumani baada ya kuripoti serikali yao tanga manake hadi dar salama wakati huo ilikuwa sehemu ya Zanzibar na pwani yote hadi kilwa sasa ukisema hakuna muda Zanzibar haikuwahi kutegemea bara itakuwa unachekesha na wala hujui usemalo. tanganyika haiwezi kuifikia Zanzibar hata kwa asilimia 10 kama hufahamu waulize wazee wa zamani wakitangnyika wanajua hivyo,,manake historia ya tanganyika baada ya uhuru nyerere aliipiga marufuku ili watangyika wasijue asili yao wapi na badala yake wakawa wanasomeshwa ya kupigania uhuru nyerere, kinyengetile basi.
Nonda,
..ZNZ hawachangii ktk mapato wala matumizi ya serikali ya muungano.
..hata yale malalamiko kwamba TRA inakusanya fedha ZNZ na kuzileta D'Salaam yamethibitika kuwa si ya kweli.
..pesa zote zinazokusanywa na TRA ZNZ zinabaki hukohuko visiwani.
..YES, deni la Tanesco ni la kibiashara, lakini hata siku moja suala hilo haliamuliwi mahakamani kama ulivyo utaratibu. mara zote ZNZ hugoma kulipa kwa visingizio mbalimbali, halafu Tanganyika huamua kuwalipia. kuna kipindi Tanesco ilikuwa chini ya management ya makaburu ambao waliamua kuwakatia umeme wa-ZNZ.
. Nonda, kuna ushahidi wa research iliyofanywa na Prof.Teddy Malyamkono na wasomi wenzake kuchambua utegemezi wa ZNZ na ukwepaji wa majukumu yake ktk muungano. Wasomi hao wameandika kijarida kuhusu suala hili.
..mwisho, nasimama tena kusema muungano wa Tanganyika na ZNZ uvunjwe.
At last, umefungua macho,umeona!
How do we do that?
Hiyo sasa ndio iwe kauli mbiu.
Kichwa cha habari za makala.....Tanganyika,Tanganyika, Tanganyika
Na tupeane fikra, vipi tutafika hapo tunapotaka. Kupata Tanganyika yetu. bila kuvishwa joho au koti la muungano.
Sasa mshawishi pacha wako, MJJ badala ya kuipa coverage kubwa Zanzibar sasa, ianze kuidai au kuifufua Tanganyika.
Tena aache huu msamiati wa Bara/ Tz bara.
Hata Muungano kama ulivyo tutumie jina lake la asili. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Wachina wanasema safari ya maili elfu,huanza kwa kupiga hatua ya kwanza/mwanzo.
Hongera Nguruvi3.
JokaKuu
Iliwekwa thread juu ya Jussa Kumtukana/kumdhalilisha Sitta.Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-18.html#post3071438
Hii ripoti inayotajwa na Jussa, Prof. Teddy ameigusia katika kufikia hitimisho la utafiti wake/wao?
Mimi napata tabu kuamini kuwa Zanzibar wanaweza kugoma tu kutochangia au kulipa kile walichokubaliana na Tanganyika kifanyike. Lazima kuna kitu kimejificha au kinafichwa hapa.
Lakini leo nikubali hitimisho la Prof. Teddy kuwa Zanzibar ndiyo tegemezi au inayonufaika na Muungano/ inapata faida.
Sasa tuone upande mwengine wa hoja, Tanganyika inaibeba Zanzibar(inaipa faida Zanzibar) na kwa hivyo, Tanganyika inajiingiza hasara/ inapata hasara na inaendelea kufanya hivyo.
Kuna hoja ya kuwa Zanzibar wanang'ang'ania muungano. Kama hitimisho la Prof. Teddy ni sahihi basi inaingia akilini kuwa Zanzibar yenye kupata faida(inayofaidika) kung'ang'ania muungano.
Je kwa Tanganyika ambayo inapata hasara kwa nini mbali na umaskini uliopo(inakopa, misaada na ufadhili) inaendelea kuipa Zanzibar faida huku yenyewe inapata hasara, na tuseme,hainga'ng'anii muungano?
Kitu ambacho mimi sikifahamu, au hakiingii akilini ni kwa nini Tanganyika iingie hasara na iendelee kubeba kiroba cha misumari? Je huu si ndio hasa ungefaa kuitwa ung'ang'anizi wa muungano?
Lakini, Hasara yote hii ambayo Tanganyika inapata katika Muungano badala ya kudai kuvunja muungano, inafanya kila mbinu kuleta serikali moja. Pia wanatokea watu wenye mawazo kuwa tudai serikali moja. Je hili ndio suluhisho la kutoingia hasara? Au kukiwa na serikali moja ndio faida itapatikana(Manufaa ya muungano yatapatikana)? Kwa vipi?
Na mfumo huo wa serikali moja utakuwa ni mfumo wa aina ipi ya Muungano?
Mimi nasimama kuwaomba wabunge wa Tanganyika wapeleke Mswada binafsi wa kutaka Zanzibar ifukuzwe katika Muungano. Au wabunge wote wa upande wa Tanganyika (bara) wanabariki mazingaombwe ya muungano unaoutia Tanganyika hasara? Uzalendo uko wapi?
Jamuhuri ya watu wa Zanzibar kwanza ,shengesha baadae!Ngoja waje hapa uone watakavyopiga kelele wasivyopenda kusikia ukweli!!!!
Si ndo hapo sasa kama tuvunje muungano kila taifa lijitegemee siye tubaki na bara yetuAisee yaani huu mjadala huwa hauna mwisho?
Mkuu kuhangaikia maisha yao ni kweli kabisa akili wataipata na kitakachowaongoza ni ule Ukweli wao. wazenji si wanafiki kama sisi wabara. ni waumini na wanaisimamia kweli daima.hawaruhusu kuufunika ufisadi hata kama umetendwa na ahali wake katu hawavumilii. ona sisi tunavyouana wenyewe,mikataba ya ovyo ya enzi za mangungo nchi inaliwa na tulowapa dhamana ya kutukwamua lakini walaaa baridi kabisa roho zetu.acha wende wakaijenge nchi yao sie tubaki na unafiki wetu wa kugawa bure gas yetu na akanti yetu uswiss izidi kunona. dhana ya ipo siku!!!!! Lini hiyo siku???nionavyo mimi ndo na wewe umeling'amua hilo,MM yeye anataka kuupalilia kwa kuonyesha kuwa zenji wananufaika na muungano,lakini mimi naweza kusema wakijitenga watapata akili ya KUHANGAIKIA MAISHA YAO