mfumo uliopo bado ni mzuri tatizo lipo kwa wasimamizi wa mfumo huu,wazazi na mwanafunzi mwenyewe.
Serikali imechakachua elimu kwa kufanya mabadiliko makubwa ya mitaala yasiokuwa na basis,yaani waziri anaibuka na kusema futa masomo flani lakini msingi wa kuyafuta au kuyaongeza haupo.vitabu vimekuwa vikibadilishwa kila kukicha halafu inaavyoonekana kitabu anachosoma mwanafunzi wa dar ni tofauti na kile anachotumia mwanafunzi wa newala.yawezekana kumeruhusiwa vyuo vingi sana vya kufundisha walimu na kwa bahati mbaya inaelekea vyuo hivi havina mtaala inayofanana hivyo mwalimu akihitimu anafundisha jinsi anavyojua kwa ufupi uwepo wa utitiri wa vyuo vya walimu umesababisha aina na viwango vya ufundishaji kuwa utofauti mkubwa sana.
Kudharauliwa kwa fani ya ualimu ni mojawapo ya chanzo cha mfumo wa elimu kuharibika.leo hii mtu akipata daraja la chini form 4 au form 6 anaona kimbilio la kupata ajira ni ualimu, hakuna anayefaulu vizuri na kuchagua ualimu.
Mishahara na maslahi finyu kwa walimu yameshusha tija ya walimu.hakuna mwalimu wa kumalizia topic jumapili au wakati wa likizo,walimu hawana hamu ya kufundisha!
Utitiri wa shule za english media,hii ni biashara kutoka kenya iliyokuja kuangamiza elimu yetu.vishule hivi uchwara vinatumia walimu kutoka kenya ambao hawajajua mitaala ya kitanzania au mara nyingine vinatumia mitaala ya cambridge wakati tupo tz.
Serikali kwa makusudi au kwa kutokujua imeua kabisa shule za serikali na sasa inaelekea kuua vyuo vya serikali.kuvuruga shule kama mzumbe,ilboru,msalato,pugu na jamii yake imetufikisha sehemu tumekosa shule ambazo ni standard,hapa nitolee mfano wa hospitali kwamba mgonjwa aliyeshindikana hupelekwa muhimbili..
Yuko rafiki yangu wa uganda aliniambia wanafunzi kutoka tanzania ndio wanaojaza shule zao za english media kwani waganda wanaprefer shule za serikali kwa elimu bora.
Kiufupi serikali imeshindwa kudhibiti madhara ya utandawazi.leo hii ukikatiza kwenye vituo vya daladala jaribu kuhesabu matangazo ya '''elimu ya sekondari kwa miaka miwili''' yalivyo mengi na hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kuelezea suala hili.
Walimu ni sehemu ya tatizo kwa sababu wanafundisha wasichokipenda na wasichokijua.
Wazazi wa siku hizi hawafuatilii maendeleo ya mtoto shuleni.wazazi hawana muda wa kufundisha watoto wao.wazazi hawashawishi watoto wao wasomee au wapende fani fulani fulani.
Wanafunzi wa sasa wana nyenzo nyingi za kusomea lakini kutwa atakuwa kwenye facebook,video game,kukariri mashairi ya hussen machozi na tamthilia za amerca kusini.hata hivyo vyote hivi sio tatizo iwapo kuna ratiba inayompatia muda wa kujisomea.
Mwisho napenda kupinga hoja ya mwanakijiji kwa sababu bado hatujajua kiukamilifu ni nini hasa chanzo cha kuanguka kwa wanafunzi wetu.
Nashauri ufanyike utafiti katika maeneo yote yanayohusu elimu ili tujue tatizo liko wapi hii ndio njia pekee ambayo ni sahihi na salama ya kubadilisha mfumo wa elimu nchini,hakuna haja ya kudesa kwa wakenya.